Mafanikio ya ATCL: Safari za moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Guangzhou China zaanza

Mafanikio ya ATCL: Safari za moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Guangzhou China zaanza

Shirika la ndege la Tanzania (Air Tanzania) imefanya safari yake kwanza leo alfajiri kuelea mji wa kibiashara Guangzhou nchini China.

Air Tanzania itakuwa inafanya safari zake moja kwa moja toka Dar es Salaam, Tanzania mpaka Guangzhou nchini China huku ikitumia takribani masaa 11 ikiwa angani.

#AirTanzaniaView attachment 1777180View attachment 1777179View attachment 1777178View attachment 1777182View attachment 1777181View attachment 1777184View attachment 1777183
Ilikuwa na abiria wangapi?
 
Tulitakiwa tuwe na rout nyingi za nchi za afrika ila rout kama za China na Dubai zipate kuleta matokeo mazuri.
 
... ila masaa 11 duh! Inge-stop japo Mumbai, India au Dhaka, Bangladesh, au Rangoon, Myanmar!
Wabongo hawakosagi kasoro .... Kwa long haul bado huo ni muda wa kawaida ndege ya kisasa sana huchoki sana sio kama enzi hizo tunasafiri na ndege choo kinanuka ...
 
Tulitakiwa tuwe na rout nyingi za nchi za afrika ila rout kama za China na Dubai zipate kuleta matokeo mazuri.
Lazima uwe na strategic plan sio kukurupuka tu starting point ni hiyo mengine yata kuja
 
Hiyo route atcl wakitulia watafanya sana biashara

Ova
Sanaaa!
Nchi jirani zote wanweza kutumia ndege hiyo na wakatua Dar Es Salaam na tukatumia zile ndege ndogo kuwa peleka ncho za karibu karibu , amabzo ni zaidi ya saba( Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Congo, zambia , Malawi, hata sudan kusini na somalia pia.
 
Hii route ni very strategic kwa Tanzania
Huu ni wakati sasa wa kuimarisha uchumi kama tunavojua Guanzhou ndio kama industrial hub ya Uchina.
Route ya pesa haswa ni dubai yaan hapo ndipo kuna pesa ipo wazi ila tuna bungua macho tu. Emirate wana leta boeng 777 -300 ER ni dege kubwaaa balaaa lina meza watu kama 290+ ikiwa full ...lkn hawa emirate wana lishushaa kila kuchwapo
 
Natamani kujua imeondoka na abiria wangapi, lakini pia inaweza kuwa kivutio cha utalii kitendo cha kutua kwenye viwanja vya watu natumai watasoma jina waijue Tanzania.
For the first time katika uwanja huo itaitwa "Air Tanzania flight number T255 JPM will be arriving shortly directly from Dar es Salaam Tanzania".
Watu wewee, ukiwa hapo uwanjani, lazima mwili usisimke.
 
Natamani kujua imeondoka na abiria wangapi, lakini pia inaweza kuwa kivutio cha utalii kitendo cha kutua kwenye viwanja vya watu natumai watasoma jina waijue Tanzania.
Wamepata 75% ya abiria ( 240 B787-8 capacity).
 
Route ya pesa haswa ni dubai yaan hapo ndipo kuna pesa ipo wazi ila tuna bungua macho tu. Emirate wana leta boeng 777 -300 ER ni dege kubwaaa balaaa lina meza watu kama 290+ ikiwa full ...lkn hawa emirate wana lishushaa kila kuchwapo
Hiyo route ngumu,kuna Emirates Airline na FLY DUBAI hapo,Fly Dubai nauli nafuu.
 
Hongera ATCL Gwanzuu ni mji muhimu kwa bidhaa solo la Africa
It's Guang Zhou...

Inatamkwa guang' (hii ng mwishoni inatamkwa kama ngi pasipo kuitaja hiyo i hapo mwisho)

na Zhou...inatamkwa kama njou...


Wabongo wengi si watafiti wa kutamka matamshi ya lugha za watu, basi huita huo mji kwa majina yao kama Guanzu, Gwanzu, Guangzu, Guazu n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Team corona kimyaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]wakati huko ndio chimbuko la ugonjwa aiseee
Wachina wameweza kuidhibiti sana Covid...

Tatizo pekee ninaloona litakuwa issue ni vikwazo kadhaa ambavyo pengine serikali ya Beijing itakuwa imeviweka kwa wasafiri wasio wakazi wanaoingia huko...

Mambo ya masharti ya chanjo, karantini n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba JINA la huyo Rubani ,nimemkubali masaa 11angani?[emoji16][emoji44]
Mbona ni standard kwa sababu ndege inayoenda moja kwa moja Baiyun na sio Beijing au Shanghai...

Mfano KQ, inatumia masaa 10 hadi 10.5 kati ya JKIA hadi Baiyun...

ET yenyewe inatumia takribani 9.5 toka pale Bole hadi Baiyun...

ATCL itakuwa inatumia muda zaidi kidogo kwa sababu nadhani 'barabara ya ndege' kwa ndege zinazotoka Afrika, lazima ziende kaskazini kidogo ndipo zianze kuelekea huko Uchina, sidhani kama ikinyanyuka tu hapo JNIA, inakata bahari ya Hindi kwenda mashariki...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom