Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

IMG_20200224_140236_611.jpg


Hey guys try this 👆 registration is total free. You earn everytime you invite someone who joins for free too. Someone from Nigeria invited me, apparently its only 9 days old in Nigeria, and making waves. I said why not since I'm only putting my email address up there, no money required.

Let's give it a try
 
haiingii akilini kuwa umefanya kazi kwa miaka mine na miezi miwili halafu ukimbie uache stahiki zako zote ukiwa umebakiza miezi isiyozidi sita kuzipokea!!!
Huu upuzi hata mjinga haamini!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani hawapotezi stahiki zozote baada ya kuhama.
Kimsingi stahiki kubwa ni kiinua mgongo
Kiinua mgongo kitapigiwa hesabu kulingana na muda uliofanya kazi. Badala ya kulipwa kiinua mgongo kwa miaka 5 au miezi 60 waliyofanya kazi, wao watalipwa miezi 56 walioishia
 
1. Upande mmoja ni faida kwa chama walichohamia kujipatia wanachama (mbinu nzuri na inakubalka kisiasa)

2. Upande wa mwingine, ni ngumu sana kuamini kuwa diwani kwa cheo chake na aliyebakisha miezi mitatu muhula wake uishe apate mafao yake eti kirahisi tu ahame chama dakika hizi za mwisho!!

3. Ni wazi kuwa biashara imefanyika hapo. Walioshikilia mfuko wa mafao yao ya fedha wameamua kuwalipa kabla ya wakati...
 
Chadema yote imehamia CCM. Then?

Watanzania ndio mjue kuwa hawa wanasiasa sio ndugu zenu!

CCM na CHADEMA wote ni matapeli wenye sare tofauti tu!
Wanasiasa ni ndugu zetu. Wanatoka kwenye jamii yetu ile ile. leo wewe unawatazama hivyo wanasiasa, hebu tutazame kwenye sekta yako kukoje? Tuna janga la kitaifa hatutaki tu kukiri. hebu jiulize kama ni kweli hao madiwani 11 wameamua kuhamia CCM nini kilitokea kabla ya kufikia uamuzi huo maana hatujasikia kama kulikuwa na tatizo Chadema Mbeya la kiwango hicho, maana yake ni kwamba kulikuwepo na kipindi ambapo watu walikuwa wakikutana kupatana, maana haiwezekani kama wote walikuwa wakifikiria kitu kimoja. na hapo maana yake yalikuwa yakijadiliwa maslahi binafsi kabla ya kufikia decision. na kama ni hivyo, hawa watu wanafuata nini CCM?

Muda wa kumaliza udiwani wao umebaki kidogo sana, kwanini wasikae wakamalizia kipindi chao kwa maslahi ya wananchi kama kweli wapo kwa ajili ya wananchi? Na kwanini CCM nao kama wanajali maslahi ya wananchi na sio maslahi ya matumbo yao, wasisubiri wamalizie kuwatumikia wananchi?
 
Kamati ya manunuzi Lumumba muda wa mavuno huo...kuleni michela ya bure bure.... peleka 60% baki na 40%.
 
hao wamefuta fursa! wanataka kuendelea na nyadifa zao na hawaoni haki kutendeka so wamekuja huko na kwa vile wao ni bora kuliko wafia chama chenu waliopo lazima watasimamishwa kama wagombea na kupita bila kupingwa kama ilivyokuwa kwa waitara na mollel!!hahahahahahah
 
NAFIKIRI TATIZO SIO CHADEMA, TATIZO LITAKUA KWA HAO WANAOHAMA NI WA BINAFSI WANAANGALIA MASLAHI YAO ZAIDI.
NAFIKIRI KUNA MKAKATI WA KUUA NGUVU YALE MAENEO YALIYOKUA NA UPINZANI MKALI NA NDIO MAANA HATA KIGOMA MJINI KWA ZITO KABWE PIA MADIWANI WALIHAMA JE ACT NAKO TUTASEMA KUNA TATIZO?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema yote imehamia CCM. Then?

Watanzania ndio mjue kuwa hawa wanasiasa sio ndugu zenu!

CCM na CHADEMA wote ni matapeli wenye sare tofauti tu!
CCM ndiyo matapeli wakuu, hata ningekuwa mimi Diwani wa CDM wakinipa 50m siwezi ziacha...navaa miguo yao rangi ya nzi wa toilet ki geresha toto huku mpunga wa walipa kodi aka wa bure huo kwapani...
Jioni nashinda CDM napanga mikakati ya ushindi ki siri siri.
 
Usiihusishe wanaohama na Uongozi wa Juu wa Chadema , hauhusiki usije kubeba dhambi bure , kama hujui endelea kutokujua lakini usitunge uongo
Mkuu uongozi wa juu wa CDM unahusika sehemu moja tu, kushindwa kuzuia hii hali isiendelee.
Wawe wabunifu kutafuta suluhisho la tatizo lililopo mbele yao ndio maana ya uongozi.

Matumaini ya wanachama wao wa kawaida yapo kwao, haitoshi kulalamika wananunuliwa huku haufanyi kitu kukabiliana nao zaidi ya kulalamika kama wanasubiri hisani ya viongozi wa chama shindani kukomesha hili tatizo.

Kazi ya uongozi ni kutafuta majibu, ni kama wnavyotaka Raisi awajibike kwa makosa ya watendaji wake ngazi ya wilaya au kata.
 
Tulia alivyosema Jimbo lazima alibebe sasa nimekuelewa..

Pesa imeshindwa kumpa uhai maiti tu ila mengine aisee inaweza

Manunuzi ya wazi wazi...kweli Taifa la viwanda hili...
 
Kwanini chama kinapitisha wagombea ambao wananunulika au waoga kupambana?
Kwanini chama kinapitisha watu ambao hawavumilii njaa?
Fungua akili, macho na masikio. Usilishwe maneno
Suala la wanasiasa kuhama ni pana lakini linaelezeka.
Utapata jibu sahihi kama utajua;
Kwa nini Godbless Lena alihama TLP akaenda CDM
Kwa nini Msigwa alihamia CDM kutoka TLP
Kwa nini LISSU alitoka NCCR kwenda CDM
Kwa nini Hamad Rashid alitoka Cuf akaunda ADC
Kwa nini Zito, Kitila, Migamba, Mwampamba na wenzao walitoka CDM wakaunda ACT
Kwa nini Maalim Seif alikimbia CUF akajisajili ACT
Kwa nini Lowasa alitoka CCM akaenda kuinunua CDM, achilia mbali wale walihamia C M kama Kutoka upinzani kama Mwampamba, Mwigamba, Mashinji, Aman Kabourou, Dr. Slaa, Said Arfi
Kwanini kuna wanasiasa waliokata tamaa na wakaamua kustaafu kama kina PROF. SAFARI!?



Anyway, mifano ni mingi inayoonyesha sababu na mazingira tofauti yanayopelekea wanasiasa kuhama.
Ya mwisho kabisa ni kununua.
 
Acheni kutu pumbaza Tunataka kujua issiue ya Lugola. Ni lini mnamfikisha mahakamani? Maana hizi zuga ni za kuwafanya Watanzania wasahau ya Lugola and company.

Hivi CCM chama chenye miaka mingi kwenye siasa kuliko vyama vyote Africa mmefikia mahali pa kusherehekea kupokea wapinzani?

Mna tia aibu. Ni kwamba mmekosa kabsa mbinu mbadala wa kufanya siasa? Nawainea huruma. Maana sasa huku mna bebwa na dola, huku tume ya uchaguzi, kule kununua wapinzani hadi raha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata hiki kinachofanyika ni SIASA pia.

Senti bai yuzingi tecno T301
 
Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally amesema kati ya Madiwani hao, 10 ni Madiwani wa Kuchaguliwa na Mmoja ni wa Viti Maalumu huku timu hiyo inayoongozwa na Meya ikiwa na Viongozi Watatu wa Juu wa CHADEMA.

Amesema kuwa Madiwani hao wanatoka katika Jiji la Mbeya kwenye Halmashauri inayoongozwa na CHADEMA na Mbunge wa Jimbo hilo ni Joseph Mbilinyi (Sugu) na kuwa huo ni ugeni mkubwa tangu aanze kupokea Wageni.

Aidha, amesema ameongea na Madiwani hao na kumueleza kwanini wanafanya uamuzi huo wakati huo na amefurahi sana maana kazi yake ni kuifanya CCM kutoa ushawishi na kupata wafuasi kila kona ya Nchi.
Watu wanaondoka kwenye chama chenye DEMOCRASIA, kwanini?? Lakini pia kina mlengo Wa MAENDELEO, why???? Something wrong is there in
 
Fungua akili, macho na masikio. Usilishwe maneno
Suala la wanasiasa kuhama ni pana lakini linaelezeka.
Utapata jibu sahihi kama utajua;
Kwa nini Godbless Lena alihama TLP akaenda CDM
Kwa nini Msigwa alihamia CDM kutoka TLP
Kwa nini LISSU alitoka NCCR kwenda CDM
Kwa nini Hamad Rashid alitoka Cuf akaunda ADC
Kwa nini Zito alitoka CDM akaunda ACT
Kwa nini Maalim Seif alikimbia CUF akajisajili ACT
Kwa nini Lowasa alitoka CCM akaenda kuinunua CDM


Anyway, mifano ni mingi inayoonyesha sababu na mazingira tofauti yanayopelekea wanasiasa kuhama.
Ya mwisho kabisa ni kununua.
Suala la kuhama vyama wanachama wa kawaida au viongozi wachache au wastaafu ni kawaida sana sikatai.
Kuhama wanachama wengi ndani ya muda mfupi sio kawaida ni tatizo.
Kuhama viongozi wahandamizi wengi ndani ya uda mfupi ni tatizo zaidi.
Kuhama viongozi wa ngazi za juu kabisa wawe wastaafu au waliopo madarakani ni tatizo kubwa sana sana.
Kuhama viongozi wawakilishi wa wananchi kwenye majimbo au kata ni tatizo kubwa mbele ya walio wapa nafasi ya kuwawakilisha na kuwasemea kupitia chama walichokiamini ajenda au itikadi zake.
 
Back
Top Bottom