Maeneo ambayo Waislam wanawapiga Bao Wakristo

Maeneo ambayo Waislam wanawapiga Bao Wakristo

Hawezi kutenga usabato na Ukristo,hapo kachemsha,,,unajiita mkristo huku anashindwa kuilinda Imani yake.....(nilivyokuwa Sunday school mwalimu alituambia atakuja mpinga kristo siku moja na panga atakuuliza unachagua Ukristo au unaukana,?teacher akasisitiza,ukiukana moja kwa moja motoniiii,,,,we nilisema sitaikana Imani yangu,niliogopaaaaa🤣🤣🤣🤣🤣🤣) Sasa huyu kijana anaonekana ni mwepesi Sana kwenye Imani.

Imani inalindwa Kwa kutenda Mema, kupenda wengine, kuona ukweli na kuusema, kutenda HAKI Kwa wote pasipo kupendelea. Hiyo ndio Imani ya kweli.

Ukristo na uislam au vyovyote vile ni matawi katika mti mmoja ya kuhakikisha Watu wanakuwa Watu Wema, Watu Bora katika kuishi katika mapito Yao hapa Duniani.

Watibeli ni Watu wasiolimitiwa katika kutafuta ukweli na Haki. Popote penye ukweli na Haki, na Wema Sisi tunachukua mazuri tuu.
Ninapenda Sabato Kwa sheria kadhaa zilizonjema, ninapenda Ukristo Kwa sheria kadhaa zilizonjema, ninapenda uislam Kwa sheria Fulani zilizo njema, ninapenda Uafrika Kwa sheria kadhaa zilizo njema.

Ndivyo Watibeli tulivyo.
Karibu Sana Mkuu
 
Robert Heriel umepata shida gani kuanza kudhalilisha Ukristo. Dini uliyoipokea na kukuwezesha wewe leo kutambua taranta yako ya uhandishi kupitia mifumo iliyojikita kwenye Ukristo kama shule n.k.

Tafakari sana Robert.

Hakuna sehemu niliyodhalilisha Ukristo Mkuu.
Nilichosema ni Ukweli.

Hata Yesu alipokuwa akisema ukweli, dini yake ya Uyahudi iliona anatukana Wayahudi (dini) lakini hakuwa akifanya hivyo.

Embu niambie kipi nimesema Uongo hapo?
 
Kumkataa BWANA YESU Ni kuukataa uzima wa milele

Uzima wa milele ni kumjua Mungu wa kweli na wajumbe wake,
Swali litakuja, wajumbe wake ni kina Nani?
MTU yeyote Mwema, atakayekupa habari njema na ya Haki ujue huyo ni mjumbe wa Mungu.
 
Wazungu hawana mahari, wanaendelea na utamaduni wao, dini haijaingilia wala kuharibu chochote.

Usisahau kwamba ishu za mahari kwenye Quran ni utamaduni wa waarabu, mirathi nk.

Sasa tunazungumzia Ukristo Vs Uislam.

Mfano ishu ya Mahari hapo, Kwa nini dini kubwa kama Ukristo imeshindwa kutoa muongozo kwenye Jambo kama Hilo na kuachia Mila na desturi ambazo hapohapo Mila hizo kuna Wakati Ukristo unazichukulia kama Ukafiri na upagani.
Tofauti na uislam, wenyewe ni mfumo mzima ambao unatoa sheria, Kanuni na taratibu Kwa karibu kila Jambo Kwa wanadamu, na hauachii Mila na desturi za Watu kujiamulia (kwani zipo Mila na desturi ambazo zinautata mkubwa ikiwemo upagani na ukafiri).
Hicho ndicho ninachoelezea.

Mfano ishu ya Talaka, ni ishu ambayo Kwa hakika ni lazima Watu waachane, lakini Wakristo hawajapewa hiyo sheria na hawana kifungu cha kurejelea kwenye sheria za Mungu(Torati). Zaidi Wakristo wanaachana kiholela(wakiamuliwa na sheria zisizo za dini Yao, kipagani au kikafiri). Bado huoni Hoja yangu.

Angalia Waislam, wao Talaka kwao ni sehemu ya ibada, laizma ifanywe Kwa kufuata Kanuni, kuna mambo ya Eda, n.k. bado huoni bao la kisigino hapo?

Mfano, Mwanamke akifiwa na mumewe kwenye uislam itampasa akae Eda Kwa muda Fulani(umetajwa Kwa sheria za kiislam) kisha ndipo Aolewe na Mwanaume mwingine ikiwa atataka. Hapo ni kuepusha mambo kama kubambikiwa mtoto.
Lakini Ukristoni hakuna kitu kama hicho. Bado hauoni Hilo ni Gap?

Umesema wazungu, Kwa hiyo kuna ukristo wa wazungu na Ukristo wa waafrika, na Ukristo wa Wachina na Wahindi?
Lakini uislam Duniani kote unafanana, bila kujali huyu ni mchina, muarabu, muafrika au vyovyote.

Unasema Mahari na mirathi ni utamaduni WA Waarabu. Walioandikwa kwenye Quran asilimia 90% ni Wayahudi, wakiwemo kina Yakobo, Moses, Yusufu, Daudi, n.k. na Waebrania wakiwakilishwa na Ibrahim. Hao ni Waarabu?
 
Watu msio na akili hutegemea kuungwa mkono kwa kila kitu, mkipigwa husema ni chuki. Hii ni open discussion, kaishi kwenye ulimwengu wa mataahira wenzio msiotaka kupigwa mnachokisema.
Napenda sana watu wanaojitambua kama wewe, wasioogopa kuhoji, wanaojiamini na kusimamia kile wanachokiamini, wasioogopa kupingwa na wajinga, wajinga wanachojua ni kuunga mkono kila kitu kwasababu ya upeo wao hafifu, wasamehe tu.
 
Mleta mada umezungumzia mengi kwenye bandiko lako ambayo kwangu sikubaliani nayo kwa asilimia mia, hapa nataka tuzungumzie suala la usafi.

Unaposema wanawake wa kiislamu wamewaacha mbali mno kwenye suala la usafi wale wasio waislamu [wakristu] unakuwa umetumia kigezo gani kuhitimisha hivyo?

Nijuavyo, usafi unajumuisha yafuatayo, kuoga, kuswaki, perfume, na mengine..

Sasa kama wanawake wa kiislamu wanaoga kwa kutumia maji yale wanayotumia wasio waislamu..

Wanajipaka sabuni zile wanazotumia wasio waislamu...

Wanajipuliza perfume zile wanazopuliza wasio waislamu..

Wanaswaki kwa kutumia dawa za meno zile wanazotumia wasio waislamu..

Wanajipaka mafuta yale wanayojipaka wasio waislamu..

Wanavaa mavazi haya wanayovaa wasio waislamu, ukiondoa hizo nikab, ambazo siamini kama pekee ndio zinamfanya mwanamke awe msafi..

Sasa tueleze, kwenye mazingira hayo, ambapo unaona wamefanana matumizi ya vitu vingi vinavyohusika na usafi, unapoandika wanawake waislamu "wamewaacha mbali mno" wale wasio waislamu, unakuwa umetumia kigezo gani?

Unasema wao wamefundishwa usafi msikitini, kwa hiyo kuoga walifundishwa msikitini mpaka wanawake wakristu hawajui kuoga kwasababu hawakupitia mafunzo msikitini?

Kwamba kwako kuoga kwa mwanamke mkristu ni tofauti na anavyooga mwanamke mwislamu, tuseme wanawake waislamu wakioga wanasafisha miili yao, je, wanawake wakristu wakioga wanasafisha nini?

Au kwako wanawake waislamu wana sabuni zao, maji yao, perfume zao, dawa zao za meno nk wanazoogea na sio hizi zinazouzwa madukani?

Hata kwenye maeneo ya chooni ulipoandika, kwamba wakristo wengi vyoo vyao vichafu, nashindwa kukuelewa hii research yako uliifanyia wapi, hivi umewahi kupita huko uswahilini wanapoishi hao unaowasifia hapa ukayaona mazingira yao?

Nimeona wakati ukiandika hii mada yako ulikuwa umetawaliwa na mihemko iliyopitiliza, ungepunguza mihemko kidogo angalau ungeandika kitu kinachoeleweka zaidi, lakini sio kuandika "wamewaacha mbali mno" kwenye mazingira gani? haya tuliyopo au mengine?!
 
Kwahiyo unapinga au unafafanua zaid, ila nacho jua uislamu ni wasiku nyingi kuliko uyahudi Jewish
Unafahamu utahudi? Haya nieleze Uyahudi ulianza lini na Uislam ulianza lini?
 
Unafahamu utahudi? Haya nieleze Uyahudi ulianza lini na Uislam ulianza lini?
Mkuu mimi sijui mambo ya kubishana kwa dini, kama wewe una hoja na maelezo kuhusu mwanzo wa hizo dini wekeni hapa tuisome tukubaliane na wewe au tukupe sisi tulicho kua tunajua ila sio kubishana kama walokole wanavo fanya.
 
Mleta mada umezungumzia mengi kwenye bandiko lako ambayo kwangu sikubaliani nayo kwa asilimia mia, hapa nataka tuzungumzie suala la usafi.

Unaposema wanawake wa kiislamu wamewaacha mbali mno kwenye suala la usafi wale wasio waislamu [wakristu] unakuwa umetumia kigezo gani kuhitimisha hivyo?

Nijuavyo, usafi unajumuisha yafuatayo, kuoga, kuswaki, perfume, na mengine..

Sasa kama wanawake wa kiislamu wanaoga kwa kutumia maji yale wanayotumia wasio waislamu..

Wanajipaka sabuni zile wanazotumia wasio waislamu...

Wanajipuliza perfume zile wanazopuliza wasio waislamu..

Wanaswaki kwa kutumia dawa za meno zile wanazotumia wasio waislamu..

Wanajipaka mafuta yale wanayojipaka wasio waislamu..

Wanavaa mavazi haya wanayovaa wasio waislamu, ukiondoa hizo nikab, ambazo siamini kama pekee ndio zinamfanya mwanamke awe msafi..

Sasa tueleze, kwenye mazingira hayo, ambapo unaona wamefanana matumizi ya vitu vingi vinavyohusika na usafi, unapoandika wanawake waislamu "wamewaacha mbali mno" wale wasio waislamu, unakuwa umetumia kigezo gani?

Unasema wao wamefundishwa usafi msikitini, kwa hiyo kuoga walifundishwa msikitini mpaka wanawake wakristu hawajui kuoga kwasababu hawakupitia mafunzo msikitini?

Kwamba kwako kuoga kwa mwanamke mkristu ni tofauti na anavyooga mwanamke mwislamu, tuseme wanawake waislamu wakioga wanasafisha miili yao, je, wanawake wakristu wakioga wanasafisha nini?

Au kwako wanawake waislamu wana sabuni zao, maji yao, perfume zao, dawa zao za meno nk wanazoogea na sio hizi zinazouzwa madukani?

Hata kwenye maeneo ya chooni ulipoandika, kwamba wakristo wengi vyoo vyao vichafu, nashindwa kukuelewa hii research yako uliifanyia wapi, hivi umewahi kupita huko uswahilini wanapoishi hao unaowasifia hapa ukayaona mazingira yao?

Nimeona wakati ukiandika hii mada yako ulikuwa umetawaliwa na mihemko iliyopitiliza, ungepunguza mihemko kidogo angalau ungeandika kitu kinachoeleweka zaidi, lakini sio kuandika "wamewaacha mbali mno" kwenye mazingira gani? haya tuliyopo au mengine?!

Mkuu nashukuru Kwa mchango wako.

Kuhusu suala la usafi Hilo mbona lipo wazi Kabisa.
Angalia Binti za kiislam (sio wote) akiingia chooni hata kukojoa, mtazame utakufa kabeba kopo Dogo lenye maji ya kujisafisha Baada ya kukojoa. Hii pia inatumika Kwa wanaume wa kiislam (sio wote) Ila ni wengi ukilinganisha na Wakristo ambao hawafanyi hivyo.

Njoo chooni, Waislam wakienda chooni wanamalapa ya chooni ambayo ukifika utayakuta pale. Waislam hawaingii na viatu ndani ya nyumba zao. Waislam hawaingii na viatu katika nyumba za ibada ikiwemo misikitini.
Lakini Wakristo hufanya kinyume na wao.

Usafi ni pamoja na vyakula, Waislam hawali Nguruwe, Waislam hawaruhusiwi kushika hata wanyama ambao ni najisi. Hiyo ni Kwa Imani Yao. Lakini vipi Wakristo? Achana na wasabato ambao ni kundi Dogo. Nazungumzia Wakristo katika ujumla wao.

Waislam wakienda kuswali lazima wajiswafi, watawadhe miguu Yao, suruali zenye mikojo au nguo za ndani zenu mikojo hazitakiwi misikitini.
Lakini vipi Kwa Wakristo?
Ukristo wenyewe unadai usafi wa Roho, lakini uislam umejikita kwenye usafi kuanzia kwenye Mwili, rohoni Hawana uthibitisho.

Ukiambiwa usafi sio tuu kuoga, ni zaidi ya Hapo.

Usiwaonee Wivu ninapowasifia Mkuu, Kwa sababu kunawakati pia ninawaponda na kuwakosoa Kwa Yale ambayo ninayona kwao wamepuyanga.
 
Halafu sijui kuna uhusiano gani kati ya uislamu na biashara.

Walio wengi wa wafanyabishara na matajiri Kinyongo bongo na kiafrika Afrika ni waislam.
 
Halafu sijui kuna uhusiano gani kati ya uislamu na biashara.

Walio wengi wa wafanyabishara na matajiri Kinyongo bongo na kiafrika Afrika ni waislam.
Kuna maelekezo ya mtume (SAW) kwamba mambo matatu ni katika dini:

1. Muumini kuwa na chanzo binafsi cha mapato.

2. Muumini kumiliki makazi yake binafsi (nyumba).

3. Muumini kumiliki kipando (usafiri wake binafsi).
 
Back
Top Bottom