Mafanikio ya ATCL: Safari za moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Guangzhou China zaanza

Mafanikio ya ATCL: Safari za moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda Guangzhou China zaanza

PICHA : Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) leo alfajiri limezindua rasmi safari za moja kwa moja Kutoka Dar es salaam hadi Guangzhou, China baada ya kuahirishwa mara kadhaa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo janga la Corona.

Uzinduzi huo umeongozwa na Mhandisi. Dkt. Leonard Madaraka Chamuriho, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi.

Hizi ni picha kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3, Raia wa China wakiwa kwenye maandalizi tayari kuanza safari.

... angekuwepo angeenda kuzindua na hili!
 
Wanaficha hili Mkuu wahuni hawa. Kama safari za kwenda chato hawakusema kama zinaingiza hasara kubwa sana hadi yule dhalimu aliporudisha namba. Hizi safari za China nazo bila shaka zitakuwa ni hasara tupu. Safari za India ambazo zimesitishwa wiki moja iliyopita kuna mtu namfahamu alienda huko February mwaka huu kwa matibabu. Kwenda na kurudi viti vilivyokuwa havina abiria ni vingi kuliko vilivyokuwa na abiria ila wahuni hawa wanapiga kimya.



Natamani kujua imeondoka na abiria wangapi, lakini pia inaweza kuwa kivutio cha utalii kitendo cha kutua kwenye viwanja vya watu natumai watasoma jina waijue Tanzania.
 
Hongera kwa hayati magufuli kwa kununua hizi ndege hijapo kuwa aupo nasi hila umeacha makubwa kwa kununua ndege ambazo alipigiwa kelele naamin zitaleta maendereo hapa 🇹🇿
 
Unasemea yule aliyesema ATCL inapata faida kumbe shirika linaingiza hasara ya 60bil per year?
Chuki zako kwa JPM haziwezi badilisha ukweli alifufua shirika la ndege.
Sasa hivi mnapata heshima na bado mnaongea vibaya.
Hata hivyo kumridhisha kila binadamu ni ngumu so endeleeni na drama zenu.
 
Magufuli miaka yote kashindwa mama ndani ya siku 60 tu shirika limeanza kutoa ndege nje...

Kweli rais tunaye..
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] hicho kibali chenyewe cha kwenda China kimekuja kupatikana mwaka huu mwezi wa kwanza ila changamoto kubwa ilikuwa ni Covid na kama utakumbuka mwezi wa 3 mwishoni ilibidi waanze safari lakini ikashindika wakasema watatoa tena tarehe y kwenda ndo hiyo ila yooote bado ukimuona mwewe wa ATCL utamkumbuka JPM
 
Hivi ndege ya abiria ina tofauti gani na ndege ya mizigo? Nifahamishe!

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Ndege ya mizigo kama ya mizigo inawekwa sakafu maalumu kwa kuwekea makasha/containers za mizigo za ndege na haina viti, vyoo na majiko. Huwa ina choo kimoja na jiko moja kwa wafanyakazi. Na ni kawaida sasa wafanyakazi ni marubani wawili tu. Ila ndege zote za abiria zinaweza kubeba mizigo kwa ama kutolewa viti na vyoo/majiko kwa muda lakini mizigo siyo kwa makasha maalumu.
 
Back
Top Bottom