Madhara ya kuoa Mwanamke ambaye hajasoma na Golikipa ni haya!

Madhara ya kuoa Mwanamke ambaye hajasoma na Golikipa ni haya!

Muulizeni mleta mada kama ameshaoa na muda gani katika ndoa. usikute analeta nadharia badala ya uzoefu wake katika maisha ya ndoa
 
MADHARA YA KUOA MWANAMKE AMBAYE HAJASOMA NA GOLIKIPA NI HAYA!

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nimeona kuna vijana hapa wanadanganyana na kuwa na mawazo ya kizamani.

Ati wao wataoa wanawake wenye elimu duni na wasiofanya kazi isipokuwa kazi za nyumbani (golikipa).

Sasa kwa ninyi mliofanya maamuzi ninyi sina neno na nyie kwa sababu huo ni uchaguzi wenu.

Wazo hili ni zao la kizamani ambalo msingi wake ulikuwa kwa jamii isiyoamini kama Mwanamke naye ni mtu.

Lakini ujumbe huu nimeandika ni kwa wale ambao bado hawajafanya maamuzi au hawajui wachague kipi kati ya kuoa Mke aliyesoma na anayefanya kazi za taaluma au Mke ambaye hajasoma na ambaye atakuwa mama wa nyumbani.

Yafuatayo ni madhara ya moja kwa moja ambayo utayapata kwa kuoa Mwanamke ambaye hajasoma na ambaye hana kazi yaani mama wa nyumbani;

1. Atakuwa Mwanamke Cheap na wagharama nafuu Kabisa.
Hakuna kazi rahisi kama kutongoza Mwanamke ambaye hajasoma na hana kazi. Ni rahisi kama kunywa uji wa mgonjwa. Yaani shwaaa!

Moja ya vitu vinavyompa mtu thamani kwa dunia ya leo ni Elimu.

Hata wanaume watakaomtongoza mkeo watakuwa Lundo kama siafu wekundu, hawamuogopi, wamuogope kwa kipi hasa! Lakini mdada shule ipo tena anawazidi mpaka wanaume Unafikiri hapo kuna nini.

Mpeleke mkeo ambaye hajasoma na hana kazi yoyote Kwenu siku ukitokea msiba uone jinsi atakavyotumikishwa kwa kusugua masufuria na makazi yasiyo na hadhi. Wakati huo Wake wa ndugu zao wamekaa mguu juu na hakuna kima yeyote atakayewasogelea isipokuwa wao wenyewe waamue.

Jipe hadhi kijana acha woga wa kijingajinga.

Unataka familia yako iwe cheap? Unataka watoto wako wajisikieje wakimuona mama yao(mkeo) akitumikishwa kwa kazi dhalili?

2. Mwanamke kuwa Mnafiki na kushindwa kusimama katika nafasi yake ya mke na Mama.
Mke wako hana elimu alafu hana kazi. Atawezaje kusimamia majukumu yake kama mke na kama Mama?

Mke lazima awe na elimu ya kiwango fulani angalau Diploma kwa zama hizi. Kisha awe na kijikazi au kazi ya kuingiza mapato.

Mke ni Mama wa watoto wako lakini pia ni Mama yako mlezi wakati mwingine.

Lazima uwe na Mwanamke ambaye ataweza kubeba jukumu la kukutunza na kukulea kimwili na kiroho na wakati mwingine kiakili pale ambapo utakengeuka.

Sasa unachukua Mwanamke shule hana, hana kazi, Mwanamke anakuogopa badala ya kukuheshimu kisa hana kipato.

Umekengeuka kidogo hakuna wakukurudisha kwenye mstari.

Nawajua wanaume wengi ambao wao ndio chanzo cha kuvunja nyumba zao kwa kukengeuka kwao. Aidha kutumia vibaya uanaume na ubaba wao vibaya.

3. Mkeo hataheshimiwa na Watu wa nje.

Raha ya mke aheshimiwe. Sio kila siku mke anakondeana kwa kudharaulika.

Binadamu ni kiumbe mwenye dharau Sana.

Kanisani atadharaulika. Mtaani hivyohivyo. Kisa hana elimu wala hana kazi. Yaani yupo yupo tuu.

4. Kugawa Uroda kirahisi.
Ni kweli wanawake wengi hugawa uroda lakini kuna kugawa Uroda kirahisi.

Fuatilia hata jamii yenye umalaya mwingi wanawake wao hawana elimu wala hawana kazi.

Yaani Mwanamke awe mwalimu au daktari au mwanasheria alafu awe Malaya, hiyo sio rahisi.

Ila mkeo akiwa hana elimu jua kabisa hata bodaboda hawamhofii. Yaani mwanaume yeyote anaweza kuruka naye kwa sababu mkeo ni level ya chini ambaye yeyote anaweza kutunda yake.

Lakini Mwanamke mwenye elimu na kipato ni kama Mnazi. Mpaka umpate lazima jasho likutoke na wapandaji huwa wachache.

Fikiria mkeo ni mkurugenzi Unafikiri ni wafanyakazi wake wangapi wana ujasiri wa kumtongoza? Lazima wawe na hofu.

Alafu fikiria mkeo hana elimu yoyote Unafikiri kuna mtu anamhofia kumfuata?
Hakuna!

Sasa mwanamke Watu wanatakiwa Wamheshimu yeye bila hata ya uwepo wako. Sio mkeo aheshimiwe kisa umemuoa yaani ni mke wa mtu. Hapo umepigwa.

Yaani Watu wanakuheshimu tuu wewe ndio maana hawamfuati mkeo lakini ukiwa haupo Watu wanajigaragaza. Lakini Mwanamke akiwa na kazi nzuri na elimu hata asipokuwa na mume anaheshimika na wanaume hujifikiri mara mbilimbili kumfuata.

Yote kwa yote Maisha ni ubatili. Lakini Watu wanachokazana ni kuepuka ubatili wenye maumivu, dharau, majonzi na taabu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Taikon wa Fasihi kweli ni matako wa fasihi

Huu uzi hauna usingekuja hapa kama wewe usingekua masikini

Huu uzi umekujia kichwa ukauandika kwa urefu wa ajabu kilichokusukuma ni umasikini ulio nao

Be rich kiasi kwamba your wife has an option to stay home na kulea watoto wa ukaribu,kwenda kazini kuajiriwa kwa mwanamke ni umasikini mkali wa mume ndio chanzo
 
Muulizeni mleta mada kama ameshaoa na muda gani katika ndoa. usikute analeta nadharia badala ya uzoefu wake katika maisha ya ndoa
Acha mke,hana demu hata wa kuungia maana ni masikini na hajitambui,weak male!

Weak males wanataka strong females wawasaidie majukumu ya kiuchumi!

Mtu kukaa nyumbani kuleta watoto wako huyu masikini anaitwa "goalkeeper" what a dummy!
 
Mtu kujiheshim ni malezi yake tu, elimu yake au kutokua na elim siyo vigezo wapo wasio na elimu kubwa ila wanajisheshimu sana na hao wenye elim huku maofisini watu wanapokezana tu kama wanacheza basket
 
Taikon wa Fasihi kweli ni matako wa fasihi

Huu uzi hauna usingekuja hapa kama wewe usingekua masikini

Huu uzi umekujia kichwa ukauandika kwa urefu wa ajabu kilichokusukuma ni umasikini ulio nao

Be rich kiasi kwamba your wife has an option to stay home na kulea watoto wa ukaribu,kwenda kazini kuajiriwa kwa mwanamke ni umasikini mkali wa mume ndio chanzo

Tatizo la binadamu mliowengi ni wanafiki wa kiwango cha juu.
Sio ajabu hapo una binti na unasomesha kabisa lakini hapa unakuja unaandika vitu vinavyokinzana na matendo yako(unafiki asilia).

Sio lazima mkeo aajiriwe mnaweza fungua makampuni au miradi yeye akawa anasimamia.

Torati, inaposema kufanya kazi inahusu Mwanamke na mwanaume. Hiyo ni amri.

Mkeo anafanyakazi kwaajili yake, familia pamoja na taifa.

Kutaka mwanamke asifanye kazi ni kuongeza umaskini katika jamii na nchi.
Fikiria Wanawake wapo milioni 32 kasoro alafu nusu nzima ya rasilimali Watu hiyo iwe tegemezi. Unategemea nini kama sio umaskini uliopindukia.

Tunapojadili hoja hizi wengine tunajadili kwa marefu na mapana. Wajinga na wenye upeo mdogo wanawaza tuu vitu vidogovidogo kama sijui mke kuchepuka, sijui kukudharau. Sasa kama ni mwanaume bwege kwa nini wasikudharau?

Mnataka Wanawake wasisome na kufanya kazi ili wasijue madhaifu yenu ya ubwege na kutokujiamini?
Wewe kama kweli mwanaume Oa mke Msomi, mwenye kazi au kipato, kisha muongoze ukíweza basi wewe mwanaume.

Sio unatafuta mjinga mmoja asiyejiweza kimapato unamweka ndani alafu unajiita wewe ni mwanaume.
 
Unapenda utegemezi sio.
Utegemezi ni umaskini sijui kama unajua.
Yaani wanawake milioni 31 wa Tanzania wawe mama wa nyumbani. Nchi hii si itakuwa fukara mpaka basi. Kwa sababu nusu ya rasilimali Watu haitumiki na ni tegemezi.

Fikiria siku umekufa au umefukuzwa kazi, au unaumwa na mkeo amezoea ugolikipa, na hana uwezo wala uzoefu wa kutafuta. Hivi huko si kutafutana maneno. Au ndio ninyi mnategemea ndugu watakuja kuwasaidia wakati mkeo kama angekuwa na elimu na kazi mkasaidizana maisha wala msingefikiria habari za ndugu.

Hivi siku unaumwa unafikiri watoto wako wanakuwa katika hali gani wakiwaza kuwa mzee akidondoka hapa sisi tumekwisha. Hayo huyafikirii.

Haya umemuacha mkeo kama single Mother hawezi kujitafutia na hana taaluma yoyote mingi si ndio mnafanya wanawake waishi maisha magumu ya kunyanyasika huku duniani.

Hivi Mwanamke akiwa na taaluma yake na anafanya kazi hata siku mumeachana Unafikiri atakusumbua hata pesa ya kumtunza mtoto au watoto wako? Au ukifa Unafikiri atasumbua Watu.
Wewe sijui unaongea nini,,mimi nmekuambia ukioa mwanamke ambae sio muajiriwa unaenjoy namaanisha anaweza akafungua biashara akawa na msaidizi lakini mda wowote ambapo utamuhitaji unampata lakini sio hivyo unavyowaza wewe et wanawake 31m wote wasiingize kipato

Alafu unaongea nadharia tu nahisi wewe bado hata hujaoa unatusumbua kujibu sisi ambao tunayajua mais

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe sijui unaongea nini,,mimi nmekuambia ukioa mwanamke ambae sio muajiriwa unaenjoy namaanisha anaweza akafungua biashara akawa na msaidizi lakini mda wowote ambapo utamuhitaji unampata lakini sio hivyo unavyowaza wewe et wanawake 31m wote wasiingize kipato

Sasa kuajiriwa na kujiajiri kuna tofauti gani? Kote si ni kufanya kazi?

Embu kuwa Serious
Alafu unaongea nadharia tu nahisi wewe bado hata hujaoa unatusumbua kujibu sisi ambao tunayajua mais

Sent using Jamii Forums mobile app
Afadhali unasema unahisi, hata ulichoandika ni hisia zako tuu hazina uhalisia
 
Kwahiyo wasio na elimu wasiolewe ?

Na tulionana eleimu hatuna kazi tusiolewe? 😅

Kila mmoja atabaki kwenye fungu lake.

Niliandika kwa sababu kuna Watu walikuwa wanapromoti Watu wasioe Wanawake waliosoma na wenye kazi wakatoa madhara yao. Kisha wakatoa faida ya kuoa Mwanamke asiye na elimu wala kazi. Nami nimewakumbusha tuu madhara ya kuoa wanawake wasio na elimu na magolikipa.

Najua lengo la Watu wa aina hiyo ni kutaka kuirudisha dunia nyuma.
Wanatoa mifano ya wazazi wetu ambao walinyimwa haki nyingi ikiwemo ya kusoma ati ndio wanalinganisha na dunia ya sasa ambayo imetoa haki kwa kila mtu
 
Back
Top Bottom