Madhara ya kuoa Mwanamke ambaye hajasoma na Golikipa ni haya!

Asee hii ilitaka kunitokea kipindi fulani wife anamtoto mmoja.
Wife wangu ni mpole sana na anapenda kufanya kazi hasa akiwa sehemu za misiba au sherehe anajituma mpka unaweza sema huyu ni mfanya kazi nn... kuna ndugu hawamjui na wanajiskia sasa sijui walimuonaje wakaanza kumtuma mara hiki mara kile ikafika muda mtoto hataki kukaa na mimi nikamuita wife tukawa tumekaa kwenye gari akaja ndugu yangu mmoja akamwambia kule kazi haijaisha......
Wife akamuuliza kwani unanionaje mbona kazi nyingi nasukumiwa mimi kwakua namjua wife nikamwambia ndugu yangu hebu tuache tuna maongezi ndio ananipa mkanda maana mimi nilikua na baba zangu na wajomba tunapiga stori nikamwambia wasikuchanganye fanya kwa kiasi hawa watu wanaangalia nani wanamuweza wanampa makazi kibao..... Tulipomaliza msiba kukawa na kakikao na kutambuana basi ndipo nikawatambulisha ndugu kwa mke na mke kwa ndugu ndipo heahima ikaja na wengine walimuheahimu zaidi walipokuja kwangu.....

Ngozi nyeusi tuna shida moja kudharauliana kulingana na nini tunacho ukiona mtu kapoa basi unahisi ni wakumkandamiza wengine wamelelewa hivyo kuwa wapole ila sio wanyonge maana wife kasoma na mbali ya kusoma ni mpambanaji (namshukuru sana Mungu) ila kwenye swala la upole dah hadi nakasirika maana kazidisha na ndivyo alivyo habadiliki japo namsema sana na kumuelekeza tukifika kwa ndugu fanya hiki na hiki ila lazima atakugeuka utamkuta anachakarika kwenye vyombo kupika yaani hadi najiskia vibaya.
 
Kweli mwanamke anatakiwa kulea watoto nyumbani lakini akipata kazi lazima achepuke, akitongozwa na wanaume ishirini lazima atatokea mmoja atamkubalia tu.
 
😄😄
Siku ukipata Stroke au umestaafu au kufukuzwa kazi au kufa alafu umeacha watoto wadogo ndio utajua jinsi ulivyokuwa na mawazo mgando.

Pesa ya Mwanamke inaweza isikusaidie wewe lakini ikasaidia wàtoto wako.
Kuna wale wanaosema ukiwa na 100k na mke akawa na 100k jumla ni 200k ila ndani mnakua na 100k nashangaa sana maana mbona wanawake wana huruma upendo na wanajituma njiu yetu lakini tukiwa wakweli na kuwapenda..... Mimi kuna muda hadi nashangaa watu wapo dunia gani kulalamikia wanawake wakati ukipata wa kufanana nae basi mambo yanaenda na hakuna ubinafsi
 
Mkuu utu na Elimu vitu viwili tofauti, utu unaanzia ngazi ya familia, mfano viongozi wetu si wana Elimu kubwa mbona hawana utu ?
 
Kama mume anaheshimiwa automatically mke ataheshimiwa and vice versa
 
Umbile la mwanamke ni kukaa nyumbani hii ndio asili. Ona kinachotokea baada ya mwanamke kutolewa nyumbani ? Leo wote sisi mashahidi.
Uko sahihi. Ukimfungulia biashara mwanamke ni kama umempa lesseni ya kutafutwa na mabwana wengine. Ataanza kuchepuka mpk ushangae.
 
Kuna chizi mmoja alijichanganya akamfungulia calling point mke wake, enzi hizo watu wengi hawana simu, wanaenda kupiga simu kwenye kibanda Cha soggy doggy, haikuchukua hata mwezi kibanda alikifunga, alivyoulizwa ilikuwaje, alisema Kuna siku alisahau kitu nyumbani akiwa kazini ikabidi aruke chap kurudi kukichukua, akapita calling point kuchukua funguo kwa wife wake, Ile anatokea kapaki kigari chake pembeni Anakuta mbele ya office Kuna ndinga la vx limepaki, kabla hajashuka kwenye kigari chake ikabidi afanye servey kidogo, kupiga jicho dukani Anakuta wife wake anashikwa matako na kibosile flani mwenye Ile ndinga, alitoka mbio akamfurusha yule kibosile na pale pale duka likafungwa, mkewe alikuwa ni zile pisi kali zilizonyooka slay queen, jamaa hawezi kumuacha mkewe lakini kiduka alikifunga, jichanganye uoe Pisi kali halafu umuache aende kazini ndio itakuwa imeisha hiyoo
 
Taikon ktk makala zako toka nikufahamu 2018 kama sikosei. hii makala ulipaswa kuifuta kabisa maana umeandika mambo ya ajabu na ya hovyo sana.

Ulichokiandika mwanaume anaejielewa vizur lazima akupuuze
 
Bado alikuwa mfanyabiashara.
Khadija mpaka anakufa ni Mfanyabiashara.

Vigezo kwa uislamu vipo vitatu.
1. Uzuri wa Mwanamke
2. Mali
3. Dini na nasaba ya mwanamke
Hujajibu swali nililo kuuliza.

Pili, hivyo sio vigezo kwa Uislamu inaonekana huujui Uislamu. Ile hadithi inaongelea kwa kawaida watu huwa wanaoa kwa kuangalia vigezo vya :

1. Uzuri wa mwanamke
2. Nasaba ya mwanamke
3. Mali

Ila Mtume akasema katika hayo yote angalieni dini ya mwanamke kwani Mikono yako haitagusa michangana kwa maana hautaanguka au kupata madhila.

Mama Khadija alipo olewa na Mtume biashara zake alimuachia Mtume na yeye akawa nyumbani.

Jaribu kuwa unasoma na usiwe unasikia au kuokoteza mambo kwa ambao hawajui Uislamu.
 
Elimu ya dunia inachochea Akili ya asili.

Ndio maana Watu wanapelekwa shule.
Hii sio kweli basi hao waitwao au wenye akili wasingekuwa wanafanya mambo yenye kudhuru akili zao. Akili kijana haipimwi kwa kusoma secular itakuwa hujui akili ni nini.

Watu wanapelekwa shuleni sababu ya kasumba na kupata hela tu na nafasi.

Elimu ya dini ndio inafanya mtu kuwa smart na makini zaidi.
 
Kwa sababu Mwanamke naye ni mtu.
Sifa ya mtu lazima afanye kazi.
Vinginevyo labda asiwe mtu.

Moja ya sheria ya Mungu au ya asili ni kufanya kazi kwa mwanaume na Mwanamke.
Swali anafanya kazi wapi na kazi gani ?

Hakuna aliye pinga hilo la kufanya kazi shida mnaona kazi ni za maofisini na kutafuta hela. Hili sio umbile la mwanamke ndio maana kama akili yako inafanya kazi vizuri utaona Kuna faida chache na hasara kubwa mno.
 
Akiwa amesoma na hamna pesa? Unafikiria vitu kibwege sana wife material hapimwi kwa elimu yake. Ndoa sio ajira ya ofisini
 
I hope
Mambo yanawaendea easy huko na mkeo
Mwenye Phd
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…