Maelezo ya Wenje yamenyooka zaidi kuliko tuhuma za Lissu! Huenda Mbowe bado ni mtu sahihi zaidi kuongoza CHADEMA

Maelezo ya Wenje yamenyooka zaidi kuliko tuhuma za Lissu! Huenda Mbowe bado ni mtu sahihi zaidi kuongoza CHADEMA

Sasa hayo maelezo yaliyonyooka yako wapi? Labda, hata wewe huyaamini hayo maelezo yake. Wenje ni ZZK tu, hawezi kuacha fursa yoyote ya hela, namjua kwa karibu sana.

Labda nikuache na wosia wangu, ni kwamba, mtu pekee wa kumwamini katika harakati, ni wewe mwenyewe.

Ova
Haahaa kweli na kakiri yeye ni mfanyabiashara
 
Lissu amekaa kitandani muda gani? Au unadhani Wenje alimkopesha Lissu from day one? Wenje anasema ile siku Lissu amepigwa risasi Wenje alipigiwa simu na Mbowe kuhakikisha Lissu anapelekwa Agakhan hospital lakini Wenje kwa uzoefu wake na kujuana kwake na watu wakahakikisha anapelekwa Nairobi hospital na guarantee ya kulipa aliitoa yeye Wenje
Mkuu haiondoi ukweli kuwa premise nzima ya sakata hili la udalali wa rushwa ya Abdul, kwa mujibu wa maneno ya Wenje ina rangi zote za rushwa.

Kumsaidia Tundu Lissu isiwe scapegoat, hata ingekuwa ni yeye Wenje aliyedhurika kuna mtu angemsaidia tu.

Ajitete kwa namna nyingine lakini sio kwa kuingiza madhila aliyopitia mwenzie.
 
Kuna Kitu Chadema huwa hamkielewi Kwa sababu wengi wenu ni watoto wa juzi tu

Hata hamjui nani waliasisi Chadema na Kwa sababu gani!!

Hamjui kwanini Mwita Waitara, Patrobas Katambi na Cecil Mwambe wakiletwa Chadema

Tena hamjui kwanini Shibuda na Marando 😄😄😄

Niishie hapo 🐼
Hiyo ni vyama vyote vya opposition, timu ya NCCR-mageuzi ilianzishwa na timu ile pendwa tupu.
Nyerere katika ubora wake.
 
K
Ingekuwa hivyo basi angekuwa ameishapata maana hajaanza jana kudai malipo yake serikalini. Hata alipoonana na Mkuu wa Nchi Ulaya alimwambia kuhusu malipo yake. Si wanasema dalili ya kichaa ni kurudia kufanya kile kile siku zote na kutegemea matokeo tofauti? Ulitaka Lissu aendelee kuwaomba watu wa serikali ambao siku zote wanampiga dana dana?

Amandla...
Wewe ndo kichaa kama Rais alikutana naye na hakutoa malipo kwaiyo mwanaye asiye na cheo chochote ndo anaweza kumlipa?
 
Kwamba Wenje amemwona kwa mara ya kwanza shereheni, hapo hapo akaanzisha suala la madai ya Lisu na kufikia hatua ya kumpigia Lisu simu. Mtu ambaye ulikuwa humjui unakutana naye mara hiyo na kumuekeza matatizo yako. Kisha yeye anajotolea kumfuata nyumbani msaidiwa badala ya kumtaka mwomba msaada kumfuata.
Aiseh
 
Inawezekana kabisa ukizingatia pia kuna pesa ambayo Wenje alikuwa anategemewa atalipiwa kutokea malipo ambayo Lissu angelipwa na serikali, imetokea wamekaa na mtu wa karibu kabisa wa demigod wa nchi akaona ngoja ajaribu bahati yake labda wanaweza kumtendea Lissu haki yake na yeye akaambulia shillingi alizotumbukiza kuokoa uhai wa Lissu.
Huo ni uzwazwa, kujipendekeza Hilo litawatesa Sana wapinzani, kulialia
 
Nimesikiliza maelezo ya Ezekiel Wenje aliyetuhumiwa na Lissu kumpeleka Abdul kumuhonga pesa, ukiniuliza mimi naona maelezo ya Wenje yamenyooka sana kuliko tuhuma alizokuwa anarusha Lissu dhidi ya watu anaodai wamehongwa.

Swali ambalo limebaki sasa ni kwamba Lissu anafanya mambo haya kwa sababu au faida zipi ukizingatia inaleta mgawanyiko sana ndani ya chama chake!

Nilikuwa nasubiria kwa shauku kumsikia Mbowe atajibu vipi tuhuma za watu wake kuhongwa pesa za Abdul lakini maelezo ya Wenje yamenyooka sana, yanatosha na naona yana ukweli mkubwa kuliko tuhuma za Lissu.
Kwani wenje kasemaje ili tuamini kuwa kanyooka kimaelezo,pointi ni zipi hasa tudadavulie mkuu
 
Mbowe is the right person in the wrong time .

Mbowe ni amefika kiwango chake cha mwisho he has nothing to offer

Akiendelea ataharibu .
Na CCM wameliona hilo jambo ndio wanataka wapitie hapo kuwa wanapata mseleleko
 
Nimesikiliza maelezo ya Ezekiel Wenje aliyetuhumiwa na Lissu kumpeleka Abdul kumuhonga pesa, ukiniuliza mimi naona maelezo ya Wenje yamenyooka sana kuliko tuhuma alizokuwa anarusha Lissu dhidi ya watu anaodai wamehongwa.

Swali ambalo limebaki sasa ni kwamba Lissu anafanya mambo haya kwa sababu au faida zipi ukizingatia inaleta mgawanyiko sana ndani ya chama chake!

Nilikuwa nasubiria kwa shauku kumsikia Mbowe atajibu vipi tuhuma za watu wake kuhongwa pesa za Abdul lakini maelezo ya Wenje yamenyooka sana, yanatosha na naona yana ukweli mkubwa kuliko tuhuma za Lissu.
Kukubaliwa kulipwa haki yako Kwa masharti nayo ni hongo.Huwenda alipewa masharti. Hilo nalo linahitaji D MBILI Kulielewa?
 
Wenje ameelezea hilo kwamba ni kawaida duniani kote kutumia watu maarafu au walio karibu na viongozi kushawishi kukwamua mambo yanapokwama, japo hili kweli ni tatizo la kimfumo lakini sio rushwa kama inavyoelezwa na Lissu kwa maana ya "pesa za Abdul".
Kama ni rushwa anaweza kusema live??
 
Nimesikiliza maelezo ya Ezekiel Wenje aliyetuhumiwa na Lissu kumpeleka Abdul kumuhonga pesa, ukiniuliza mimi naona maelezo ya Wenje yamenyooka sana kuliko tuhuma alizokuwa anarusha Lissu dhidi ya watu anaodai wamehongwa.

Swali ambalo limebaki sasa ni kwamba Lissu anafanya mambo haya kwa sababu au faida zipi ukizingatia inaleta mgawanyiko sana ndani ya chama chake!

Nilikuwa nasubiria kwa shauku kumsikia Mbowe atajibu vipi tuhuma za watu wake kuhongwa pesa za Abdul lakini maelezo ya Wenje yamenyooka sana, yanatosha na naona yana ukweli mkubwa kuliko tuhuma za Lissu.
Yako wapi hayo maelezo ya wenje? Yaelekea na wewe Abdul amekupitia.
 
Umeshindwa hata kuandika muhtasari wa maelezo yake, japo kwa sentensi moja au mbili? Uandishi wako mbona wa mhemko sana?

Tutajadilije hapo sasa?
Ukiona hivyo ujue amepaliwa na hela za Abdul ndiyo maana anajitekenya mwenyewe.
 
Kwamba alionana na Abdul kwenye event,siku hiyo hiyo wakafahaniana na akaanza kumuelezea suala la Lissu,inaingia akilini kweli? Yaani uonane na mtu siku hiyo hiyo uzoeane naye kwa haraka tena kwenye sherehe? Anyway tutajua mengi
 
Wenje kajikanyaga kanyaga ovyo ovyo tu hajaeleza kile kinachodaiwa

Mara Abdul alisema Lissu tayari kashalipwa mara wakaenda kwa Lissu wakachukua nyaraka

Hapo kuna kitu behind the scenes tumefichwa.
Wenje hata ukimuangalia usoni tu unajua huyu ni mtu wa dili,janja janja nyingi.
 
Maelezo ya Lissu kama nimemuelewa vizuri ni haya:
1. Wenje aliongozana na Abdul kwenda nyumbani. Sijui kama alikuwa tayari na appointment na Wenje au la.
2. Alipofika Wenje akamtambulisha Abdul ambae Lissu alikuwa hamjui.
3. Wenje au Abdul wakamwambia Lissu kuna zawadi yake kama atapunguza makali dhidi ya serikali.
4. Ili kuthibitisha kuwa wana nia njema wakamtajia wengine ambao wamepewa zawadi. Ingawa haijasemwa lakini katika hao waliotajwa ni lazima Boss wake Lissu alikuwemo pamoja na wengine.
5. Lissu akawafurumusha na kuwaambia kuwa haongeki.

Inaelekea pia Lissu alishtaki kwa Boss wake lakini kwa mshangao akaona hamna hatua iliyochukuliwa dhidi ya Wenje. Ndio akajua kuwa kweli kuna wakubwa nyuma ya Wenje. Kwa vile alitoa hizo shutma kwenye Kamati Kuu ya chama chake kuna wenzake ambao nao walianza kukosa imani na uongozi wa chama. Halafu, hamadi, huyo huyo Wenje mtoa rushwa anatangaza nia ya kugombea nafasi ambayo Lissu ameishika. Lissu kwa kutambua kuwa Wenje ni mtu wa Boss na kujua uwezo wa Boss wa kucheza foul akajua kuwa kibarua chake kitaota nyasi. Ndio maana akaamua kushambulia nafasi ya Boss kwa sababu alijua hilo hawatalitegemea na attack is the best form of defence. Ndio maana tumefika hapa tulipo.

Amandla...
Kifupi Lissu alifanya counter attack
 
Back
Top Bottom