Uchaguzi 2020 Maendeleo yapi CHADEMA wataleta tofauti na ya chama kilichopo madarakani?

King Kong III wananchi hawana hela au wewe ndio hauna hela?
Wananchi including na mimi hatuna pesa.........Mkuu kama upo kwenye channel ambayo unapata pesa mshukuru mungu ,sisi tupo mtaani tunaona hali halisi,hali mbaya ,kitaa kuna njaa,kitaa pesa hakuna tunalia njaa kali......Ukiweza kufanya analysis utaona transactions za mizinga kwenye x-pesa imeongezeka.
 
MGAGAGIGIKOKO wewe tu! Kiwiliwili kinavuta hewa karne ya 21 but ... akili ya kikwenu, pre-historic in dimensions. Si uufiche tu?
 
Next time usipende kuwaongelea watu wengine mzee sema wewe huna ila sio hatunapesa lakini pia nimegundua why unawachukia matajiri
 
Kwakuwa historia inaonyesha hakujawahi kuwa na chama kingine tawala tangu tupate uhuru ndiyo maana mawazo mgando km haya yanajitokeza.

Ukizoea kulamba sukari, haizuii wewe kujua kuwa kuna sukariguru na asali pia ambazo zaweza kuwa mbadala wa sukari unayolamba!
 
2. Maendeleo yapi CHADEMA wataleta tofauti na chama kilichopo au zaidi ya chama kilichopo?

Tukiangalia kwenye chama Chao maendeleo gani wameleta kwa watanzania?

Tokea nimfuatilie Tundu Lissu sijawahi kumuona akijitolea kusaidia mwananchi yoyote wa kawaida kupitia taaluma ya uanasheria aliyonayo zaidi anaitumia kwaajili ya chama chake Je unaamini hivi atawasaidia watanzania akiwa madarakani
[/QUOTE]

Wakati Lissu akimsimamia Max Melo founder wa hii JF kwenye kesi zake mlizombambikia na serikali yenuyakidhalimu alikua akikisaidia Chama pale?
Puguani mkubwa wewe...hata Melo akisoma hiitaka taka uliyoiweka haps nadhani atajuta kuruhusu watu Kama nyinyi kupata access ya JF..
Huo upuuzi wako wewe andika kule kule kuhusu WCB yenu na usiulete humu!
 
Wewe piga kura chagua Serikali ya Chadema, halafu uje kutoa ushuhuda hapa, Tanzania haijawai kuongozwa na chama kingine tangu uhuru, hivyo huwezi kuwaaminisha raia kwamba Chadema hawajafanya kitu wakati hawajawai kuongoza serikali, Sasa ni wakati raia tuipe ridhaa CHADEMA iunde Serikali halafu miaka mitano baadae uje uposti hapa.
 
We unavyozani ukimchagua Lissu ndio atakuletea hela mfukoni?
Haki,Uhuru na Maendeleo ya watu.

Ndio tatizo la kutokujua sera zaidi ya ushabiki....Soma vizuri ilani ya chadema halafu kisha uje kujijibu na swali lako.

Akiingia Lissu.
-Atarejesha fao la kujitoa hivyo nitaenda kuchukua fedha zangu NSSF.
-Atapunguza makato ya Loan Board kuja 3% hivyo 12% itaongezeka kwenye mapato yangu.
-Kodi ya PAYE atoapunguza hadi kuja single digit hivyo salary itaongezeka.
-Atapunguza VAT kutoka ya sasa 18% hadi 10% hivyo bidhaa zote zitashuka bei kwa 8%
-Atarudisha utawala wa mamlaka kwa watu,watu ndio watakuwa wanaamua no more ubabe.

Vitu ni Vingi....
 
Nakuhurumia Sana mzee baba hivyo ndio wanasiasa walivyokudanganya Kama alisema Lowassa Ni fisadi baadae akageuza gia angani akamwita msafi unaamini vip hivyo vitu vilivyoandikwa kwenye ilani atavitekeleza?
 
Pole sana,
Umeisha dumaa kiakili, yaani huoni kuwa uhuru, haki na maendeleo ya watu, ndio stahili zako?
Unyonge huu lazima ufike mwisho 28/10.
 
Kama mazuzu wanamtegemea Polepole ndio 'awafafanulie'.
Mwana CCM haruhusiwi hata kuitazama ilani ya uchaguzi ya CHADEMA.
Akikutwa ni hatari hata kwa maisha yake.
Kilichobaki ni kupiga na kulinda kura ZETU ili kuwakomboa hawa waTz wenzetu waliyopotea.
Tarehe 28/10 ndio siku yetu ya ukombozi.
 
Ndugu kapumzike, ni dhahiri kuwa umekaukiwa kabisa hoja za msingi, kama alivyo mgombea wenu.
Ni aibu kubwa kwa watu wa chama kikongwe namna hii, kuendelea kuokoteza vi hoja na vioja duni kuliko hata vya watoto wa chekechea.
Wale tuliobahatika kushuhudia zama za muasisi wa chama hicho na uwezo wa kujenga na kufafanua hoja, sasa hivi ni mwendo wa kuziba nyuso zetu kwa viganja vya mikono, kwa soni.
 
Naona unaelezea kuongoza nchi sio rahisi!!!
Je we umejuaje kua sio rahisi ni kazi ngumu? Una uzoefu na kuongoza nchi?

Au unaongelea kitu usichokijua?
 
Kwanza kabisa kabla ya kuleta hayo maendeleo Chadema watakuwa na kazi ya kuturudisha kwenye reli maana tumeshapoteza direction.
 
Ujobile/Umesema
 
Yaani bandiko ya wanaccm kwasasa ukisoma utangulizi tu umemaliza kilichomo kwenye bandiko zima,alafu yote yanafanana.

Kwa rasilimali tulizokuwa nazo toka uhuru,ingalitumiwa kuwapa watu na nchi maendeleo sasa hivi tungekuwa mbali kabisa
Lakini chama hikihiki kimeongoza nchi bila mafanikio.
Watu mpk karne hii bado wanakula ugali na kachumbari tena kwa taabu na jasho jingi.

Mmechokwa,kwanini mnalazimisha kutawala watu waliowakataa?
CCM+JIWE NI TATIZO
Kwanini umlazimishe mke kuwa nawe wakati amekuchoka?
ONDOKENI,HAKUNA ANAYEWAOENDA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…