Mkuu nashukuru Kwa mchango wako.
Kuhusu suala la usafi Hilo mbona lipo wazi Kabisa.
Angalia Binti za kiislam (sio wote) akiingia chooni hata kukojoa, mtazame utakufa kabeba kopo Dogo lenye maji ya kujisafisha Baada ya kukojoa. Hii pia inatumika Kwa wanaume wa kiislam (sio wote) Ila ni wengi ukilinganisha na Wakristo ambao hawafanyi hivyo.
Njoo chooni, Waislam wakienda chooni wanamalapa ya chooni ambayo ukifika utayakuta pale. Waislam hawaingii na viatu ndani ya nyumba zao. Waislam hawaingii na viatu katika nyumba za ibada ikiwemo misikitini.
Lakini Wakristo hufanya kinyume na wao.
Usafi ni pamoja na vyakula, Waislam hawali Nguruwe, Waislam hawaruhusiwi kushika hata wanyama ambao ni najisi. Hiyo ni Kwa Imani Yao. Lakini vipi Wakristo? Achana na wasabato ambao ni kundi Dogo. Nazungumzia Wakristo katika ujumla wao.
Waislam wakienda kuswali lazima wajiswafi, watawadhe miguu Yao, suruali zenye mikojo au nguo za ndani zenu mikojo hazitakiwi misikitini.
Lakini vipi Kwa Wakristo?
Ukristo wenyewe unadai usafi wa Roho, lakini uislam umejikita kwenye usafi kuanzia kwenye Mwili, rohoni Hawana uthibitisho.
Ukiambiwa usafi sio tuu kuoga, ni zaidi ya Hapo.
Usiwaonee Wivu ninapowasifia Mkuu, Kwa sababu kunawakati pia ninawaponda na kuwakosoa Kwa Yale ambayo ninayona kwao wamepuyanga.
Angalau hapa sasa umepunguza ile mihemko ya mwanzo, umeanza kutumia maneno sio wote, tofauti na mwanzo.
Hao wanawake wa kiislamu unaosema wakiingia chooni watakuwa na maji ya kujisafisha, mbona hilo ni kawaida tu kiafya, wanawake wote wanashauriwa kwasababu za maumbile yao, wahakikishe sehemu zao za siri zinakuwa safi kila wakati, hili hata kwa wanawake wakristu nimelishuhudia mara nyingi, hivyo napinga unavyotumia kigezo hiki kuwafagilia wanawake wa kiislamu.
- Suala la malapa ya chooni, hapa napo nakushangaa, hii sio sababu ya kuhalalisha usafi wa wanawake wa kiislamu, kwasababu, malapa yoyote, ilimradi yawe masafi, mtu yeyote anaweza kuingia nayo chooni, hii mentality yako ni kama vile mtu kila mara akiingia chooni anaenda kukanyaga mavi, wacha haya mawazo, hata vyumbani mwao, wanaingia na viatu vikiwa safi, haina maana wanakanyaga vumbi/tope na kuingia nalo ndani, hapa napo nakupinga.
- Nakuona unagusia mpaka suala la najisi, sijui umeyatoa wapi hayo mamlaka, katazame nini maandiko ya biblia yanasema kuhusu najisi. Mambo ya nguo za ndani kutonuka mikojo, kwahiyo kuna wanawake wakristu huingia kanisani na chupi zinazonuka mikojo? hii mada yako haina uthibitisho wa vingi.
Huo usafi wa zaidi ya hapo ni upi ambao wanawake wakristu hawana?
Ninapoona mapungufu ya wazi kwenye hoja zako, nakuonesha upungufu huo, halafu unaniambia nawaonea wivu, ndio nazidi kuona vile uliandika hii mada yako ili kutafuta sifa tu, usifiwe na hao unaowapamba, lakini sio kuelimisha, ndio maana mwanzo nikakwambia, ulielemewa sana na mihemko wakati ukiandika haya.
Nimekwambia, pita huko uswahili uyaone maisha wanayoishi hao unaowasifia hapa, halafu rudi usome hiki ulichoandika hapa uone kama kina mantiki, ndio maana nikakuuliza, unavyosema "wamewaacha mbali mno" kwenye mazingira gani? haya tunayoishi, au kuna mengine kichwani mwako?
Kama wewe ni mstaarabu, waombe radhi wanawake wakristu kwa namna ulivyowaandika hapa.