Hapa leo umepotoka kabisa na kuwadharau wanawake wa nchi yetu, mama zetu hata mama yako najua hajasoma, pamoja hajasoma alikuzaa, kakukuza, umekuwa, umesoma na kuelimika, huoni leo unamtusi vibaya hata mama yako mzazi aliyekuzaa, kukulea na kupata elimu na elimu hiyo ndio unarudisha haya majibu kwa mama zetu, hiyo elimu uliyopata hukufanya vema kuwasema hivi wanawake au wamama zetu wengi hawakusoma, umewatusi, wamekuzaa, wamekulea, wamekusomesha, leo unawajibu hivi, sikutegemea, ila kumbe elimu ndio imekufanya umejisahau na kuwa kipofu wa maisha hivi?
Nakupa elimu kidogo ushtuke, hakuna mwanamke hataki kupata elimu au kupata kazi nzuri au kufanya biashara nzuri awe na kipato kizuri ili awe na maisha mazuri, sbb ni nyingi huchangia hali unayoona wanawake wetu wengi wako hivyo, sbb kubwa hasa ni umaskini, ufukara na wakati mwingine wamepoteza wazazi wao wakiwa wadogo sana, hivyo ni bora uone uchungu na madhila yao waliyopitia na kuwa na hali ngumu mno kimaisha, ila bado wanaolewa na kuzaa na kulea watoto na kuwasomesha katika hali hiyo hiyo, hivyo kuwabeza na kuwadharau ni mbaya sana, hakuna mtu anapenda kuwa tegemezi, au maskini au akose elimu bora bali ni maisha tu, umaskini wetu, kama wewe hali yako ni nzuri piga magoti chini mshukuru Mungu sana na waombee wanawake hao wawe na hali nzuri ila usiwabeze hata kidogo, hiyo ni dhambi mbaya sana.
Usitumie elimu yako kama fimbo kuwadharau wanawake ambao hawakusoma, hiyo ni dhambi kubwa sana sana na inatia uchungu, waache hao ndio mama zetu, dada zetu, wake zetu, mashemeji zetu hata kama hawana elimu, wanaolewa sana tu, ndio dunia ilivyo, usiwazidishie machungu ya kuwakebehi, dharau au kuwang’ong’a, waache hao wanwake zetu, ni wetu sisi, Mungu alichonipa nitagawana nao hao hao, elimu sio sbb ya kuwa toa ubinadamu wao kana kwamba hawafai kuolewa,, waache waache hao wanawake ndio wetu sisi wengine, tunawapenda sana, tutawajali sanaaa, tutawahudumia sanaa, na kuwatunza mno na mahaba kwao hayatapungua hadi milele na milele, elimu isiwe chanzo cha kuwaona sio wanawake wasio kamilika kuolewa au binadamu ambao hawajakalimika, sisi tunawaona ni wanawake 100% kama wanawake waliosoma, waache kabisa.
Nakushauri, elimu uliyopata usirudie kuwaongelea hawa wanawake au mama zetu ambao hawana elimu au kipato, waache kabisa, Mungu atakupa adhabu mbaya, hao ni watu wa Mungu, Mungu anajua kuliko wewe na hali zao anajua, waache, waache, waache
Mama na dada zetu mjisikie na amani na furaha na upendo, haijalishi una elimu duni au huna, still nyie ni mashujaa na mnaendeleza dunia hii na Mungu ndio kafanya hivyo, Mungu yuko pamoja nanyi, baadhi ya vijana elimu imewapotosha kabisa na kuwafanya vipofu hawajui wametoka wapi na kuenda wapi, na kujisahau na kuanza kutusi walikotoka, leo umeharibu sana.