Maelezo ya Wenje yamenyooka zaidi kuliko tuhuma za Lissu! Huenda Mbowe bado ni mtu sahihi zaidi kuongoza CHADEMA

Huu ni uthibitisho kuwa CHADEMA bado chama kichanga sana, kina safari ndefu kama ya miaka 25 kushika nchi.
Tuliyoyaona huko nyuma, sasa ni hali halisi kwa wanachama wote. Ni wakati wa kuisaidia CDM, kuonyeshwa njia.
 
Kwanini alimpeleka Abdul kwa Lissu?. Kwahio alimsaidia Ili yeye Abdul baada yakumsaidia wenje yeye ananufaika vipi?.

Wajinga ni wengi na mapenzi kwa Mbowe yanawapumbaza
 
Wenje knew exactly what he was doing....

Kama ulivyosema kuwa, Wenje amekuwa na poor judgement ktk maamuzi yake....

Walifikiri Tundu Lissu kwa kuwa anahitaji fedha sana wakati ule (may be), he couldn't have a choice zaidi ya kuzipokea tu pesa hizo, kwa kusema zileteni....

Na bila shaka inawezekana walimwambia, chukua tu na itasemwa umelipwa za matibabu yako...!

On the other hand...

Shida ya Freeman Mbowe na wapambe wake, ni kuwa, pamoja na uzoefu wake mkubwa ktk siasa za mageuzi alikuwa hajawaelewa CCM vyema kuwa ni watu wadanganyifu na wenye hadaa ya kufa mtu...

Na ona sasa, wanamwingiza katika fedheha kubwa na mbaya sana, sababu ikiwa ni pesa zilizomuuza Yesu Kristo kwa majambazi...

These people are great manipulstors...

Wameingizwa mkenge kwenye maridhiano lakini bado hawajifunzi tu....

Kama ana hekima na busara, ingekuwa bora sana akatambua makosa na udhaifu wake na kisha achukue maamuzi magumu ya kupumzika kuliko kuendelea kujifedhehesha. Na huko tuendako inawezekana akadhalilishwa zaidi..?

Kwenye hili, eleweni kuwa Wenje ni mjumbe tu. Lakini nyuma yake yuko Freeman Mbowe mwenyewe...!!
 
Chawa pro max
 
Kwa mawazo yako unafikiri kweli Abdul alikwenda nyumbani kwa lissu kumsaidia? Yaani mtoa msaada anamfata mtu anaetaka kumsaidia nyumbani kwake hivi hivi. Kwanza Wenje muongo ni hivi lissu aliogopa kwenda kule hotelini ndo maana akawambia waje nyumbani wala sio kwamba alikuwa anaumwa.
 
Umesahau Wenje walikutana na Abdul katika shughuli/sherehe fulani, wakawa wamekaa meza moja lakini Wenje akiwa hamjui ni nani, ndipo akatambulishwa huyu ni mtoto wa Rais katika kupiga story ndipo akamuuliza kwa nini lakini Serikali ya mama yake haitaki kumlipa Lissu madai yake, Abdul akasema mbona anafahamu ameshalipwa ndipo Wenje akampigia Lissu simu baada ya sherehe amthibitishie Abdul kwamba bado hajalipwa pesa zake anazoidai Serikali ndipo wakapanga hadi huko kukutana Lissu akiwa na nyaraka za matibabu ili Abdul asaidie kufanikisha hilo jambo.
 
Halafu anagombea Makamu mwenyekiti endapo atashinda na Lisu akashinda hawa watafanya kazi kama mtu na msaidizi wake?
Hapo ndipo chama kitakaposambaratika. Kwa akili ya kawaida lazima viongozi wenye hekima na busara wamshauri mmoja ajitoe au apingwe ili asishinde kwa manufaa ya chama (Uma).
 
shenzi hayo maelezo yakowapi?
 
Njia aliyotumia Wenje inaweza kuwa ina shida lakini ameelezea sababu ni zipi ilikuwa hivyo na akatolea mfano jinsi nchi hii contractor anaweza akajenga na kukamilisha mradi vizuri kabisa akiwa na certificates zote lakini akawa anazungushwa katika malipo yake ndipo ambapo watu wanatumia watu wanaowajua watu wenye mamlaka ili tu kukwamua haki zao. Kumtumia Abdul ili kushawishi malipo halali ya Lissu yalipwe na serikali japo ni jambo la hovyo lakini sio rushwa kama anavyoelezea Lissu kuhongwa "pesa za Abdul".
 
Inawezekana Abdul alikuwa akitaka kumsaidia Lissu lakini akiwa na ajenda zake nyingine za ziada za kisiasa, inawezekan alikuwa anamtaka amsaidie kwa huruma tu lakini pia inawezekana alitaka kumsaidia kama mtoto wa mwenye mamlaka tu kujisikia vizuri kushawishi mamlaka, hilo ni la Abdul sasa.

Kuhusu kuumwa Wenje anasema Lissu alikuwa anaumwa tangu wanatoka Arusha kurudi Dar kuelekea siku ya kukutana na Abdul, kama Lissu alidanganya hilo ni lake Lissu pia.
 
Swali ambalo limebaki sasa ni kwamba Lissu anafanya mambo haya kwa sababu au faida zipi ukizingatia inaleta mgawanyiko sana ndani ya chama chake!
Nimeshawaambia lisu ni mtu mbinafsi sana, sijui kwa nini nyie hamuelewi tu. Anafanya hayo kwa manufaa yake binafsi ili apate sympathy toka kwa nyumbu na hatimaye apigiwe kura kuwa mwenyekiti wa chama. Hizo ni calculated moves zake ili apate kura za huruma. Yuko tayari kusema au kufanya lolote kwa manufaa yake binafsi.
 
Nimeiweka ili kuonyesha how ridiculous the whole thing is. Wenje, seriously, aende kumhonga Lissu nyumbani kwake? Atakuwa mjinga namba moja.

Amandla...
 
It still does not make any sense. Hasa ukimuingiza Mbowe ambae bila shaka alikuwa anajua kuwa Lissu ameanza kupoteza imani nae. Na kwa nini leo? Na kwa nini amhonge Lissu? Ili anyamaze? Hamjui Lissu? Hapa Lissu ameingia choo cha kike. Nia yake ni kummaliza mtu ambae alidiriki kusema wazi kuwa atashindana nae. Ego yake imempeleka pabaya.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…