Maelezo ya Wenje yamenyooka zaidi kuliko tuhuma za Lissu! Huenda Mbowe bado ni mtu sahihi zaidi kuongoza CHADEMA

Na wewe umeamini kabisa hii porojo? kwamba Abdul anajua Lissu ameshalipwa pesa zake wakati hajalipwa ukizingatia Lissu amekuwa akipiga kelele juu ya pesa zake kwa muda mrefu tu?
 
Na wewe umeamini kabisa hii porojo? kwamba Abdul anajua Lissu ameshalipwa pesa zake wakati hajalipwa ukizingatia Lissu amekuwa akipiga kelele juu ya pesa zake kwa muda mrefu tu?
Abdul hawezi kuwa anafuatilia kila siku kujua kama Lissu ameshalipwa pesa zake, Abdul ana maisha yake na ishu zake nyingine.
 
Ni kawaida sana kwenye siasa dola kuinfiltrate moles wa vyombo vya usalama na hii sio dhambi ni jukukumu la msingi la vyombo.
 
Nadhani hukumsikiliza vizuri!!

Wenje ni dalali kweli!! Why aambatane na Abdul kwenye madai halali ya Lissu?

Rais alishakubali kumshughulikia madai ya Lissu, ni vipi Wenje kujitwika jukumu la kumtafuta Abdul? Kwanini hakufuata taratibu za kiserikali? Wenje ajitoe kugombea umakamu wa Mwenyekiti haraka sana
 
Wenje kajikanyaga kanyaga ovyo ovyo tu hajaeleza kile kinachodaiwa

Mara Abdul alisema Lissu tayari kashalipwa mara wakaenda kwa Lissu wakachukua nyaraka

Hapo kuna kitu behind the scenes tumefichwa.
Hivi ndivyo wafanya biashara walivyo. Wao ni pesa tu, wala hakuna cha kutetea wanyonge.
Watanzania wana akili san, ndio maana kila uchaguzi wanawapotezea mbali.
 
Abdul hawezi kuwa anafuatilia kila siku kujua kama Lissu ameshalipwa pesa zake, Abdul ana maisha yake na ishu zake nyingine.
Kwamba Wenje,mwanasiasa mashuhuri kabla ya mwezi wa 10 mwaka jana alikuwa hamjui kabisa Abdul ndio akatambukishwa ukumbini wakati watu wengi tu huku mtaani wanamfahamu Abdul hasa ukizingatia miezi miwili kabla (August) mwaka jana zilisambaa habari kwenye media nyingi nchini juu ya Abdul kuiwakilisha serikali ya Tanzania nchini Uganda na picha zake kusambaa kwa wingi kwenye mitandao
 
kwahiyo kwa akili zako ulitaka wenje ajisemeeje??
 
Lissu alisema Abduli alikuwa anataka kumpa RUSHWA ili aache kumkomalia Mama yake.

Wenje anasema alimpeleka Abduli ili Tundu Lissu alipwe madai yake sasa nadhani Lissu anatakiwa anyooshe zaidi maneno yake ili tujue nini ni nini na lipi ni lipi.
 
Hata wewe kuna mazingira ukikutana na Abdul unaweza usimjue kama ni yeye .
 
Hiyo shughuli iliyowakutanisha ilikuwa haramu? Kama haikuwa haramu aitaje! Vinginevyo unatusikitisha sana wewe mtu mzima kuuamini uongo wa mchana kweupe.

Hivi Kwa mfano wasingekutana kwenye hiyo shughuli Wenje angeweza kunisaidia vipi Lissu kuhusu madai yake halali?

Pengine wewe mwandishi wa mada hii ni Wenje
 
Kwa ambao hawana akili kama wewe ni sawa
 
Hivi vichekesho huwa mnavipataje?
 
Lissu hakumtaja kwa jina.
 

Lazima tujiulize maswali haya ,Wenje kwa muda mrefu alikua hana jina kubwa hasa kipindi hiki cha Awamu ya Tano inayojiita ya sita ,imekuwaje mtoto mdogo kama Abdul amtafute Wenje ili amfukie Lisu?
Je, Abdul ni nani kwenye CCM na kwa nini aanze kuwatafuta watu Baada ya Kashfa ya DP World?
Je, hii haionyeshi wazi kuwa ni watu wengi hasa viongozi wa CHADEMA wa kanda walipewa fedha za DP World kuzima maandamano yaliyokuwa yameitishwa na Mwabukusi na wanaharakati wengine?

Ikumbukwe kuwa Wanaharakati waliitisha maandamano kupinga kuuzwa kwa bandari ya DSM .

Wanaharakati akiwemo Dr.Slaa wakaanza kutumia jukwaa la Chadema kuratibu maandamano , Wanaharakati wakaviomba vyama vya siasa viungane nao kuhamasisha na kupanga maandamano nchi nzima . CHADEMA wakajitokeza kukanusha kuwa wao hawa mpango wa kushiriki kwenye maandalizi wala kuhamasisha wanachama wao kuandamana nchi nzima kupinga uuzwaji wa Bandari . Maandamano ya Mwabukusi yakakosa nguvu kubwa . Bandari inauzwa kizembe kabisa nchi ikiwa na chama kikubwa kabisa kinachosema kina kubalika nchi nzima bila kuandamana wala kushiriki kwenye maandamano yaliyoandaliwa na wanaharakati ,wasiokuwa na vyama .

Hapa ndipo wanapitia mashaka ya Mapeswa ya Rushwa yaliyotolewa na viongozi wa vyama vyote na wakalamba asali kimya kimya . Lisu Pekee alijitokeza hadharani kupinga rushwa ya kuuza nchi na Bandari zetu .
Lisu Pekee anaonekana wazi kuwa suala la bandari zetu kuuzwa linaloleta kuliko kuliko viongozi wote wa vyama vyote vya siasa Tanzania. Akifuatiwa na wanaharakati wazalendo pamoja na Kanisa Katoliki linalosimamia misingi ya haki kwa watu wote duniani tofauti na mengine yanayojali zaidi vipato vyao na kuziba midomo.


Lisu ni Mwanasiasa wa karne na muujiza unaotembea .
 
Hizo taratibu za kiserikali si ndio zimeshindwa? Hivi wale ambao kila siku wanamlilia hali Rais au Makonda hawajui kuwa kuna taratibu za serikali? Hivi wewe ukiona unapigwa dana dana malipo yako haumtafuti mtu ambae ana access na anayeweza kukusaidia? Kuna kitu gani cha ajabu kwa Wenje kusema " ngoja niongee na Abdul labda anaweza kutusaidia kwa kumkubusha mama yake kuhusu ahadi yake?" Tatizo liko wapi?

Amandla...
 
Unahitaji uwe kichaa ili utetee huu uchafu yaani malipo ya Lisu ayaulizie Kwa Abdul ambaye sio mfanyakazi wa serikali
 
Sio kweli tutajie ushawahi sikia wapi pengine?
 
Hata wewe kuna mazingira ukikutana na Abdul unaweza usimjue kama ni yeye .
Kwamba Wenje amemwona kwa mara ya kwanza shereheni, hapo hapo akaanzisha suala la madai ya Lisu na kufikia hatua ya kumpigia Lisu simu. Mtu ambaye ulikuwa humjui unakutana naye mara hiyo na kumuekeza matatizo yako. Kisha yeye anajotolea kumfuata nyumbani msaidiwa badala ya kumtaka mwomba msaada kumfuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…