Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

KUNA mjadala mkali unaendelea kuhusu vinywaji baridi hususan soda, baada ya utafiti wa hivi karibuni kuonesha kuwa soda inaweza kuwa na madhara zaidi kiafya kuliko hata sigara!

Hii inaweza kuwa changamoto nyingine kubwa kumkabili binadamu katika masuala ya afya, kwani makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake bila kutaja madhara ya vinywaji vyao.

Soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi (obesity), ugonjwa wa ini (liver disease) na hata tabia za vurugu (violent behavior). Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, unywaji wa vinywaji baridi mara kwa mara unachangia tabia ya ugomvi kwa asilimia kati 9-15!

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa nchini Marekani, soda huwekwa ‘fructose' (sukari) nyingi ikiwa katika mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala anasema: " Ninaposema kunywa soda ni hatari sawa na mtu anayevuta sigara au pengine zaidi, siyo jambo la kutia chumvi, bali ndiyo ukweli halisi".

Dk. anaendelea kusema kuwa unywaji wa soda kwa njia nyingi ni mbaya kuliko uvutaji wa sigara, ila kutokana na kampeni kubwa ya matangazo inayofanywa na makampuni haya, inafanya vinywaji hivi vyenye sukari kuonekana havina madhara kwa watu wasio na hatia, hasa watoto wetu!

SABABU KUBWA YA KUIPIGA KIBUTI SODA

Unayesoma makala haya kuhusu madhara ya soda kwa mara ya kwanza bila shaka utakuwa unashangaa na kujiuliza; soda ina ubaya gani? Kwa mujibu wa Dk. Mercola, hakuna sababu yoyote ya kuendelea kunywa soda, labda ujikute uko katikati ya jangwa na hakuna kinywaji kingine isipokua soda!

Kiafya, unywaji wa soda au vinywaji vingine baridi vyenye ‘fructose' una madhara. Unywaji wa kiasi cha kopo moja tu la soda kila siku, utakuongezea uzito wa mwili wa kilo 10 kila mwaka na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (diabetes) kwa asilimia 85!

‘FRUCTOSE'
‘Fructose' ni kirutubisho kilichomo ndani ya sukari na kiwango kinachowekwa wakati wa utengenezaji wa soda ni kingi kuliko kawaida. Inaelezwa kuwa miaka 100 iliyopita, Mmarekani mmoja alikuwa akitumia kiasi cha gramu 15 ya sukari (fructose) kwa siku, tena kwa kula matunda. Miaka 100 baadaye, (yaani hivi sasa), robo ya Wamarekani wote wanatumia kiasi cha gramu 135 (kutoka 15) kwa siku, tena kwa kunywa soda!

Ulaji wa sukari (fructose) kiasi cha gramu 15 kwa siku hauna madhara kiafya, labda uwe na ugonjwa wa kisukari (high uric acid levels). Hata hivyo, kwa kula sukari mara kumi zaidi ya kiwango cha gramu 15 kinachokubalika kiafya, inakuwa ndiyo chanzo cha unene wa kupindukia na magonjwa mengine hatari yanayoibuka mwilini (degenerative diseases).

Utafiti unaonesha kuwa vinywaji vingi baridi vina sukari nyingi kuliko wastani unaotakiwa. Badala ya kuwa na asilimia 55 ya ‘fructose' na asilimia 45 ya ‘glucose', vingi vina asilimia 65 ya ‘fructose', ikiwa ni karibu asilimia 20 zaidi na inavyotakiwa.

Utafiti zaidi umeonesha kuwa ‘fructose' ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la ugonjwa wa ini kwa watoto wengi nchini Marekani, ingawa hawatumii kilevi chochote (alcohol). Inaelezwa kuwa ‘fructose' huleta madhara kwenye ini kama inavyofanya pombe. juma: JE NI KWELI SODA INA MADHARA KULIKO SIGARA?
 
Dr MziziMkavu inawezekana kabisa soda zina madhara katika mwili wa binadamu lakini kwa maoni yangu madhara ya kunywa soda kamwe hayawezi kufikia madhara makubwa yanayosababishwa na uvutaji wa sigara....Sigara nomaaaa zinaua kwa kiwango cha juu sana lakini bado zina wapenzi wengi sehemu nyingi duniani. Wengine unaweza kuwasikia wanakohoa kupita kiasi mpaka wanatia huruma lakini bado wamo tu!!!!
 
Sigara mbaya sana kuliko soda kama shida ni fructose ni vyema kufanya mazoezi(lengo ku-burn calories) kila siku kama ni mpenzi wa soda ila ukivuta sigara sana hata ukifanya mazoezi vipi hauwezi kutibu mapafu yalianza kuaribika na moshi wA sigara!
 
Mkuu ni kweli kabisa. Ila mimi nasherekea kutimiza mwaka mmoja sasa tangu nia che kunywa soda na juice za wakina Azam. Ilikuwa mwaka jana mwezi wa nane mwanzoni nilipo stop kunywa soda na sasa nisha zoea kabisa. Hizi soda ni noma
 
Kunywa Soda ukiwa unajua Madhara yake

15.jpg

KUNA mjadala mkali unaendelea kuhusu vinywaji baridi hususani soda, baada ya utafiti wa hivi karibuni kuonyesha kuwa soda inaweza kuwa na madhara zaidi kiafya kuliko hata sigara!

Hii inaweza kuwa changamoto nyingine kubwa kumkabili binadamu katika masuala ya afya, kwani makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake bila kutaja madhara ya vinywaji vyao.

Soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi (obesity), ugonjwa wa ini (liver disease) na hata tabia za vurugu (violent behavior). Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, unywaji wa vinywaji baridi mara kwa mara unachangia tabia ya ugomvi kwa asilimia kati 9-15!

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa nchini Marekani, soda huwekwa ‘fructose’ (sukari) nyingi ikiwa katika mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala anasema: ” Ninaposema kunywa soda ni hatari sawa na mtu anayevuta sigara au pengine zaidi, siyo jambo la kutia chumvi, bali ndiyo ukweli halisi”.

Dk. anaendelea kusema kuwa unywaji wa soda kwa njia nyingi ni mbaya kuliko uvutaji wa sigara, ila kutokana na kampeni kubwa ya matangazo inayofanywa na makampuni haya, inafanya vinywaji hivi vyenye sukari kuonekana havina madhara kwa watu wasio na hatia, hasa watoto wetu!

SABABU KUBWA YA KUDHARAU SODA

Unayesoma makala haya kuhusu madhara ya soda kwa mara ya kwanza bila shaka utakuwa unashangaa na kujiuliza; soda ina ubaya gani? Kwa mujibu wa Dk. Mercola, hakuna sababu yoyote ya kuendelea kunywa soda, labda ujikute uko katikati ya jangwa na hakuna kinywaji kingine isipokua soda!

Kiafya, unywaji wa soda au vinywaji vingine baridi vyenye ‘fructose’ una madhara. Unywaji wa kiasi cha kopo moja tu la soda kila siku, utakuongezea uzito wa mwili wa kilo 10 kila mwaka na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (diabetes) kwa asilimia 85!

‘FRUCTOSE’
‘Fructose’ ni kirutubisho kilichomo ndani ya sukari na kiwango kinachowekwa wakati wa utengenezaji wa soda ni kingi kuliko kawaida. Inaelezwa kuwa miaka 100 iliyopita, Mmarekani mmoja alikuwa akitumia kiasi cha gramu 15 ya sukari (fructose) kwa siku, tena kwa kula matunda. Miaka 100 baadaye, (yaani hivi sasa), robo ya Wamarekani wote wanatumia kiasi cha gramu 135 (kutoka 15) kwa siku, tena kwa kunywa soda!

Ulaji wa sukari (fructose) kiasi cha gramu 15 kwa siku hauna madhara kiafya, labda uwe na ugonjwa wa kisukari (high uric acid levels). Hata hivyo, kwa kula sukari mara kumi zaidi ya kiwango cha gramu 15 kinachokubalika kiafya, inakuwa ndiyo chanzo cha unene wa kupindukia na magonjwa mengine hatari yanayoibuka mwilini (degenerative diseases).

Utafiti unaonesha kuwa vinywaji vingi baridi vina sukari nyingi kuliko wastani unaotakiwa. Badala ya kuwa na asilimia 55 ya ‘fructose’ na asilimia 45 ya ‘glucose’, vingi vina asilimia 65 ya ‘fructose’, ikiwa ni karibu asilimia 20 zaidi na inavyotakiwa.

Utafiti zaidi umeonesha kuwa ‘fructose’ ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la ugonjwa wa ini kwa watoto wengi nchini Marekani, ingawa hawatumii kilevi chochote (alcohol). Inaelezwa kuwa ‘fructose’ huleta madhara kwenye ini kama inavyofanya pombe.
 
Soda! Mimi nilishapiga marufuku nyumbani kwangu,
familia yangu wanalijua hili labda tu wafanye kusudi...
 
Mi nakula kama kawa: Hao watu wakija na mambo yao na ukifuatilia saana hutakula kitu. Mbona chumvi inaozesha (rust) chuma na wakati huohuo ni muhimu sana mwilini. Ukianza kusema eti coke inaweza safishia masinki ya choo/bafu hivyo ni hatari mimi nakuwa sina uhakika sana kama ukinywa na ikiwa mwilini itakuwa kwenye form ileile, reaction yake! Sawa na maji ya baridi ukinywa lakini ili mwili uyafyonze (absorption) ni lazima yawe kwenye joto linalohitajika la mwili vinginevyo wewe ni maiti. ….. hata baadhi ya watu wenye miaka iliyozidi 90 wengi wao pombe n.k. wachache nilishapata waliokuwa hata wanavuta fegi pia. Ni vema kuwa makini na kupunguza vitu fulanifulani, lakini pia hawa majamaa wa tiba mbadala wanachanganya sana, eti sijui rejea edeni nk usile nini…, kweli mengine ni ya msingi lakini biasha imekuwa mbele sana na karibu wote ni warohotu wa fedha. Hayo matunda , mbogha za majani na vyakula karibu vyote sio mbegu za asili ni genetically modified, sasa unaruka nini unakanyaga nini. Cha msingi ni kuwa na kiasi kwa vitu fulanifulani lakini ufuatiliaji wa kama vile hutakufa
 
Mh.. Mie niliacha kunywa soda kitambo bt nimeanza tena kuzinywa..
Bia nazo wanasemea vpi..? Huyo Dr alieongoza utafiti sio mlevi kweli..? Anapiga debe watu waingie kwenye ulevi..?
Just kiddin bt serious.. Kuna kinywaji chochote ambacho ni salama..? (Ukitoa maji of course)..
 
Hili la madhara ya soda linafahamika tangu siku nyingi,waulize hata wasabato watakwambia.Ila kama fructose ndiyo sukari inayotumika mle,sina hakika labda nipitie tena ingrediends zake.Na vipi kuhusu asali na miwa ambayo ina kiwango kikubwa zaidi cha fructoste huyo Mercola anasemaje?
 
Back
Top Bottom