Maelezo ya Wenje yamenyooka zaidi kuliko tuhuma za Lissu! Huenda Mbowe bado ni mtu sahihi zaidi kuongoza CHADEMA

Hahaha wewe umependa sauti tu, lakini huwezi kusema maelezo ni manyoofu bila ushahidi.

Katika tuhuma yoyote, kinacho mtakatisha mtuhumiwa ni ushahidi usioacha shaka, wewe umesikia tu maelezo ukanogewa na sauti usha fikia conclusion.

Hatuendi hivyo, tunataka ushahidi tujiridhishe na siyo maelezo mazuri.
 
Mfumo...
 

..Wenje ameshindwa kueleza alikutana na Abduli katika shughuli gani, na nani aliwatambulisha. Mpaka hapo utaona kwamba ni mjanja mjanja.

..pia kitendo cha kukaa kimya kwa muda mrefu asijitokeze tangu awali kueleza kilichojiri kinaleta ugumu kumuamini.

..Wenje anakutana na Abduli badala ya kumtaka atetee mambo ya msingi, anaanza kumdai mafao ya Lissu?
 
Si kasema Lissu alikuwa anaharisha tokea Arusha Au hukusikia?

Sasa hiyo ni tafsir yako ya Rushwa ..

Nchi hii haya mambo yanayokea mara nyingi na ni ya kawaida sana...

Suala la gaps za miez sita ndio Lissu anakuja kusema hilo unalionaje

..miezi 6 haikutosha Abduli kumpatia Lissu mafao yake, ili waweze kumblackmail?
 
Watz sio wajinga
 


Ni kweli lakini bado Lissu atasaidia ingawa inabidi awe na watu wengi wa kumsaidia
 
Lissu angefariki ingekuwaje? Wenje angeidai familia ya Lissu hizo pesa.

Wakati Lissu yuko mahututi alijua kuwa anapewa mkopo?

Ulikuwa msaada au mkopo?
 
Lissu asubirie labda 2029. Pia dhamira yake huenda sio nzuri sana. Atoa tuhuma za jumla jumla
 
Lissu ameni disappoint sana. Sijui kwa nini nimepoteza muda wangu kumwamini.
 
Lissu angefariki ingekuwaje? Wenje angeidai familia ya Lissu hizo pesa.

Wakati Lissu yuko mahututi alijua kuwa anapewa mkopo?

Ulikuwa msaada au mkopo?
Lissu amekaa kitandani muda gani? Au unadhani Wenje alimkopesha Lissu from day one? Wenje anasema ile siku Lissu amepigwa risasi Wenje alipigiwa simu na Mbowe kuhakikisha Lissu anapelekwa Agakhan hospital lakini Wenje kwa uzoefu wake na kujuana kwake na watu wakahakikisha anapelekwa Nairobi hospital na guarantee ya kulipa aliitoa yeye Wenje
 
Mbowe is the right person in the wrong time .


Mbowe ni amefika kiwango chake cha mwisho he has nothing to offer

Akiendelea ataharibu .
Mkuu kwa wanaona mbali watakusoma. πŸ™‹β€β™‚οΈβœοΈπŸŽ―πŸ’πŸŽπŸ‘πŸ‘ŒπŸ‘ŠπŸ‘πŸ€πŸ™
 
Mbona hutumii hata akili ndogo tu ktk hili mkuu, kama lissu angekua muongo ktk hizi shutuma nzito zinazokichafua chama direct, unadhani muda wote huo angekua hajachukuliwa hatua?

Mapenzi yako kwa mbowe yasikupofushe mkuu, hapo wenje anajitetea tu hakuna la ziada.
 
Mkuu uchambuzi wako umeegemea upande. Unamhukumuje Tundu Lissu kuwa hana sifa za uongozi wakati hajawahi kuwa mwenyekiti wa Chadema.

Unatumia kipimo gani cha kusema Mbowe ana sifa za uongozi ilhali Tundu Lissu hana wakati miaka yote ishirini ya maraisi watatu wa CCM, Mbowe hajaleta tangible impact kwenye chama chake.

Kama ndivyo, ilikuwaje Chadema chini ya Mbowe ikaona kuwa Tundu Lissu ana sifa za uongozi kiasi cha kumchagua miongoni mwa wagombea wengi ndani ya chama chake, kugombea urais kipindi ambacho Tundu Lissu alikuwa bado anaumwa na nyakati ngumu za Magufuli, ila kwenye kogombea uenyekiti sasa hivi ndio akose sifa za uongozi???

Mkuu Inakuingia akilini kweli???

Kuna mengi ya kumdisqualify Mbowe kustahili sifa ya kuwa au kuendelea kuwa mwenyekiti Chadema as compared to Tundu Lissu or any other.

Kwa kifupi tu, Miaka 11 ya uenyekiti wa Mbowe Chadema ilipiga hatua 3 mbele na miaka 9 iliyofuata Chadema imerudi nyuma hatua 7 and it is obvious.

Kwa msingi huu akiendelea itakuwaje???

Mkuu hata kama unamchukia au humtaki Tundu Lissu, at least kuwa fair kwa wote kwenye uchambuzi wako.
 
πŸ™‹β€β™‚οΈβœοΈπŸŽ―πŸ‘πŸ‘ŒπŸ‘πŸ‘ŠπŸ€πŸ™
 
Hayo maneno Yana element za wapenda rushwa na kujipendekeza, wenje anamsemea mpaka Abdul, anaujua moyo wa Abdul? Wenje alichemka, aache kujipendekeza
 
Dogo usiwe kipofu, Abdul ana nafasi Gani katika serekali ya mama yake

Unadhani huu utetezi wenu mwepesi utafuta tuhuma za rushwa kweli?
 
Haahaa wenje tamaa imemponza, pesa za lissu Abdul anahusika vipi? Lazima kulianza na kitu kimerukwa? Wenje aache tamaa eti mtoto wa rais, then so what?
 
Acha kujifanya mjuaji, hamna kitu pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…