Maeneo ambayo Waislam wanawapiga Bao Wakristo

Sio marketing, dini kwetu ni total way of life

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Wakristo tatizo lao ni kupokea kila kitu bila msingi wowote.
Wao wanaona ni bora kulisaidia kanisa kuliko watu wenye uhitaji.

Kuna jumapili moja nilienda kanisani, kukawa na sadaka 2. Moja ni ile ya kawaida ambaho najua kazi yake.
Hii ya pili ilikua ni mashindano ya matoleo kati Me na Ke, nilishangazwa sana na hili. Yaani utoe tu afu wiki ijayo uje usomewe kua ni jinsia ipi ilitoa zaidi.
 
Kuna sekta waislam wako njema.

Ila ni kama ukristo tu wanaouharibu ni baadhi yao, ila wana misingi mizuri ya maisha.
Sema baadhi ya waislam wanaoendesha dini kwa hisia ndo wanaharibu, wanadharau dini nyingine, wanatukana watu humu mitandaoni.

Kuna jamaa id yake nimeisahau, ni muislam ambae hata umtukane yeye anakujibu kwa staha tu bila kurudisha kejeli wala tusi. Sio hawa kina FaizaFoxy kidogo tu kakudhihaki, kaidhihaki dini yako nk. Binafsi nawaelewa sana watu wa hivo sio hawa wabwatukaji
 
Nje na Quran, kuna kitabu kingine Chochote hata cha kihistoria kinachothibitisha hayo madai yako?
Quran ndo umul kitabu mother of all hollybooks, vitabu vyote vya nyuma yake viliunganishwa humo baada ya watu kuingiza maneno yao ie interpolluted and extra polluted, Quran ndo final source of law/sheria hamna kitabu kingine wskika zaidi ya Quran na Muhammad ndo mtume wa mwisho hamna mtume mgine baada yake. Yoyote anae jitokeza anakua batili au impostor ch 2:2 Quran.
 
Tatizo wabongo uelewa bado mdogo sana.
Wakristo hawana Muongozo wa mahari,mazishi,talaka nk.
Hivyo hapo wanafuata mila zao kulingana na jamii husika.

Sasa mtu akifuata mila zake kwanini tena unaulaumu ukristo badala ya kulaumu mila zake??
Mkristo akiamua kutozika bali kuchoma maiti kulingana na mila zake bado hakatazwi.

Kwahyo kwenye maswala ya mazishi,talaka,mahari msiufananishe uislam na ukristo...fananisheni uislam(tamaduni za waarabu) na tamaduni za kimila za kitanzania.

Mnajishughulisha sana na maswala ya kidunia ya kimwili wakati ukristo umebase kwenye maswala ya kiroho
 
Niliwahi kumsikia Shekh mmoja anasema walikuwa na kikao Cha pamoja na Mapadri, basi wakaambizana kila Dini (Waislam na Wakristo) waseme chochote kizuri kuhusu Dini nyingine.

Waislam wakasema uzuri ktk Ukristo ni wafuasi wao wanavyo watii viongozi wao, ni watiifu sana. Na Wakristo wao wakasema uzuri ktk Uislam ni wafuasi kuhudhuria Kwa pamoja swala 5 Kila siku.

Yule Shekh aliyekuwa anasema hayo akasema anatamani Waislam wangekuwa watiifu Kwa viongozi wao kama Wakristo.
 
Kwenye maziko nakurekebisha kidogo. Kwa wakristo we umeangalia mjini ambako watu wanaona msiba ni fasheni na sehemu ya kujibrand..huku vijijini hatupo hivyo. Majeneza yetu yapo simpo tu na wala hatuhitaji vazi jipya au mavazi ya wafiwa.

Hata chakula chetu sio ishu..tunaweza changiana unga tukanywa uji basi..tumemaliza.
 
Acha kulinganisha dini usije mkufuru Mungu dini zote ni nzuri

Na usafi au wema wa mtu ni yeye mwenyewe
 
Kuna swali ukijiuliza nadhani utapata hamu ya kujua zaidi ya hapo ulipo. Je mitume/watu wema kabla ya Abraham walikuwa ni dini gani? i.e. Noah, Enoch ect. Hakuna anayepinga kwamba waliongozwa na Mungu mmoja tunaemuabudu sie, ama sivyo?
Kwa mafundisho ya kiislamu ni kwamba wote hao walikuwa ni waislamu ila huo unaoitwa uyahudi ilikuwa ni jamii ya watu ambao kwa bahati kupitia kwao walitoka mitume wengi waliokuwa referenced kwenye vitabu vya muongozo kutoka kwa Allah i.e. Zaburi, Taurati, Injiil na Quran. Tazama namna Quran inavyo aknowledge vitabu kabla yake na mitume kabla ya Muhammad (SAW). Uislamu unaeleza wazi ya kwamba katika kila jamii alitumwa mjumbe kutoka kwa Mungu (Allah) until when the final revelation was made complete to manking through Muhammad (SAW) Quran 5:3.
According to Uislamu, dini ni mfumo wa maisha na sio tu kusali na kuamini. No wonder unaona superiority ya Uislamu kwa dini nyengine katika mambo yanayomfanya mwanadamu kuwa bora na kupatikana kwa jamii bora kupitia mafundisho yake kwasababu ni muongozo unaotoka kwa mwenyewe muumbaji wa mwanadamu (Allah).
 
Natamani sana uislamu. Shida ni Kujiripua na kuvaa mabomu. Ila ni wazuri sana hasa stara. Siyo huku kwetu watu wana roho mbaya kama sijui nini?
Tambua huko kujripua unakoongelea ni siasa za kimagharibi na makundi ya kigaidi waliyoyatengeneza wao wenyewe kwa maslahi yao kutoka Middle East. Soma historia then niambie wapi waislamu walikuwa wakijilipua kabla ya siasa za Marekani na middle East from the last 30 years? ukiangalia vizuri utagundua ni trend iliyo asisiwa miaka ya tisini kuja juu, je Hakukuwa na Uislamu kabla ya hapo? Leo hii ukiongelea waarabu na Uislamu umewekewa propaganda ya ugaidi, hebu tafuta narration ya wazungu miaka mia nyuma kama utakuta hizo arguments.
Ukifanikiwa kutoka katika hilo dimbwi la fikra wanalotaka wamarekani ubakie unaogelea ndo utaujua Uislamu wa kweli ni kitu gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…