Maeneo haya kampeni ya afya ya kinywa ikafanyike sana, hali ni mbaya

Mtu kama unampenda na unamtakia heru, ni kumwambia ile kijasiri na hakikisha ukimwambia mpe mbinu za kuikata hiyo hali kisha ,, zidisha ukaribu zaidi akipona baasi atakuona mtu wa maana sana.
 
1. Pemba
2. Unguja
3. Shinyanga
4. Mbeya
5. Kondoa

Nb maeneo hayo Nimeyapanga kutoka juu kwenda kwenye unafuu.

Mikoa hii hakuna wimbi la watu wanaonuka midomo hongereni
1. Kilimanjaro
2. Arusha
3. Tanga
4. Tabora
Descending Order......Hahaha.
 
Mtu kama unampenda na unamtakia heru, ni kumwambia ile kijasiri na hakikisha ukimwambia mpe mbinu za kuikata hiyo hali kisha ,, zidisha ukaribu zaidi akipona baasi atakuona mtu wa maana sana.
Huyu Dereva wangu nimeshindwa nimwambieje.....harafu mtu mzima. Yaani anatema mpaka unataka kutapika
 
Mada sensitive sana hii japo imekuja kimzaha kidogo.

Bahati mbaya wengi tunatuka vinywa na hatujui, walio karibu yetu wanaona haya kutuambia, so tunaendelea kutia aibu mtaani kwa kunuka vinywa.
 
Bei gan hiyo dawa
 
Shida ni kwamba yule muhusika Mwenye hy shida huwa kashaizoea hy harufu so kwake anaona kawaida haimkeri...pia Ukila Vyakula vyenye viungo vingi pia ni tatizo,kuna viungo mfano wa vitunguu Huwa vinaingia mpk kwemye damu,yan mtu aliyekula vitunguu vingi ile harufu Huwa inaenda mpk Kwenye damu so Huyu mtu akiwa anapumua Huwa anatoa hy smell Sasa mbaya zaid awe amepigwa jua kma lile la dar....utamchukia
 
Unaweza ukawa unapiga mswaki kila siku na harufu ikawa Pale pale.....ishu ni kwamba unapigaje Huo mswaki,na unapiga muda gani?
 
Ulimi unanuka Wazee asikwambie mtu...kwenye kupiga mswaki komaa sana na ulimi,kunywa sana maji mengi,pendelea kula malimao pia.
 
Huyu Dereva wangu nimeshindwa nimwambieje.....harafu mtu mzima. Yaani anatema mpaka unataka kutapika
Kimsingi tatizo ni kubwa kwa kweli. Dah kuna jamaa mmoja tulisafiri naye alafu barabara ya vumbi jamaa hawafungui kioo mnakula AC tu. Tulipata wakati mgumu kwenye gari maana si kwa harufu ile.
 
Wife huwa namchana. Ameenda kuoga sasa anapiga mswaki. Haiwezekani mtu akuletee limdomo mkisi huku unstoa harufu.
 
Hii ishu ni kubwa sana wazee...
Usione watu smtims anagombana na mkewe kila siku Afu wewe wa pembeni kila uliwaskiliza ujue sababu ya Maana hta huioni,wengine mpk wanaachana kabisa...ukiulizA sababu utaskia "hajatulia huyu","hajui kupika","anachelewa kurudi","hanisikilizi".....Yan unaweza ukashangaa hzo sababu zote unazoziskia zikawa si kweli ila sababu kuu ikawa ni mmoja ananuka mdomo na mwenzie katumia njia zote kumwambia imeshindikana,so kwa vile washazaa wanaishia tu kugombbana kila saa kila siku ila sasabu inaegemezewa na ishu nyingne kabisa...ile sababu yenyewe haswa haisemwi kwasbb kwanz ni aibu wao kwa wao Lakini ni aibu kuwaambia watu mke wangu ananuka mdomo....so Hiyo ishu Inakuwa kma zimwi hv lipo ndani linawatesa ila Mnashindwa kulimaliza

Katika uislam Mtume Muhammad s.a.w aliliona Hili na alijua linaweza kuleta matatizo makubwa sana ukipuuzia Lakini akasena hivi:
Lau si kuwa ningewalemea watu wangu, ningewaamuru wapige mswaki kila wanaposwali."*

Hii ni jinsi gani Mtume s.a.w anatia Uzito Kwenye hiyo ishu.
Lakini pia alikataza mtu aliyekula vitunguu kwenda kuswali mpk ajisaifishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…