Maeneo haya kampeni ya afya ya kinywa ikafanyike sana, hali ni mbaya

Maeneo haya kampeni ya afya ya kinywa ikafanyike sana, hali ni mbaya

Jamani pemba!!! 😭 Nilikuwa huko November 2024.

Asubuhi makazini si watu tunakuwa tumeoga tumepiga mswaki? Nategemea ndio muda watu wanakuwa wasafi kuliko muda wote. Ila hizo vumba zinazosikika…!!!!
Pemba ni hatari , ndio maana nimeikweka ya kwanza , nimekaa miaka 2 huko.
 
Kunuka mdomo kwa zama hizi ni kujitakia
Hv tuseme uliwanusa au inakuaje kuaje
 
Mademu zao vipi wanajua kukususia ujilie hadi umwage ubongo?
Hao wanajitakia , wengi hawapigi mswaki ...kuna wala mirungj na sigara wanajisahau sana ..Mtu akishakula hayo madude anaona mdogo uko sawa ila ananuka.

Wengi wakiamka wanavuta sigara au kunywa kahawa basi mpaka anasahau kusafisha kinywa.
 
Watu wanaoishi kwenye maeneo yenye maji yenye flourine nyingi kama Arusha huwa na meno magumu sana. Hayatoboki kirahisi na kuleta harufu. Ila hiyo hiyo flourine husababisha meno yao kuwa ya brown. Wengine wale sugu harufu hutoka tumboni, hawa wajiepushe nyama nyama na vyakula vyenye mafuta mengi.
 
Namba 1 na 2 mkuu naunga mkono 100% na 100% zingine na nakuongeza zingine 100%
Hawa jamaa sijui tatizo ni ushamba ama elimu au umasikini maana umasikini ni wa kiwango cha juu sana huko.
Uchafu kwao ni sehemu ya maisha yao.
Sio wanawake wala wanaume wanashindana kwa uchafu.
Wao wakishavaa zile nguo nyeupe na nyeusi wanajiona wasafi tayari.
% kubwa wameanza kununua na kulalia magodoro 2020 na wameongezeka 2023.
Serikali ipeleke elimu ya usafi wa jumla Pemba na Unguja.
 
Jamani pemba!!! 😭 Nilikuwa huko November 2024.

Asubuhi makazini si watu tunakuwa tumeoga tumepiga mswaki? Nategemea ndio muda watu wanakuwa wasafi kuliko muda wote. Ila hizo vumba zinazosikika…!!!!
Hapa JF Maghayo Busu la Kenge anaongoza kwa kunuka domo yaani linavuta mibange yake linakuja Jf kuchat sasa changanya domo baya na miharufu ya bange ni shida tupu.
 
Kuna dawa inasemekana haziondoa harufu mdomoni, pendekezeni na dawa nzuri za kutumia. Kuna dawa ya meno inaitwa eternal, hii ni kiboko, hapa tunasaidiana siipigii promo dawa
 
Ambao wamesoma dawa ya meno ya Red wakavutiwa nayo wajue zipo za aina mbili kuna moja iko poa sana unakua fresh kuna nyingine ukishaitumia in 4 hours unaanza hisi kinywa kinakua na harufu ya hovyo.

Nikagundua Red yenye doa la kijani ni nzuri kuliko yenye doa jekundu. Jina refu la hii dawa ni Red (Dabur).

Pia ni vizuri mtu ukiwa na floss sticks, badala ya hizi toothpick ambazo hazipiti katikati ya meno. Floss sticks zinapita kila sehemu na zinaondoa mabaki vizuri mno.
 
Back
Top Bottom