Maendeleo: Ndege za ATCL mbioni kuanza kutua Chato

Umeandika hii ukiwa umetumia kichwa chako vizuri au umejiandikia tu?.
 
Idadi ya watu haina uhusiano wowote na uwezo wao wa kupanda ndege.
 
Katika hao watu 4ml wangapi wanauwezo wa kupanda ndege?
 
Geita kuwa na uwanja wa ndege sio tatizo especially kutokana na shughuli zake!.

Tatizo ni location ya uwanja ulikowekwa ni x770 wangeuwekea Katoro ambayo ni mpakani mwa Geita (wilaya) na wilaya ya chato na pia ni jirani kabisa na Geita mjini.

Asilimia 99.8 ya abiria wote wa Geita ni wafanya biashara wa Madini na wafanya Kazi wa migodi ya GGM na centre yake ni Geita mjini.

Muda mwingine bongo haihitaji ufikiri sana maana utapata msongo wa mawazo bure.

Anyway muombee jirani apate maana hata asipokupa ugali kuna namna nyingine utafaidika!

As-salamu alaykum TANZANIA
 
Sijui chato inasifika kwa kitu gani! Kwa sababu kama ni madini tunasikia hasa Geita na kama ni Biashara zingine kama za nguo tunasikia Katoro na kama ni rais anakaa Dodoma au Dar- Kuna mtu anaweza kunisaidia?
 
Sijui chato inasifika kwa kitu gani! Kwa sababu kama ni madini tunasikia hasa Geita na kama ni Biashara zingine kama za nguo tunasikia Katoro na kama ni rais anakaa Dodoma au Dar- Kuna mtu anaweza kunisaidia?
Mheshimiwa akistaafu atakaa Chato hivyo wanafanya maamuzi ila kumfurahisha wasije kuwa wanajipu lililo iva.
Nawasilisha...
 
Waza kibiashara zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Geita ambayo Chato inatoka inachangia 330 billion kwa mwaka ni tajiri kutoka 1) Dar es salaam, 2) Mwanza 3) Geita. Mikoa kama Arusha, Dodoma , Tanga, mbeya inafuatia kwa mbali sana.

Na dhahabu imekwisha pita utalii au sekta nyingine yeyote kwa kuingiza mapato kwa uchumi wa Tanzania kwa mbali sana.

Ki uchumi sioni tatizo lolote tena wamechelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…