Nimesikiliza maelezo ya Ezekiel Wenje aliyetuhumiwa na Lissu kumpeleka Abdul kumuhonga pesa, ukiniuliza mimi naona maelezo ya Wenje yamenyooka sana kuliko tuhuma alizokuwa anarusha Lissu dhidi ya watu anaodai wamehongwa.
Swali ambalo limebaki sasa ni kwamba Lissu anafanya mambo haya kwa sababu au faida zipi ukizingatia inaleta mgawanyiko sana ndani ya chama chake!
Nilikuwa nasubiria kwa shauku kumsikia Mbowe atajibu vipi tuhuma za watu wake kuhongwa pesa za Abdul lakini maelezo ya Wenje yamenyooka sana, yanatosha na naona yana ukweli mkubwa kuliko tuhuma za Lissu.
Lazima tujiulize maswali haya ,Wenje kwa muda mrefu alikua hana jina kubwa hasa kipindi hiki cha Awamu ya Tano inayojiita ya sita ,imekuwaje mtoto mdogo kama Abdul amtafute Wenje ili amfukie Lisu?
Je, Abdul ni nani kwenye CCM na kwa nini aanze kuwatafuta watu Baada ya Kashfa ya DP World?
Je, hii haionyeshi wazi kuwa ni watu wengi hasa viongozi wa CHADEMA wa kanda walipewa fedha za DP World kuzima maandamano yaliyokuwa yameitishwa na Mwabukusi na wanaharakati wengine?
Ikumbukwe kuwa Wanaharakati waliitisha maandamano kupinga kuuzwa kwa bandari ya DSM .
Wanaharakati akiwemo Dr.Slaa wakaanza kutumia jukwaa la Chadema kuratibu maandamano , Wanaharakati wakaviomba vyama vya siasa viungane nao kuhamasisha na kupanga maandamano nchi nzima . CHADEMA wakajitokeza kukanusha kuwa wao hawa mpango wa kushiriki kwenye maandalizi wala kuhamasisha wanachama wao kuandamana nchi nzima kupinga uuzwaji wa Bandari . Maandamano ya Mwabukusi yakakosa nguvu kubwa . Bandari inauzwa kizembe kabisa nchi ikiwa na chama kikubwa kabisa kinachosema kina kubalika nchi nzima bila kuandamana wala kushiriki kwenye maandamano yaliyoandaliwa na wanaharakati ,wasiokuwa na vyama .
Hapa ndipo wanapitia mashaka ya Mapeswa ya Rushwa yaliyotolewa na viongozi wa vyama vyote na wakalamba asali kimya kimya . Lisu Pekee alijitokeza hadharani kupinga rushwa ya kuuza nchi na Bandari zetu .
Lisu Pekee anaonekana wazi kuwa suala la bandari zetu kuuzwa linaloleta kuliko kuliko viongozi wote wa vyama vyote vya siasa Tanzania. Akifuatiwa na wanaharakati wazalendo pamoja na Kanisa Katoliki linalosimamia misingi ya haki kwa watu wote duniani tofauti na mengine yanayojali zaidi vipato vyao na kuziba midomo.
Lisu ni Mwanasiasa wa karne na muujiza unaotembea .