Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,175
- 2,294
Huu ni uthibitisho kuwa CHADEMA bado chama kichanga sana, kina safari ndefu kama ya miaka 25 kushika nchi.Nimesikiliza maelezo ya Ezekiel Wenje aliyetuhumiwa na Lissu kumpeleka Abdul kumuhonga pesa, ukiniuliza mimi naona maelezo ya Wenje yamenyooka sana kuliko tuhuma alizokuwa anarusha Lissu dhidi ya watu anaodai wamehongwa.
Swali ambalo limebaki sasa ni kwamba Lissu anafanya mambo haya kwa sababu au faida zipi ukizingatia inaleta mgawanyiko sana ndani ya chama chake!
Nilikuwa nasubiria kwa shauku kumsikia Mbowe atajibu vipi tuhuma za watu wake kuhongwa pesa za Abdul lakini maelezo ya Wenje yamenyooka sana, yanatosha na naona yana ukweli mkubwa kuliko tuhuma za Lissu.
Tuliyoyaona huko nyuma, sasa ni hali halisi kwa wanachama wote. Ni wakati wa kuisaidia CDM, kuonyeshwa njia.