Mimi namwona Rais Magufuli kama ni Rais ambaye mpaka sasa AMEOKOA na KUPONYA watu wengi sana ukilinganisha na ilivyokuwa kabla yake. Mungu ambariki sana Rais wangu.
AMEOKOA na KUPONYA watu wengi kwa:-
(1)Kuongeza Bajeti ya madawa zaidi ya mara 7 ya Bajeti iliyokuwa ikipangwa miaka iliyopita.
(2)Kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma wakiwemo WAUGUZI na MADAKTARI. Hii imeepusha vifo ambavyo vingesababishwa na uzembe wa watumishi wa hospitali.
(3)Kusimamia kwa dhati utendaji kazi unaozingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi. mfano, madereva waliokuwa wanaendesha magari ya abiria kwa uzembe, sasa wanaendesha kwa uadilifu, hivyo AJALI ambazo zingetokea kwa uzembe zimepungua sana.
(4)Haki na uwajibikaji katika OFISI za umma vinatendeka, hivyo manung'uniko na STRESS kwa watu wengi vimepungua sana.
Mathalani, mimi nina ndugu yangu ambaye alifiwa na mme wake ambaye alikuwa ni Mwanajeshi(JWTZ). Amefuatilia mirathi karibu miaka 3 bila mafanikio. Lakini alipoingia tu madarakani Mh.Magufuli, alipata mirathi yake si zaidi ya WIKI mbili tena bila usumbufu wowote.
Kwa hiyo, Rais Magufuli anastahili pongezi za dhati kwa kazi nzuri.
Nijuavyo mimi ni kwamba, hata watu wamnenee mabaya namna gani, lakini kwa Mungu hakuna Siasa. Mungu anampenda mtu anayesaidia watu.
Kama Rais, kuwapa watu UHURU wa kuongea na kufanya watakavyo katika nchi ili tu wasikubugudhi lakini ukasahau kutenda yaliyo mema kama haya yaliyopo sasa kwa kuogopa kusemwa vibaya na watu, hakika utakuwa umefanya kosa kubwa zaidi. TENDA MEMA KATIKA NCHI, MUNGU NDIYE ATAKAYEKUHESABILIA HAKI, WALA SI MWANADAMU.
Mungu ambariki Rais wetu Magufuli. Amina.
 
Mbona lile jinga bashitte linalofanya kazi kwa mazoea kutumia jina la mtangazaji wa redio hivi hamulioni lipolipo tuuu na kutafuta kiki.
Mnazani ataendelea mpaka lini?
Mmeshindwa kumng'oa sasa asubiri muda ukifika atajua bashitte ni nani
Mkuu michago ya shule ipo palepale kilichobadilika ni kuwa hakusanyi mwalimu[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Wewe binafsi amekusaidia mirathi!!! Na ajira kwa vijana wetu vipi? Nani kakudanganya stress hamna wakati watu madaraja hawapandi? Na wakipanda ni kimitaa
 
Magufuli akuna ancho fanya zaidi ya kulinufaisha tumbo lake
 
Sanasana naliona moja zuri, la ujenzi wa reli! Miradi mingine yote aliikuta inaendelea, ilibuniwa na Kikwete, Yeye anaimalizia tu. Miradi kama ya flyovers, barabara na mingine ameikuta, anaimalizia!
Kikwete aliianzisha bila ya ghiliba za kuwafukuza maelfu ya watu kazi bila ya malipo kwa kisingizio cha vyeti feki ili mishahara na viinua mgongo avitumie kwa miradi ya kutafuta kiki! Mradi kama wa ununuzi wa ndege sita hauna manufaa ya moja kwa moja kwa mlalahoi!
 
1. Kuwafuta watu elfu 12. Ajira
2.kufuta ajira za waalimu toka mwaka 2015...kuingia kwenye system.
3.ajira za madaktari kuingia kwenye system
4.Kukataza mikutano ya hadhara kwa vyama pinzani.
5.kunyima haki ya kukueleza na kuikosoa serikarli
6.kuvunja katib ya ccm kwa kutowapa haki kutendeka kuchagua wabunge na madiwani wanaowapend kuwawakilisha katika nyanja hizo. Katika kata na majimbo pinzani ambayo walitoka vyama vingine
7. Kutopata taarifa za mwananchi wanaopata madhara na matanga ya kutekwa na kuuwa kuwa walipatiwa matatizo hayo na nani
 
yote aliyofanya pombe matokeo yake ni
NJAA
UTEKAJI
MGAO WA UMEME
UVUNJWAJI WA NYUMBA
KUONGEZEKA KWA MIKOPO
 
Kumpa nguvu zote na ulinzi mkubwa pamoja na kumpa mamlaka naibu waziri ambaye anamamlaka nani awe na nani asiwe
 
Kumpa nguvu zote na ulinzi mkubwa pamoja na kumpa mamlaka naibu raisi ambaye anamamlaka nani awe na nani
 
Unafiki wa Wanywa maji ya bendera ya Lumbumba haujawahi waacha salama. Leo mnadhubutu kumkashifu mtukufu wenu wajana? Kisa vitayajana ilipita mnapigania ugali wa Leo. Shame on you guys.
Viwanda tumeona TIRION 1.5
 
Kuwa mkweli, serikali haina shamba.
 
Tatizo la nchi hii ni maadui watatu ujinga, umaskini na maradhi..... Elimu inapanda, au inashuka? Huduma za afya zimeboreka? Umaskini unapungua au kuna viashiria vya kuupunguza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…