Mimi namwona Rais Magufuli kama ni Rais ambaye mpaka sasa AMEOKOA na KUPONYA watu wengi sana ukilinganisha na ilivyokuwa kabla yake. Mungu ambariki sana Rais wangu.
AMEOKOA na KUPONYA watu wengi kwa:-
(1)Kuongeza Bajeti ya madawa zaidi ya mara 7 ya Bajeti iliyokuwa ikipangwa miaka iliyopita.
(2)Kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma wakiwemo WAUGUZI na MADAKTARI. Hii imeepusha vifo ambavyo vingesababishwa na uzembe wa watumishi wa hospitali.
(3)Kusimamia kwa dhati utendaji kazi unaozingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi. mfano, madereva waliokuwa wanaendesha magari ya abiria kwa uzembe, sasa wanaendesha kwa uadilifu, hivyo AJALI ambazo zingetokea kwa uzembe zimepungua sana.
(4)Haki na uwajibikaji katika OFISI za umma vinatendeka, hivyo manung'uniko na STRESS kwa watu wengi vimepungua sana.
Mathalani, mimi nina ndugu yangu ambaye alifiwa na mme wake ambaye alikuwa ni Mwanajeshi(JWTZ). Amefuatilia mirathi karibu miaka 3 bila mafanikio. Lakini alipoingia tu madarakani Mh.Magufuli, alipata mirathi yake si zaidi ya WIKI mbili tena bila usumbufu wowote.
Kwa hiyo, Rais Magufuli anastahili pongezi za dhati kwa kazi nzuri.
Nijuavyo mimi ni kwamba, hata watu wamnenee mabaya namna gani, lakini kwa Mungu hakuna Siasa. Mungu anampenda mtu anayesaidia watu.
Kama Rais, kuwapa watu UHURU wa kuongea na kufanya watakavyo katika nchi ili tu wasikubugudhi lakini ukasahau kutenda yaliyo mema kama haya yaliyopo sasa kwa kuogopa kusemwa vibaya na watu, hakika utakuwa umefanya kosa kubwa zaidi. TENDA MEMA KATIKA NCHI, MUNGU NDIYE ATAKAYEKUHESABILIA HAKI, WALA SI MWANADAMU.
Mungu ambariki Rais wetu Magufuli. Amina.