Mnyonge mnyongeni ila haki yake Mpeni.
Nimekaa hapa nikawa natafakari utendaji kazi wa Rais wetu kipenzi “The Man himself President Magufuli”
Ki ukweli kazi kaifanya katika hii miaka yake miwili na nusu kwa sasa, achana na sisi tunaolalamika sijui maisha magumu mara mtaani pesa hakuna napenda kukuhakikishia kama hautaki kufanya kazi lazima tu maisa kwako yatakuwa magumu na utaendelea kumsingizia na kumchukia Mheshimiwa Rais bure.
Hebu jamani tujaribu kuona hapa mafanikio ya Mheshimiwa Rais japo kwa uchache na wale wajuvi zaidi watajaribu kinisaidia kwa kuongeza nyama
1. Tukianza na Sekta ya Elimu
Hili hata ungekuwa kipofu ata uwezi kubishana na mimi kuwa limefanikiwa kwa kiwango cha juu, nadhani tunakumbukumbu MH.Rais aliahidi elimu bure kuanzia Elimu ya msingi mpaka kidato cha nne na amefanya, sasa watoto wetu hatusumbuani maswala ya ada wala michango huko mashuleni kitu kilichopelekea wazazi wengi kupeleka watoto wao shule na ninahakika baada ya miaka kadhaa Tanzania itakua miongoni mwa nchi zenyeidadi kubwa ya wasomi.
Ukiangalia mpaka sasa kunaongezeko kubwa la wanafunzi wanaoandikishwa kujiunga na shule ya msingi. Mfano mwaka 2015 idadi ya wanafunzi wa shule ya msingi ilikuwa ni wanafunzi milioni 8,235… na kwa sasa tunajumla ya wanafumi miliono 10 na kitu unaweza kuona ongezeko lililopo hapo. Shule za sekpondari kwa mwaka 2015 tulikuwa na wanafunzi milioni 1,804056 kwa sasa tunawanafunzi takribani milioni 2,354234 kunaongezeko ku bwa sana hapo pia.
Mbali na kuongezeka kwa wanafunzi vifaa vya kufundishia na nyezo nyingine mashuleni vimeboreshwa mfano mzuri ni madawati, tatizo la madawati sasa limepungua kwa zaidi ya asilimia 80, walimu wa kutosha .
2. Tukija katika Nyanja au sekta ya Afya
Hapa napo hakuna mtui anaeweza kubisha ni kwa kiasi gani MH.Rais kajitaidi kutimiza kile alichokiahidi na badi muda anaomwingi sana kuendelea kuboresha na kukamirisha kile alichowaahidi watanzania, kipindi cha nyuma ilikua nadra sana ukaenda hospital ukamaliza kufaniwa tiba na kuandikiwa dawa ukaipata ile dawa uliyoandikiwa katika dirisha la hiyo hospitali ya serikali, sanasana utaambiwa uende duka lililo maali flani. Kwa sasa hiyo biashara haipo.
Serikali ya Rais magufuli imejitahidi sana katika swala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vingine, mfano MSD imeingina mikataba na umla ya wazalishaji wa dawa 110 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo wazalishaji 10 kutoka hapahapa nyumbani. Upatikanaji wa dawa muhimu kwa sasa umepanda hadi Asilimia 85 ukilinganisha na huko nyuma ambapo upatikanaji wa dawa muhimu haukufika hata asilimia 50.
Bajeti ya dawa na vifaa tiba kwa mwaka 2017-2018 ni bilioni 269 am bayo ni kama mara kumi ya bajeti ya mwaka 2015-2016 ambapo bajeti ilikua bilioni 29 tu.
Uboreshaji wa huduma mbali mbali mfano kwa sasa tunafanya upandikizaji wa figo hapahapa nchini kipindi cha nyuma wagonjwa wenye matatizo ya figo walitakiwa kupelekwa nje ya nchi. Hadi kufikia sasa hivi serikali imefunga mashine za upandikizaji wa figo zaidi ya 140 katika hospitali mbalimbali kitu ambacho ni maendeleo makubwa sana, hii ni kwa uchache tu.
3. Uboreshaji wa njia mbalimbali za usafiri na usafirishaji.
Hapa nitaongelea mifano mikubwa miwili ambayo ni Reli na usafiri wa anga. Tukianza na usafiri wa anga, hapa kila mtu atakuwa ni shahidi kuwa shirika letu la ATCL lilikua limekufa kabisa kilichokuwa kinasubiliwa ni mazishi tu, lakini huwezi kuamini lilivyofufuka ghafla baada ya MH.Rais kukamata madaraka tumeshuhudia haraka sana Rais alinunua ndege mbili aina ya Bombardier Q-400, sasa watu wanafika Kigoma, Dodoma, Katavi n.k kwa ndege kitu ambacho zamani ilikua hamna zaidi zaidi watu walitumia videge vidogo, lakini pia mwaka huu kuna madege mengina yatashuka ili kuimarisha zaidi usafiri wa anga ndani na nje bila kuisahau Boeing 787 itakayoleta balaa mjini.
Viwanja mbalimbali vya ndege vimeboreshwa ikiwemo kiwanja cha Mwanza, Mbeya, Bukoba na Julius. Pia kunaviwanja vipya vimejengwa na vinaendelea kujengwa maenep mbalimbali ikiwemo kile cha Chato.
Njoo kwenye Reli hapa ndio balaa lilipo Standard Gauge Railway ndio hiyo tena ikiwa ya kwanza katika nchi za Afrika mashariki na wengine wameamua kuiga mfano. Aitakuwa ajabu mtu kuishi morogoro lakini akawa anafanya kazi apa Jijini Dar es salaam. Hivi mnataka Rais afanye nini sasa, vitu ambavyo vilikua ndoto lakini sasa hivi ni halisi.
4. Ujenzi wa viwanda
Hili hata sina haja ya kulielezea maana kila mtu habari anayo
5. Vita dhidi ya Rushwa
Ili nalo sitakuwa na haja ya kulielezea naana kila mwenye akili timamu analijua. Wale ambao walikuwa wanaonekana malaika na mkono wa dola hauwezi kuwafikia habari wanayo na moto wanaona jinsi unavyowawakia kwa kujifanya mali ya umma ni ya kwao peke yao. Kwasasa mjini hapa akuna mbabe.
6. Ulinzi wa Raslimali zetu na Amani ya Nchi.
Hili nalo kila mtu ni shahidi, madini yetu kuwa watu walijifanya kama yao walichukua watakavyo na kuenda kuneemesha mataifa yao. Ambaye ana taarifa ni kitu gani kinaendelea apa anaruhusiwa kuniuliza nimpe habari.
Amani na utulivu naona kila mtu anashuhudia ni namna gani vinatamalaki. Akuna cha kuleta vyoko vyoko. Wale wote waliokuwa wakileta fujo fujo kipindi nchi hii ikionekana kama haina uongozi waijua ni nini hasa kinawapata kwa sasa. Kila nchi inautaratibu wake bana.
Nashukuru kwa leo na itaendelea…….