Pia na sisi tumemtazama na kumsikiliza vyema....
Kama umemwelewa na kumwamini Hezekia Wenje akiwawakilisha wenzake waliokula naye mlungula, nachelea kusema kuwa udadisi na ufahamu wako una kasoro...
Kwanini kabla hujaja na conclusion ya namna hii ukajipa nafasi ndogo tu kujiuliza maswali madogo na rahisi tu haya:
1. Tundu Lissu aliumia akiwa kazini. Ni kwanini unadhani serikali haitaki kulipa madai ya fedha za Tundu Lissu alizotumia kujitibu huku akiwa mbunge (mtumishi wa umma) ambaye yuko entitled na haki hiyo ya kutibiwa kwa gharama za serikali...?
2. Kumbe Wenje alimkopesha Tundu Lissu kwenye pesa hizo za matibabu. Na kumbe struggle ya Wenje na wenzake (akiwemo Freeman Mbowe aliyemtuma Wenje) hadi kuamua kujiuza kwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kwa mwanae Abdul. Sasa kwanini naye anasema hilo leo? Je, Tundu Lissu anajua kuwa anadaiwa na Wenje? Shilingi ngapi..?
3. Hivi, malipo halali ya serikali hufanyika kwa njia wanayotumia Abdul na Wenje?
4. Na je, madai ya Tundu Lissu (fedha za kujitibu alizopaswa kulipiwa na serikali) ni halali au batili/ hayakidhi vigezo vya kulipwa na serikali...?
5. Kama madai yake ni halali kabisa, ni haki yake alipwe fedha hizo, huyu Abdul na Wenje wanaingia hapo kama kina nani? Walikwenda kufanya nini kwa Tundu Lissu? Wana influence gani serikalini?
6. Kama madai ya Tundu Lissu siyo halali, serikali imeshawahi kumjibu kwa maandishi kuwa hutalipwa fedha zako za madai ya matibabu yako kwa hayakidhi vigezo vya malipo 1, 2, 3, 4 nk...?
##Ukiweza kujibu maswali ndiyo utaelewa Hezekia Wenje na Genge lake ni wakweli kiasi gani...!