Madereva wa mikoani, tabia na utaratibu wa kupaki mabasi sehemu ya chakula chenye bei juu mnaumiza abiria wenye kipato kidogo

Serikali yetu - mamlaka husika tunaomba mtusaidie sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inayozidi kushamiri kila kukicha, hasa kwa wale ndugu zetu wanaosafiri mikoa ya mbali wanapata tabu sana kuhusu masuala ya chakula.

• Dar - - Mwanza
• Dar - - Mbeya
• Dar - - Kigoma
• Dar -- Arusha
• Dar -- Ruvuma

Kuna tabia na utaratibu wa mabasi waliojiwekea bila kuhofia abiria wao, sio rafiki kabisa, wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu sana bila kujali abiria mifukoni mwao/kipato walichonacho. Karibia vituo vyote wanavyopaki hawa madereva unakuta Chakula cha bei ya chini ni kuazia elfu Tsh7000/- hadi elfu Tsh 8000/- na kuendelea, na ukiangalia hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei kwa hiyo, halafu chakula kinakuwa ni kidogo ikiwa mtakuwa watu wawili hamuwezi kushiba.

Jana nilikuwa natoka Dar kuja Mbeya tulipofika sehemu ya chakula, niliongozana na mama mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula bei ya mwisho ni elfu Tsh7000 alikuwa mnyonge sana, na kiasi alichokuwa nacho taslimu alikuwa na elfu Tsh5000 tu, ikambidi anunue soda na biscuit, roho iliniuma sana.

1. Madereva mnadhani kila mtu anapesa ya kununulia hicho chakula cha bei ya juu?

2. Au sehemu mnazopaki kwa ajili ya watu kula ni za viongozi wa ngazi za juu huko serikalini

Ombi langu kwa Serikali tunaomba mtoe tamko/sheria kwa mabasi yote, yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kamilifu ili abiria wote wapate huduma stahiki
bado unakulaaa mahotelin be ba vyakoo nyumbani mkuuu yalematakatakaaa yamelalaaa yanapashwaa unaonayaleo ingia kwenyebasiii

Ushajiuliza vikilala wanapeleka wapi
 
Chakula huwa hakitupwi, ni mwendo wa kukipasha tu, Labda wadudu wazaliqe humo humo ndo wanaweza kukitupa.
 
Halafu unapewa dakika 5 uwe umemaliza kula
 
Kumbuka wao wanakula bure, tena kila mwisho wa mwezi wanapata pesa nzuri kabisa!
 
bado unakulaaa mahotelin be ba vyakoo nyumbani mkuuu yalematakatakaaa yamelalaaa yanapashwaa unaonayaleo ingia kwenyebasiii

Ushajiuliza vikilala wanapeleka wapi
• Wewe huwa unabeba hivyo vyakula,?
• Maana mimi nasafiri sana, lakini huwa sioni watu na hotpot, Labda kama ana mtoto mdogo.
 
Jitahidi uwe unaandaa chakula chako mwenyewe pale unapokuwa unafanya safari ndefu,,, hii itakusaidia sana mkuu ktk kubana bajeti [emoji1431]
• Upo sahihi kabisa mkuu, ubebaji wa vyakula kutoka nyumbani bado ni kero tu, kuna watu safari zao ni zaidi ya siku mbili au tatu.
• point muhimu ni kurekebisa/kushauri mamlaka itoe tamko. Litakalo kuwa na faida pande zote.
 
Kumbuka wao wanakula bure, tena kila mwisho wa mwezi wanapata pesa nzuri kabisa!
Ndo hilo linalo tuumiza sisi maskini, sehemu yenye maslai ya watu wachache, ndo huumiza kiwango kikubwa cha watu wanyonge.
 
Watu bado mnakula vyakula vya njiani? Mimi kabla safari haijaanza nachukua Eet-Sum-Mor na Sprite (500ml). Tukutane mwisho wa safari.
Kasulu na Kaliua , menyu muhogo wa kuchemsha na karanga za kwenye mifuko. Hatari sana...! Upate ya moto! Ukijichanganya ya baridi, ameoba inakuhusu!!!
 
Tatizo ule utaratibu wetu wa zamani wa kuandaa vitu vya safari tumeuacha.
Ni vizuri kujiandalia chakula unachokipenda ili kuondoa usumbufu wenye kuweza kukuletea madhala ya shida za mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.
Lakini ni vizuri kushauri namna iliyo bora hasa ni lishe gani za kisafari zilizo muhimu.
 
Back
Top Bottom