Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

bora kurudi Eden.
tule vyakula vya asili.
kila chakula kutoka viwandani vina madhara.
Lakini naipenda Mountain dew!
 
naunga mkono hoja,
mimi kuna jino limejazwa nikinywa soda unaona kama ndo maumivu yanaanza leo.
 
Iliyobaki ni fasting kila kitu watasema ni tatizo.
 
KUNA mjadala mkali unaendelea kuhusu vinywaji baridi hususani soda, baada ya utafiti wa hivi karibuni kuonyesha kuwa soda inaweza kuwa na madhara zaidi kiafya kuliko hata sigara!

Hii inaweza kuwa changamoto nyingine kubwa kumkabili binadamu katika masuala ya afya, kwani makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake bila kutaja madhara ya vinywaji vyao.

Soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi (obesity), ugonjwa wa ini (liver disease) na hata tabia za vurugu (violent behavior). Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, unywaji wa vinywaji baridi mara kwa mara unachangia tabia ya ugomvi kwa asilimia kati 9-15!

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa nchini Marekani, soda huwekwa ‘fructose’ (sukari) nyingi ikiwa katika mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala anasema: ” Ninaposema kunywa soda ni hatari sawa na mtu anayevuta sigara au pengine zaidi, siyo jambo la kutia chumvi, bali ndiyo ukweli halisi”.

Dk. anaendelea kusema kuwa unywaji wa soda kwa njia nyingi ni mbaya kuliko uvutaji wa sigara, ila kutokana na kampeni kubwa ya matangazo inayofanywa na makampuni haya, inafanya vinywaji hivi vyenye sukari kuonekana havina madhara kwa watu wasio na hatia, hasa watoto wetu!

SABABU KUBWA YA KUDHARAU SODA
Unayesoma makala haya kuhusu madhara ya soda kwa mara ya kwanza bila shaka utakuwa unashangaa na kujiuliza; soda ina ubaya gani? Kwa mujibu wa Dk. Mercola, hakuna sababu yoyote ya kuendelea kunywa soda, labda ujikute uko katikati ya jangwa na hakuna kinywaji kingine isipokua soda!


Kiafya, unywaji wa soda au vinywaji vingine baridi vyenye ‘fructose’ una madhara. Unywaji wa kiasi cha kopo moja tu la soda kila siku, utakuongezea uzito wa mwili wa kilo 10 kila mwaka na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (diabetes) kwa asilimia 85!

‘FRUCTOSE’
‘Fructose’ ni kirutubisho kilichomo ndani ya sukari na kiwango kinachowekwa wakati wa utengenezaji wa soda ni kingi kuliko kawaida. Inaelezwa kuwa miaka 100 iliyopita, Mmarekani mmoja alikuwa akitumia kiasi cha gramu 15 ya sukari (fructose) kwa siku, tena kwa kula matunda. Miaka 100 baadaye, (yaani hivi sasa), robo ya Wamarekani wote wanatumia kiasi cha gramu 135 (kutoka 15) kwa siku, tena kwa kunywa soda!

Ulaji wa sukari (fructose) kiasi cha gramu 15 kwa siku hauna madhara kiafya, labda uwe na ugonjwa wa kisukari (high uric acid levels). Hata hivyo, kwa kula sukari mara kumi zaidi ya kiwango cha gramu 15 kinachokubalika kiafya, inakuwa ndiyo chanzo cha unene wa kupindukia na magonjwa mengine hatari yanayoibuka mwilini (degenerative diseases).

Utafiti unaonesha kuwa vinywaji vingi baridi vina sukari nyingi kuliko wastani unaotakiwa. Badala ya kuwa na asilimia 55 ya ‘fructose’ na asilimia 45 ya ‘glucose’, vingi vina asilimia 65 ya ‘fructose’, ikiwa ni karibu asilimia 20 zaidi na inavyotakiwa.

Utafiti zaidi umeonesha kuwa ‘fructose’ ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la ugonjwa wa ini kwa watoto wengi nchini Marekani, ingawa hawatumii kilevi chochote (alcohol). Inaelezwa kuwa ‘fructose’ huleta madhara kwenye ini kama inavyofanya pombe.
 
Ama kweli hawa wazungu si wema sana.
Mzizimkavu, kuna huyu mwingine ameibu kwa kasi kama ile hawa mafisadi ya kusema Ari mpya,Nguvu mpya na Kazi mpya na naona kinywaji chake kinanyweka kwa kasi kweli kweli AZAM.
Nae ni jamii moja kwa mtazamo wako wa haraka haraka.
 
Teh teh teh teh teh kwa mambo kama haya huwa najigongea mwenyewe tano.
Mie nina miaka zaidi ya 7 niliacha kunywa soda,juice zoote artificial,natural wanazouza waswahili na kutia KK,kunywa pombe,mayai ya kisasa n.k

wengi sana huniita mshamba, mara msabato sijui mlokole.

Namshukuru sana mwalimu wangu LEE alitujuza na kutuasa mengi sana juu ya afya zetu pindi amalizapo kutu train zoezi.
 
Nilijaribu kuacha kunywa Soda nikashindwa for now Nanywa Seven up Fidodido na Sprite Zenye Rango Rango Nimeacha
 
Nadhani kuna vitu vingi tu tunavitumia ila hatujui madhara yake, sasa nitaaza kupunguza unywaji wa hivi vitu.
 
Nisaidien madhara ya sigara kiundan!marafiki zangu akiwemo bosi wangu ni wavutaji sana!Naomben pia hints/tips za kuacha!
 
Nadhani kuna vitu vingi tu tunavitumia ila hatujui madhara yake, sasa nitaaza kupunguza unywaji wa hivi vitu.
Ukianza tabia ya kuacha kutumia vitu basi ujue vingi vinafuata ikiwemo vyakula kuku akiwemo, watasema hadi mahindi yanayopandwa na mbolea za kisasa n.k nawashauri mle tu kila mtu atakufa iwe leo au kesho
 
Back
Top Bottom