Maelezo ya Wenje yamenyooka zaidi kuliko tuhuma za Lissu! Huenda Mbowe bado ni mtu sahihi zaidi kuongoza CHADEMA

Yoda njoo unyooshe maelezo hapa
 
Kwamba alionana na Abdul kwenye event,siku hiyo hiyo wakafahaniana na akaanza kumuelezea suala la Lissu,inaingia akilini kweli? Yaani uonane na mtu siku hiyo hiyo uzoeane naye kwa haraka tena kwenye sherehe? Anyway tutajua mengi
Inategemea na wepesi wa kichwa chako kilivyo, sioni ugumu wa haya unayouliza ukizingatia suala la Lissu limekuwa mjadala muda mrefu katika nchi, ni kitu rahisi tu kuanzisha small talk inayohusiana na nchi inavyokwenda na kisha kuchomekea hilo.
 
Maelezo mazuri sana..nilikuwa najiuliza kwanini CDM inadidimia..kumbe akina wenje wamepewa pesa ndio maana wanakaa kimya watu wakitekwa..
 
Na hawa chawa wake ndiyo wanazidi kumpaka kinyesi kwani kadiri wanavyozidi kumtetea na kutoa maelezo ya janja janja ndiyo wanafungua milango ya watu wenye akili kuzidi kuchimba ili kuufikia ukweli halisi. Mbowe kwa uzoefu wake nilidhani angeliona hili mapema na kutangaza mapema kuwa yeye anaheshimu kauli yake aliyotoa 2019 kuwa hatagombea tena hivyo hawa wapambe nuxi wasingekuwa na kiherehere. Naona mbele ya safari Mbowe akienda kudhalilika sana. Hawa wapambe hawana cha kupoteza sana zaidi ya manufaa binafsi waliyokuwa wanapata kwa Mbowe kuwa mwenyekiti, lakini Mbowe ataathirika zaidi kwani heshima aliyojingea kwa miaka 30 inaenda kuyeyuka kama tofali la barafu kwenye jua kali.
 
Mkuu, hii ya 'Asibishane na wakati' ndilo jibu lenyewe, maana " WAKATI ni UKUTA"
 
Na wewe ukaamini huu uzushi,Lissu ndiye mwenye shida kwani Abdul ndiye afunge safari kumfuata mtu anyehitaji msaada na isiwe vice versa?
 
Mbona maelezo ya wenje yanadai Abdul alisema alishalipwa? Alijuaje?
Alisema yeye alikuwa akifahamu Lissu ameshalipwa, labda ilikuwa ni kudhani tu kwa sababu aliona Lissu hapigi tena kelele n.k
 
Wewe ni Wenje. Na uongo uliotunga unaonyesha ulivyo na akili ndogo.
 
Na wewe ukaamini huu uzushi,Lissu ndiye mwenye shida kwani Abdul ndiye afunge safari kumfuata mtu anyehitaji msaada na isiwe vice versa?
Ilikuwa wakutane hotelini, Lissu akaumwa ndio wakaamua waende nyumbani kwake.
 
Ilikuwa wakutane hotelini, Lissu akaumwa ndio wakaamua waende nyumbani kwake.
Lissu alikuzidini akili wewe na Abdul. Alijua akienda hotelini hatakuwa na ushahidi ndiyo maana akawaambia mwenda nyumbani kwake. Hili jambo siyo rahisi kukana kama unavyofikiria. Samia angetaka kumlipa Lissu wala kusingekuwepo na ulazima wa wewe na Abdul kwenda nyumbani kwake.
 
Wenje, Lissu na wengine ndani ya CHADEMA walikuwa wanahongwa pesa na Abdul ili iwaje??
 
Mkuu umemskiliza Wenje lakini ? Kuna sehemu yoyote umeona amejichanganya kwenye maelezo yake?
Siyo kujichanganya tu bali umeonyesha ulivyo mpumbavu kama huyu Abdul na mama yake. Hata kama ni rushwa kuna namna ya kutoa na siyo ujinga mliofanya. Nyie mlidhani Lissu ana uchu wa fedha kama wewe na Mbowe na hatakuwa na namna ya kuzikataa.
 
Kukubaliwa kulipwa haki yako Kwa masharti nayo ni hongo.Huwenda alipewa masharti. Hilo nalo linahitaji D MBILI Kulielewa?
Ni masharti gani ambayo yalitolewa?
 
Wenje, Lissu na wengine ndani ya CHADEMA walikuwa wanahongwa pesa na Abdul ili iwaje??
Mbowe na wewe mmeshachukuwa chenu. Lissu amekataa kwa sababu hataki rushwa. Samia anajua hakubaliki ndiyo maana amemhonga Mbowe akitaka asipate ushindani uchaguzi ujao. Mbowe ni dalali. Katudanganya siku nyingi lakini sasa hivi amefika mwisho wa utapeli wake.
 
Mkuu, heshima kwako! Je, mwaka 1985 tunge kuomba utuwekee watu 10 ambao wewe una uhakiki watakuwa Maraisi wetu WATARAJIA kwa Mujibu Taratbu zetu za kumpata RAIS wetu hadi leo 2024 ungepatia/ungekuwa sahihi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…