Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2021
Mnyonge mnyongeni ila haki yake Mpeni.

Nimekaa hapa nikawa natafakari utendaji kazi wa Rais wetu kipenzi “The Man himself President Magufuli”

Ki ukweli kazi kaifanya katika hii miaka yake miwili na nusu kwa sasa, achana na sisi tunaolalamika sijui maisha magumu mara mtaani pesa hakuna napenda kukuhakikishia kama hautaki kufanya kazi lazima tu maisa kwako yatakuwa magumu na utaendelea kumsingizia na kumchukia Mheshimiwa Rais bure.

Hebu jamani tujaribu kuona hapa mafanikio ya Mheshimiwa Rais japo kwa uchache na wale wajuvi zaidi watajaribu kinisaidia kwa kuongeza nyama

1. Tukianza na Sekta ya Elimu

Hili hata ungekuwa kipofu ata uwezi kubishana na mimi kuwa limefanikiwa kwa kiwango cha juu, nadhani tunakumbukumbu MH.Rais aliahidi elimu bure kuanzia Elimu ya msingi mpaka kidato cha nne na amefanya, sasa watoto wetu hatusumbuani maswala ya ada wala michango huko mashuleni kitu kilichopelekea wazazi wengi kupeleka watoto wao shule na ninahakika baada ya miaka kadhaa Tanzania itakua miongoni mwa nchi zenyeidadi kubwa ya wasomi.

Ukiangalia mpaka sasa kunaongezeko kubwa la wanafunzi wanaoandikishwa kujiunga na shule ya msingi. Mfano mwaka 2015 idadi ya wanafunzi wa shule ya msingi ilikuwa ni wanafunzi milioni 8,235… na kwa sasa tunajumla ya wanafumi miliono 10 na kitu unaweza kuona ongezeko lililopo hapo. Shule za sekpondari kwa mwaka 2015 tulikuwa na wanafunzi milioni 1,804056 kwa sasa tunawanafunzi takribani milioni 2,354234 kunaongezeko ku bwa sana hapo pia.

Mbali na kuongezeka kwa wanafunzi vifaa vya kufundishia na nyezo nyingine mashuleni vimeboreshwa mfano mzuri ni madawati, tatizo la madawati sasa limepungua kwa zaidi ya asilimia 80, walimu wa kutosha .

2. Tukija katika Nyanja au sekta ya Afya

Hapa napo hakuna mtui anaeweza kubisha ni kwa kiasi gani MH.Rais kajitaidi kutimiza kile alichokiahidi na badi muda anaomwingi sana kuendelea kuboresha na kukamirisha kile alichowaahidi watanzania, kipindi cha nyuma ilikua nadra sana ukaenda hospital ukamaliza kufaniwa tiba na kuandikiwa dawa ukaipata ile dawa uliyoandikiwa katika dirisha la hiyo hospitali ya serikali, sanasana utaambiwa uende duka lililo maali flani. Kwa sasa hiyo biashara haipo.

Serikali ya Rais magufuli imejitahidi sana katika swala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vingine, mfano MSD imeingina mikataba na umla ya wazalishaji wa dawa 110 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo wazalishaji 10 kutoka hapahapa nyumbani. Upatikanaji wa dawa muhimu kwa sasa umepanda hadi Asilimia 85 ukilinganisha na huko nyuma ambapo upatikanaji wa dawa muhimu haukufika hata asilimia 50.

Bajeti ya dawa na vifaa tiba kwa mwaka 2017-2018 ni bilioni 269 am bayo ni kama mara kumi ya bajeti ya mwaka 2015-2016 ambapo bajeti ilikua bilioni 29 tu.

Uboreshaji wa huduma mbali mbali mfano kwa sasa tunafanya upandikizaji wa figo hapahapa nchini kipindi cha nyuma wagonjwa wenye matatizo ya figo walitakiwa kupelekwa nje ya nchi. Hadi kufikia sasa hivi serikali imefunga mashine za upandikizaji wa figo zaidi ya 140 katika hospitali mbalimbali kitu ambacho ni maendeleo makubwa sana, hii ni kwa uchache tu.

3. Uboreshaji wa njia mbalimbali za usafiri na usafirishaji.

Hapa nitaongelea mifano mikubwa miwili ambayo ni Reli na usafiri wa anga. Tukianza na usafiri wa anga, hapa kila mtu atakuwa ni shahidi kuwa shirika letu la ATCL lilikua limekufa kabisa kilichokuwa kinasubiliwa ni mazishi tu, lakini huwezi kuamini lilivyofufuka ghafla baada ya MH.Rais kukamata madaraka tumeshuhudia haraka sana Rais alinunua ndege mbili aina ya Bombardier Q-400, sasa watu wanafika Kigoma, Dodoma, Katavi n.k kwa ndege kitu ambacho zamani ilikua hamna zaidi zaidi watu walitumia videge vidogo, lakini pia mwaka huu kuna madege mengina yatashuka ili kuimarisha zaidi usafiri wa anga ndani na nje bila kuisahau Boeing 787 itakayoleta balaa mjini.

Viwanja mbalimbali vya ndege vimeboreshwa ikiwemo kiwanja cha Mwanza, Mbeya, Bukoba na Julius. Pia kunaviwanja vipya vimejengwa na vinaendelea kujengwa maenep mbalimbali ikiwemo kile cha Chato.

Njoo kwenye Reli hapa ndio balaa lilipo Standard Gauge Railway ndio hiyo tena ikiwa ya kwanza katika nchi za Afrika mashariki na wengine wameamua kuiga mfano. Aitakuwa ajabu mtu kuishi morogoro lakini akawa anafanya kazi apa Jijini Dar es salaam. Hivi mnataka Rais afanye nini sasa, vitu ambavyo vilikua ndoto lakini sasa hivi ni halisi.

4. Ujenzi wa viwanda

Hili hata sina haja ya kulielezea maana kila mtu habari anayo

5. Vita dhidi ya Rushwa

Ili nalo sitakuwa na haja ya kulielezea naana kila mwenye akili timamu analijua. Wale ambao walikuwa wanaonekana malaika na mkono wa dola hauwezi kuwafikia habari wanayo na moto wanaona jinsi unavyowawakia kwa kujifanya mali ya umma ni ya kwao peke yao. Kwasasa mjini hapa akuna mbabe.

6. Ulinzi wa Raslimali zetu na Amani ya Nchi.

Hili nalo kila mtu ni shahidi, madini yetu kuwa watu walijifanya kama yao walichukua watakavyo na kuenda kuneemesha mataifa yao. Ambaye ana taarifa ni kitu gani kinaendelea apa anaruhusiwa kuniuliza nimpe habari.

Amani na utulivu naona kila mtu anashuhudia ni namna gani vinatamalaki. Akuna cha kuleta vyoko vyoko. Wale wote waliokuwa wakileta fujo fujo kipindi nchi hii ikionekana kama haina uongozi waijua ni nini hasa kinawapata kwa sasa. Kila nchi inautaratibu wake bana.

Nashukuru kwa leo na itaendelea…….
Hana lolote...lakini hata kama akifanya, haya yote hayawezi kuwa na maana kama raia mmoja tu akitishiwa maisha yake wachilia mbali wengi ambao tayari wamekwishakuuawa na wengine kupotea, au kuokotwa wakielea baharini au kwenye mito wakiwa wamefungwa katika viroba kama viazi!
 
Kwangu mimi mafanikio ni,watu kupigwa risasi ovyo,waandishi wa habari kunyimwa uhuru wa kufanya kazi,watu kunyimwa haki yao kukusanyika kwa mikutano ya siasa,watu kuachishwa kazi bila kufuata utaratibu unaofaa,kutekwa na watu kopotea...niiteni mburura ila sioni mafanikio mema ya huyu mtu.
 
Yule pole pole aliyesema nanukuu: KAMA UCHAGUZI UKIWA HURU NA WA HAKI BASI CCM IJIANDAE KUONDOKA MADARAKANI, mbona anaendelea kupotosha watu na kufanya siasa au yy sio mwanasiasa.
Hebu acheni UZUZU ninyi akili zenu ziko kwenye mifuko ya nyuma mkikaa mnazikalia. Ndio maana Leo POLEPOLE anawaongoza

NJAAA MBAYA SANA
Aha Yule polepole alishaakufa zamani mkuu sema
R.I.P.
 
Umevimbiwa kande na maharage aliyokupikia mke wako unakuja kuropoka hapa
 
Kwangu mimi mafanikio ni,watu kupigwa risasi ovyo,waandishi wa habari kunyimwa uhuru wa kufanya kazi,watu kunyimwa haki yao kukusanyika kwa mikutano ya siasa,watu kuachishwa kazi bila kufuata utaratibu unaofaa,kutekwa na watu kopotea...niiteni mburura ila sioni mafanikio mema ya huyu mtu.
Utaonaje mafanikio huku wewe ni kipofu
 
Subiria sasa uone ' Mangumbaru ' yakishatoka Kushiba huko Ugali watakavyokuja kutiririka na kuserereka ' Kipopoma ' tupu juu ya haya ya ukweli yote uliyoyaandika. Wanakuja sasa hivi Mkuu!
Kwa comments zako, wewe ndio Ngumbaru na Popoma no 1..
Ngoja nicheki kama kuna wengine huko mbele.
 
Mkuu hapo kwenye elimu umesema walimu wa kutosha!! Fafanua kidogo wa nyanja gani?
 
Mnyonge mnyongeni ila haki yake Mpeni.

Nimekaa hapa nikawa natafakari utendaji kazi wa Rais wetu kipenzi “The Man himself President Magufuli”

Ki ukweli kazi kaifanya katika hii miaka yake miwili na nusu kwa sasa, achana na sisi tunaolalamika sijui maisha magumu mara mtaani pesa hakuna napenda kukuhakikishia kama hautaki kufanya kazi lazima tu maisa kwako yatakuwa magumu na utaendelea kumsingizia na kumchukia Mheshimiwa Rais bure.

Hebu jamani tujaribu kuona hapa mafanikio ya Mheshimiwa Rais japo kwa uchache na wale wajuvi zaidi watajaribu kinisaidia kwa kuongeza nyama

1. Tukianza na Sekta ya Elimu

Hili hata ungekuwa kipofu ata uwezi kubishana na mimi kuwa limefanikiwa kwa kiwango cha juu, nadhani tunakumbukumbu MH.Rais aliahidi elimu bure kuanzia Elimu ya msingi mpaka kidato cha nne na amefanya, sasa watoto wetu hatusumbuani maswala ya ada wala michango huko mashuleni kitu kilichopelekea wazazi wengi kupeleka watoto wao shule na ninahakika baada ya miaka kadhaa Tanzania itakua miongoni mwa nchi zenyeidadi kubwa ya wasomi.

Ukiangalia mpaka sasa kunaongezeko kubwa la wanafunzi wanaoandikishwa kujiunga na shule ya msingi. Mfano mwaka 2015 idadi ya wanafunzi wa shule ya msingi ilikuwa ni wanafunzi milioni 8,235… na kwa sasa tunajumla ya wanafumi miliono 10 na kitu unaweza kuona ongezeko lililopo hapo. Shule za sekpondari kwa mwaka 2015 tulikuwa na wanafunzi milioni 1,804056 kwa sasa tunawanafunzi takribani milioni 2,354234 kunaongezeko ku bwa sana hapo pia.

Mbali na kuongezeka kwa wanafunzi vifaa vya kufundishia na nyezo nyingine mashuleni vimeboreshwa mfano mzuri ni madawati, tatizo la madawati sasa limepungua kwa zaidi ya asilimia 80, walimu wa kutosha .

2. Tukija katika Nyanja au sekta ya Afya

Hapa napo hakuna mtui anaeweza kubisha ni kwa kiasi gani MH.Rais kajitaidi kutimiza kile alichokiahidi na badi muda anaomwingi sana kuendelea kuboresha na kukamirisha kile alichowaahidi watanzania, kipindi cha nyuma ilikua nadra sana ukaenda hospital ukamaliza kufaniwa tiba na kuandikiwa dawa ukaipata ile dawa uliyoandikiwa katika dirisha la hiyo hospitali ya serikali, sanasana utaambiwa uende duka lililo maali flani. Kwa sasa hiyo biashara haipo.

Serikali ya Rais magufuli imejitahidi sana katika swala la upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vingine, mfano MSD imeingina mikataba na umla ya wazalishaji wa dawa 110 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo wazalishaji 10 kutoka hapahapa nyumbani. Upatikanaji wa dawa muhimu kwa sasa umepanda hadi Asilimia 85 ukilinganisha na huko nyuma ambapo upatikanaji wa dawa muhimu haukufika hata asilimia 50.

Bajeti ya dawa na vifaa tiba kwa mwaka 2017-2018 ni bilioni 269 am bayo ni kama mara kumi ya bajeti ya mwaka 2015-2016 ambapo bajeti ilikua bilioni 29 tu.

Uboreshaji wa huduma mbali mbali mfano kwa sasa tunafanya upandikizaji wa figo hapahapa nchini kipindi cha nyuma wagonjwa wenye matatizo ya figo walitakiwa kupelekwa nje ya nchi. Hadi kufikia sasa hivi serikali imefunga mashine za upandikizaji wa figo zaidi ya 140 katika hospitali mbalimbali kitu ambacho ni maendeleo makubwa sana, hii ni kwa uchache tu.

3. Uboreshaji wa njia mbalimbali za usafiri na usafirishaji.

Hapa nitaongelea mifano mikubwa miwili ambayo ni Reli na usafiri wa anga. Tukianza na usafiri wa anga, hapa kila mtu atakuwa ni shahidi kuwa shirika letu la ATCL lilikua limekufa kabisa kilichokuwa kinasubiliwa ni mazishi tu, lakini huwezi kuamini lilivyofufuka ghafla baada ya MH.Rais kukamata madaraka tumeshuhudia haraka sana Rais alinunua ndege mbili aina ya Bombardier Q-400, sasa watu wanafika Kigoma, Dodoma, Katavi n.k kwa ndege kitu ambacho zamani ilikua hamna zaidi zaidi watu walitumia videge vidogo, lakini pia mwaka huu kuna madege mengina yatashuka ili kuimarisha zaidi usafiri wa anga ndani na nje bila kuisahau Boeing 787 itakayoleta balaa mjini.

Viwanja mbalimbali vya ndege vimeboreshwa ikiwemo kiwanja cha Mwanza, Mbeya, Bukoba na Julius. Pia kunaviwanja vipya vimejengwa na vinaendelea kujengwa maenep mbalimbali ikiwemo kile cha Chato.

Njoo kwenye Reli hapa ndio balaa lilipo Standard Gauge Railway ndio hiyo tena ikiwa ya kwanza katika nchi za Afrika mashariki na wengine wameamua kuiga mfano. Aitakuwa ajabu mtu kuishi morogoro lakini akawa anafanya kazi apa Jijini Dar es salaam. Hivi mnataka Rais afanye nini sasa, vitu ambavyo vilikua ndoto lakini sasa hivi ni halisi.

4. Ujenzi wa viwanda

Hili hata sina haja ya kulielezea maana kila mtu habari anayo

5. Vita dhidi ya Rushwa

Ili nalo sitakuwa na haja ya kulielezea naana kila mwenye akili timamu analijua. Wale ambao walikuwa wanaonekana malaika na mkono wa dola hauwezi kuwafikia habari wanayo na moto wanaona jinsi unavyowawakia kwa kujifanya mali ya umma ni ya kwao peke yao. Kwasasa mjini hapa akuna mbabe.

6. Ulinzi wa Raslimali zetu na Amani ya Nchi.

Hili nalo kila mtu ni shahidi, madini yetu kuwa watu walijifanya kama yao walichukua watakavyo na kuenda kuneemesha mataifa yao. Ambaye ana taarifa ni kitu gani kinaendelea apa anaruhusiwa kuniuliza nimpe habari.

Amani na utulivu naona kila mtu anashuhudia ni namna gani vinatamalaki. Akuna cha kuleta vyoko vyoko. Wale wote waliokuwa wakileta fujo fujo kipindi nchi hii ikionekana kama haina uongozi waijua ni nini hasa kinawapata kwa sasa. Kila nchi inautaratibu wake bana.

Nashukuru kwa leo na itaendelea…….

Kaka kwenye elimu kampunguzia mzazi mzigo wa ada ila kiukweli elimu inadidimia...hili ni bomu baya sana. Hebu tujiulize ubora wa elimu ktk mazingira magumu ya ufundishaji na vitendea kazi inakuja je?

Rais ana nia nzuri sana na yafaa kupongezwa, ila ktk hili bado hatujajipanga sawa, hata Lowassa naye hii sera ingemshinda pia
 
Mkuu hapo kwenye elimu umesema walimu wa kutosha!! Fafanua kidogo wa nyanja gani?
Nyanja zote mkuu sijajua umemaanisha nini, ila ni sayansi na sanaa, sekondari na shule za misingi kwa hiyo ni kote kumekamilika
 
Asante kwa taarifa. Niko huku kijijini nafikiri hizi takwimu hazituhusu.
 
Almost point zote hizi ni za kipumbavu
Kwanza hauna uwakika na unachosema
Pili hajaua democrasia ila kauwa njia ya wanasiasa kudanganya na kucheza na vichwa vya wa2

Na kingine huna suggestion yoyote huijuayo zaidi ya kutapatapa, ko ulitaka hella ya serikali itumbuliwe ovyo na viongozi ili hella iwe nyingi kumbi za starehe???,
Kwani yeye anacheza na viwiliwili vya watu?
Makinikia iko wapi?
Mzee muhuni yule.
Zaidi Ajielewi.
 
Subiria sasa uone ' Mangumbaru ' yakishatoka Kushiba huko Ugali watakavyokuja kutiririka na kuserereka ' Kipopoma ' tupu juu ya haya ya ukweli yote uliyoyaandika. Wanakuja sasa hivi Mkuu!
UPO SAHIHI MKUU
Hiyo amani unayoisemea wewe ni IPI?
Wa Kwanza Huyu
unatetea ujinga na ww iyo elimu yenyewe ndo ile kama mtu amefeli labda kidato cha pili anapitishwa ivo ivo ili akapate zero form four

huwezi mwacha mtoto aliepata four ya 30 form 2 et akafanye CSEE form four utegemee afaulu hizo ni ndoto za alinacha
Mwingine huyu
 
Mwingine Huyu hapa
 
Inaonekana mwandishi wa makala hii ndio watu wanaopiga hela chini ya utawala huu wa sasa. Nothing more.
 
1. Kaua watu watu wengi
2. Kaua demokrasia
3. Amevunja umoja na mshikamano wetu watanzania
4. Kaua uchumi wa nchi
5. Kaondoa amani
6.Kashusha taswira ya watanzania tuliyokuwa nayo nje ya nchi
7. Kaua elimu ambayo tayari ilikuwa ICU

Amefanikiwa kuharibu mengi tena kwa kipindi kifupi
8.Kuweka Nidhamu ya woga kwa watendaji na mawaziri
9. Vitisho na kuteka teka ovyo ovyo
 
Back
Top Bottom