Madereva wa Subaru Mna Matatizo Gani?

Madereva wa Subaru Mna Matatizo Gani?

Unachosema ni kweli kabisa. Hata mimi wakati mwingine nafikiri labda sijui hizi Subaru ndo watu wanadhani ni sport cars huku kwetu! Sijui! Ila nackia Ulaya watu wanasemaga kuwa madereva wa BMW mara nyingi wanaendesha kipumbavu(labda kwasababu gari zao ni ghali), labda hizi Subaru ni version yao nyingine huku Bongo
Unajua hizi gar zinakula mafuta sana. Ukikimbia ni afadhali una save wese.
 
Aisee zungumza yote nitakuelewa ila sio kwa subaru, naendesha gari ya kawaida toyota hizi nikawa nashangaa sana jamaa yangu ana suburu wrx sti huwa atulii ni migujo tu kila awapo barabani, Wakati fulani alisafiri akaiacha kwangu ile gari aisee..
Nilipoitumia ndani ya masaa kadhaa nikawa ninafujo kuliko hata za jamaa na kujiridhisha nikaitafutia ka safari ka kwenda dar arusha nilijikuta nasafisha kisahani bila ya kutarajia. Kwa hiyo tuwavumilie tu jamaa zetu wenye kuendesha hizo gari zina radha tofauti sana.
 
Tena ukutane na manual 6 speed lazima useme pooo kama umepakiwa
 
Wewe utabaki kuwa ndugu yangu siku moja barabara ya bagamoyo msata ukishapita kiwangwa nikakutana na tochi ya kimagumashi
Uzuri jamaa alikuwa Mwelewa sana akasema hizi sheria zimepitwa na wakati ni sheria za wakati wa mchonga na maland rover yake mpaka leo hii hazijawa uptodated
Gari niliyo kuwa nayo ni speed 240 na hapo nilikuwa naenda 80 BTW speed zinataka hekima na ufahamu ni wakati gani na mahali gani pa kwenda spidi gani

Kuna kitu watu wanaita over expectation of which mimi napingana nacho kidogo...huwezi kuzidi malengo,kama gari imeundwa itembee 240km/h ukizidi hapo(jambo lisilowezekana) hapo tutasema umevuka lengo ila kama upo within basi upo ndani ya malengo!

Siku moja nami niliwahi kupigwa tochi km tano toka chalinze kuelekea Dar, the Isue ni kwamba kibao cha 50 kilikuwepo mwanzo opp na Kanisa la Mtakatifu nani sijui ila cha kumaliza kilin'gooka so hakikuwa kinaonekana...baada ya kuona nalala sana nyuma ya malori nikachomoa...hamadi hawa hapa! Tumesumbuana wee mwishoni wakaniambia nirudi wakanioneshe kibao,ikanibidi nigeuke kwa kuwa ID yangu walikuwa nayo mkononi ila cha kushangaza hawakunirudisha kwenye kibao wakanipeleka Chalinze kituo kikuu cha Polisi. Nimeandikiwa kosa la kuovertake, mwendokasi na la tatu nililichuma pale pale wakati nikiandikiwa ya mwanzo kwa kuwaambia hizo tochi ni mradi wa wakubwa na wanabambikia nazo watu makosa ili hesabu ijae kuepuka kunyanganywa tochi kesho yake!
 
Duuuuu kosa la tatu ndio lilikuwa kiboko
 
Hawatofautiani sana na wa Noah na altezza akili za kuazima wakiwa road
 
Haya ninazamini HZo subaru sijui nin nin mafuta kila kitu kwangu tutoke pale msamvu tuitafute dodoma ntakua na Volvo FH16 ina 610Horsepower au Scania R520 V8 engine 520HP mgongoni nina tani 28 za mzgo..!!!fasta alie tayar af nakutanguliza hata kilomita 1.
 
Sio kwenye public roads.....
Kwahiyo kwenye public roads zinakuwa daladala au?hata ziwe msibani zitabaki kuwa sports cars, sasa basi tuelekeze hizi subaru wapi zinatakiwa kuwa sports cars na wapi hazitakiwi
 
Soma basi uelewe.....nimewaambia wenzio na wewe public road sio za kuendesha kama mko kwenye mashindano. Nendeni kwenye rally ambapo barabara zinafungwa mnashindana mtakavyo sio mnahatarisha maissha ya wengine kwa ulimbukeni wenu.
 
Get serious the car yes but do you have the roads????

Germinate mate
Hajui afanyalo, kupata ka subaru anaona kashakuwa rally driver na ana ruhusa ya ku-rally hata mitaa ya mwananyamala!
 
Aisee zungumza yote nitakuelewa ila sio kwa subaru, naendesha gari ya kawaida toyota hizi nikawa nashangaa sana jamaa yangu ana suburu wrx sti huwa atulii ni migujo tu kila awapo barabani, Wakati fulani alisafiri akaiacha kwangu ile gari aisee..
Nilipoitumia ndani ya masaa kadhaa nikawa ninafujo kuliko hata za jamaa na kujiridhisha nikaitafutia ka safari ka kwenda dar arusha nilijikuta nasafisha kisahani bila ya kutarajia. Kwa hiyo tuwavumilie tu jamaa zetu wenye kuendesha hizo gari zina radha tofauti sana.
Wewe una fujo tu sema hukuwa na uwezo wa kuonyesha fujo zako.
 
Nimejiapiza kwamba siku nikiwiwa kuongeza mke msaidizi baada ya mashauriano na mke mwandamizi basi itanibidi mahari niwe nalipa kwa installments kupitia makosa ya barabarani ikiwa baba mkwe atakuwa Traffic!
[emoji25] [emoji87] [emoji87] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Haya ninazamini HZo subaru sijui nin nin mafuta kila kitu kwangu tutoke pale msamvu tuitafute dodoma ntakua na Volvo FH16 ina 610Horsepower au Scania R520 V8 engine 520HP mgongoni nina tani 28 za mzgo..!!!fasta alie tayar af nakutanguliza hata kilomita 1.

Usiongee tu imradi umeongea
Wewe na fuso lako sijui volvo hata noah inakupita
Kumbuka hizo subaru zina hp hadi 300+ na zikifanyiwa mapping huwezi hata kuisogelea, hata wenye vx nao watapata taabu
Labda dereva awe na hela za njaa na ni mwoga tofati na hapo huwezi kamwe ishinda subaru wrx sti.
 
Mkuu ipo moja uku sub wrx sti ni hatch back ina 750hp sasa balaa lake ni kubwa ina nguvu za ajabu
 
Back
Top Bottom