Duuh!
Nimefatilia mtiririko wako na wa Mrangi, hata sijui nianzie wapi
Yaani mmenijkumbusha mbali sana, daah kweli nimezeeka
Miaka hiyo kuanzia Upanga late 80s Mtaa wa Mindu, Jack Pemba mtoto mdogo brazameni wa kuzamia harusini, kaka yake Chuche ndio Mwamba wa Local Gyms. Kaka Mkubwa walikuwa wanamuita Terrorist ndio Gangster wa miaka hiyo na kijiwe chao INDIANA.
Tukija Don Bosco, yaani ukitoka tu shule, jioni upo ndani Football na kina watoto wa Mazyuni na kina Natepe
Basketball kina Maro, biotto , Mchungaji Ngomba, Papii
Coach Evarist, Coach Manase tunakipiga nao wote
Dj Kilosa anapiga misele na kandambili tu mitaani
Watoto wa kihindi na magari ya mashindano misele sana kuzungusha vi beetle LOVEBUG
Kijijini Upanga Tambaza kama unapajua mpaka leo vilevile
Kwenye mashindano brazameni Kolumba anasoma Azania akidanki nishangwe na makelele, Kina Kibo na Tyson wa Tambaza
Mashindano ya Don Bosco, kina sisi tulikuwa na vi fake All Star vya mtumba , Kina Janguo , Eric Mwenda, Marehemu Mpoki na Nigga one wana Original Nike Air Jordan.
Mara Mzee kapata promotion kazini, tumehamia Haile Sellasie road, miaka hiyo, ya Kina Rob D, Nigga one mtaani
Mzee wa watu Mzee Malai, nimecheza sana Basketball kwenye half court yake na kina Mazula na Warioba, halafu tunaenda kuomba mechi na watoto wa IST
Aliwapeleka PAZI wote US miaka hiyo, wote wakarudi wengine bado choka mbaya bongo,
mrangi anaielewa sana mitaa, Miaka hiyo UDA ni moja kwenda Masaki, mara Mzee Tryphon Maji huyu hapa na kIBIBI
Haile Sellasie Road sasa ni kama Uswahili mara ya mwisho nimepita, vibaa na restaurant kibao, miaka hiyo ni Oysrebay kweli, watu wakizuzura wanaonekana kabisa wamepotea mitaa, Kimyaaaa