Kuna kitu watu wanaita over expectation of which mimi napingana nacho kidogo...huwezi kuzidi malengo,kama gari imeundwa itembee 240km/h ukizidi hapo(jambo lisilowezekana) hapo tutasema umevuka lengo ila kama upo within basi upo ndani ya malengo!
Siku moja nami niliwahi kupigwa tochi km tano toka chalinze kuelekea Dar, the Isue ni kwamba kibao cha 50 kilikuwepo mwanzo opp na Kanisa la Mtakatifu nani sijui ila cha kumaliza kilin'gooka so hakikuwa kinaonekana...baada ya kuona nalala sana nyuma ya malori nikachomoa...hamadi hawa hapa! Tumesumbuana wee mwishoni wakaniambia nirudi wakanioneshe kibao,ikanibidi nigeuke kwa kuwa ID yangu walikuwa nayo mkononi ila cha kushangaza hawakunirudisha kwenye kibao wakanipeleka Chalinze kituo kikuu cha Polisi. Nimeandikiwa kosa la kuovertake, mwendokasi na la tatu nililichuma pale pale wakati nikiandikiwa ya mwanzo kwa kuwaambia hizo tochi ni mradi wa wakubwa na wanabambikia nazo watu makosa ili hesabu ijae kuepuka kunyanganywa tochi kesho yake!