Madhara ya kuoa Mwanamke ambaye hajasoma na Golikipa ni haya!


Kwani nani anayemtenga mke na mambo ya kijamii au jamii yenyewe ndio inafanya hayo?

Mimi naongea uhalisia wewe unazungumzia hisia zako.
Sio mke tuu hata wewe mwanaume kama huna elimu yoyote na kazi ya maana huna kwenye matukio ya kijamii utafanya yale ya hadhi yako ya Chini.

Hisia na mihemko yako haiwezi badili ukweli kuwa Mke aliyesoma na mwenye kazi na kipato kamwe hawezi kufanana na mke ambaye hajasoma na asiye na kazi.
 
Atakuwa yuko sahihi

Ulitaka kumaanishaje?

Nilitaka kukwambia ndoa za wanawake wasomi zinavunjika kwa sababu wanaume wengi bado wanazile akili mgando za kuabudiwa.

Unyanyasaji, ukatili, ukandamizaji, dhulma ndio Wanaume wa zamani walikuwa nazo.

Fikiria mwanaume(mume) kakosea alafu hataki kuambiwa kakosea, na akiambiwa anasema mkewe hana adabu au mjuaji.

Ndicho hichohicho kinachoendelea hata kwenye siasa. Watawala wanamawazo hayo ya wanaume wa kizamani. Kuwa mwananchi kumkandamiza na akisema anakandamizwa ataitwa mchochezi na mtovu wa nidhamu
 
Unless unatumia kilevi na hapo ulipo una hangover ila najaribu kukuelewesha kwa lugha rahisi sana still hunielewi.

Ukiwa na hela na elimu ukajitenga kwenye mazishi kwamba hubebi jeneza siyo hadhi yako na mkeo akisema kwenye msiba hawezi kupika kwa sababu ana elimu ninyi wote akili hamna,naandika fact jamii za ki-Africa hazijawahi kuishi utaratibu huo unasoma soma vijarida vya weupe unakuja ku-adopt tabia zao kwenye jamii kupitia maandishi yako.
 
1. Umeoa mwanamke mfano mwanasheria Kila siku yeye ndio anakukuta nyumbani saa 3 usiku kwa kigezo alikuwa kwenye vikao. Na hapo wewe ndio unaogesha watoto yeye akirudi ni kulala blaza umeoa au umeolewa?

2. Huyo huyo kaenda kwenye semina na bosi wake huko mkoani tena kwa wiki mbili wanalala hotel/lodge moja na kakuachia watoto. Blaza una uhakika hao watoto ulioachiwa uogeshe ni wa kwako?

3. Blaza huyo msomi kapandishwa cheo ana maokoto kukuzidi na humfikii kwa kipato tena blaza unaelewa kitakachokukuta?

4. Blaza msomi wako ana PhD kiuno anajua kukata kweli?? Wengine raha zetu ni viuno teke teke sio vyeti vya taaluma😆😆

5. Blaza sina shida na msomi wako ila ana udambwi udambwi kwenye sufuria??

Raha ya kuku wa kienyeji mtie limao na tanawizi ya kutosha. 😁
 

Unaandika fact ambayo kwenye jamii haipo.

Mtu akishakuwa na pesa Watu wanamuabudu hata vikazi vya kusugua masufuria hapewi wanapewa wasio na chochote Unazungumzia nini mkuu. Hayo mambo yapi kwenye jamii na kama hujayaona ndio nakuambia yapo Sana.

Wéwe elewa kuwa Kam huna pesa na mkeo ni mama wa nyumbani na hana kazi jamii inavyomchukulia ndio hivyo.
 
🤝🏾 Point tatu chukua wewe!
 
Unaweza kuwa na hoja. Lakini mbona mama zetu wengi humu elimu zao ndio hivyo tena lakini tumefika tulipo fika.
Hicho ni kizazi Cha zamani kabla ya fb TikTok na insta. Kwa sasa mama wengi kuanzia 90 ni mbulula sana
 
🤝🏾 Point tatu chukua wewe!

Huu ni mjadala tuu mkuu.

Hujasikia kauli ya "Tafuta pesa"
Na inafahamika kabisa kuwa pesa inapatikana kwa kufanya kazi.
Pesa inampa mtu heshima ya nje. Sasa mwanamke asiyefanya kazi ambapo ndio kipimo cha utu atapataje heshima ya nje.
Au ndio umesema atapata heshima kupitia mumewe. Kumbuka nguo ya kuazima haistiri
 
Hicho ni kizazi Cha zamani kabla ya fb TikTok na insta. Kwa sasa mama wengi kuanzia 90 ni mbulula sana

Anazungumzia mateka, Watu waliokuwa watumwa wakitumikishwa kwenye ndoa na haki zao kukandamizwa.
Watu ambao hawakuwa na uchaguzi wa kuamua hata mwanaume wa kumuoa ndio anaowazungumzia.
Unaweza kuona aliyetoa hiyo hoja ni mtu wa aina gani
 
Ni kweli lakini Mwanamke msomi na asiye soma ni tofauti Kabisa.
Mwanamke anayefanya kazi na asiyefanya kazi ni tofauti kabisa.
Ni kwel kabisa kikubwa tabia ya mtu tu, anaweza kuwa na kazi akabanduliwa huko kazini na wenzake ,mifano ipo, na anaweza kuwa mama wa nyumbani wahuni wakajipigia ukitoka mifano ipo , hii mambo hainaga mwongozo.
 
Ni kwel kabisa kikubwa tabia ya mtu tu, anaweza kuwa na kazi akabanduliwa huko kazini na wenzake ,mifano ipo, na anaweza kuwa mama wa nyumbani wahuni wakajipigia ukitoka mifano ipo , hii mambo hainaga mwongozo.

Ni sahihi.
Nakupa mfano, mkeo ni mkurugenzi katika kampuni fulani unafikiri ni rahisi kutongozwa hovyohovyo na Watu wa chini yake?

Na hapohapo unamke mwingine ni mama wa nyumbani Unafikiri ni ngumu kutongozwa hovyohovyo?

Wanaume tunajijua wengi wetu ni waoga. Binti akishafikia level fulani hata kumfuata wengi wetu ni waoga.
Wanaomfuata ni Watu wa juu au level zake ambao ni wachache

Ni kama Pyramid.
Kadiri mwanamke anavyopanda juu kimafanikio ndivyo kiwango cha wanaume Wanaomsumbua kinapungua

Mfano unafikiri kumtongoza mwanamke ambaye ni Rais au Waziri ni jambo rahisi?
 
Kwanza nataka nijue ulieandika Habari hii umeoa au lah



Mimi nitaongea kifupi tu hakuna kitu kizuri kwa mwanaume kama kuoa mwanamke ambaye Hana kazi ya kuajiriwa,,na wewe mwanaume ukiwa na kazi au biashara ambayo inakizi mahitaji yenu aise hapo unaenjoy life,,,,


Mimi nimeoa mwanamke muajiriwa Lakini mara kwa mara utanikuta kwa mama ntilie kula mara wife,,kaenda zamu usiku nimebaki mwenyew najifunika ngumi,,mara unajuandalia nguo za kazini mwenyew yani nishida aise mpaka nafikia hatua nasema siku nikiwa na kipato kizuri ntamuachisha wife kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inafikirisha
 

Unapenda utegemezi sio.
Utegemezi ni umaskini sijui kama unajua.
Yaani wanawake milioni 31 wa Tanzania wawe mama wa nyumbani. Nchi hii si itakuwa fukara mpaka basi. Kwa sababu nusu ya rasilimali Watu haitumiki na ni tegemezi.

Fikiria siku umekufa au umefukuzwa kazi, au unaumwa na mkeo amezoea ugolikipa, na hana uwezo wala uzoefu wa kutafuta. Hivi huko si kutafutana maneno. Au ndio ninyi mnategemea ndugu watakuja kuwasaidia wakati mkeo kama angekuwa na elimu na kazi mkasaidizana maisha wala msingefikiria habari za ndugu.

Hivi siku unaumwa unafikiri watoto wako wanakuwa katika hali gani wakiwaza kuwa mzee akidondoka hapa sisi tumekwisha. Hayo huyafikirii.

Haya umemuacha mkeo kama single Mother hawezi kujitafutia na hana taaluma yoyote mingi si ndio mnafanya wanawake waishi maisha magumu ya kunyanyasika huku duniani.

Hivi Mwanamke akiwa na taaluma yake na anafanya kazi hata siku mumeachana Unafikiri atakusumbua hata pesa ya kumtunza mtoto au watoto wako? Au ukifa Unafikiri atasumbua Watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…