Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2021
Amefanya mambo mazuri kiasi na hatofautiani sana na jk ktk kuleta maendeleo.. Shida ni ustawi wa wananchi yupo nyuma sana
 
Tuacheni mihemko tumsifu pale alipopatia maana nchi ilikuwa imeoza.
Fikiri mkuu hajaenda hata dubai kuosha macho kwa Uzalendo wake.
Hajaenda kwa uwoga wake tu, Mimi nashaanga anajisifu ukusanyaji wa kodi umeongezeka, watumishi hewa ameondoa amezuia madili yote lkn bado serikali haina hela. Kuna haja gani ya hayo aliyofanya wakati hatuon faida ya pesa aliyo iokoa? Akae akijua ana wakati mgumu sana maana wanamfurahia wanazidi kupungua kila siku
 
10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kaweza kujenga

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2
Nyingine 3 ziko mbioni kuja.
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
Kuna undergoing projects ambazo zipo tangu yeye hana tamaa ya kubahatika kupata huo urais kama hizo upanuzi wa airports na flyover.
Hizo hostel mimi siweki hesabu hesabu kama kina faida na tanzania kwa ujumla hata kama ina faida na tanzania kwa ujumla basi its a small issue sio ya kujisifia.
Rushwa na ufusadi tusidanganyane ipo kama kawaida sema ufisadi upo kwa wachache tena kwa wale ambao yeye mwenyewe anawalinda kama kina bashite.
na hiyo upanuzi wa barabara ya moroco is a small issue wala usiseme ni mafanikio ni aibu kusema hivyo.
Na nidhamu makazini labda ya uoga na maigizo nadhani tumeona kule bandarini yale maigizo. ethically hatuoni still zero.
Labda hizo ndege alizonunua japokuwa kuna possibility ya kufeli kwasababu ya ukurupukaji
The only thing ambao nimependezewa na kusema la ukweli hii yote imetokana na sababau hajui English ila nimefurahi kwasababu atapata kukipanua hii lugha yetu ya kiswahili huko nje. Japokuwa hasafiri kwa uoga wake wa kuadhirika.
Nawasilisha
[HASHTAG]#MakondaOut[/HASHTAG]
 
Miradi mingi inayokamilika na kuzinduliwa ama kuanza hivi sasa michakato yake ilifanyika awamu iliyopita,hivyo yeye kafanya kuzindua tu,so msije mkamsifia kwa mambo yasioyokuwa yake
 
Bei ya sembe imetoka tshs 600 hadi tshs 1500 Leo.
 
10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kaweza kujenga

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2
Nyingine 3 ziko mbioni kuja.
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
Ujenzi wa Airport Chato
 
Utakula jeuri yako.

Unadhani wewe upo salama kuliko alivyokua Nape? Acha kauli za kejeli

Rais anasema kuna watu wanashinikiza habari zao zitoke... anasahau aliyeenda na bunduki studio

Anasema hapangiwi wa kumchagua kwakuwa alichukua fomu za Urais peke yake alijiamini....mbona anawaelekeza wamiliki wa magazeti nini cha kuandika ilhali wao walikuwepo kwenye tasnia hiyo miaka zaidi ya 20 kabla ya Urais wake na hiyo genocide haikutokea?

Kama hajui hata wakopaji wa WB ni kina nani anataja mpaka Marekani na Ulaya anajua nini kuhusu genocide Rwanda? Km anabisha aruhusu mjadala huru wa nini kiini cha mauaji ya kimbari Rwanda
 
Maendeleo ya vitu hata jakaya ameyafanya Magufuli cha maana alichofanya ni kukomesha Rushwa na kuleta nidhamu
Yaani mtu anatetea walioghushi vyeti halafu unasema anapambana na rushwa? Hiyo nidhamu ya Utumishi Wa umma iko wapi?
 
Kama sote sisi sasa tuelekeze mawazo yetu katika swala la vyeti vya Bashite then basi tumepoteza lengo. Mkuu wa mkoa siyo mtumishi hicho ni cheo cha kisiasa sawa na waxiri na wabunge. Mawaziri, wakuu wa mikoa/wilaya wapo hivyo kwa ridhaa ya Rais. Ana madaraka ya kuteua na kutimua. Wote hao ifikapo 2020 watakuwa hawana kazi. Sifa ya kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika kiswahili, mawaziri hutokana na wabunge. Yamesemwa mengi kuhusu Bashite nadhani busara ya kawaida ituelekeze tusubiri yule aliyemuweka achukue hatua. Kinyume cha hapo tuwe wapole hadi 2020 wananchi waamue kupitia sanduku la kura
 
Nadhani mkuu atakumbukwa kwa majivuno, kujisifu, kudharau waliyoyafanya wengine, ubaguzi, ukabila, ukanda, udini, kupenda kiki, kukubali ubashite kwa ndugu yake bashite
Kuondoa ufisadi kwa wengine ila kwa bashite unafaa.
 
Bira kusahahu Maji na barabara. Plus umeme vijijini.
 
Kurudisha pesa za TAASISI zetu Benki kuu zile fixed account za TAASISI walikuwa wanakula vigogo
Kupambana na dawa za kulevya
Korosho bei kupanda maradufu
Kuondoa urasimu ofis za umma
Alafu aje mtu aseme magufuli sio rais mzuri??

Magufuli oyeee


Oyeeeeeeeee
 
Napata ukakasi wa kufikiri kuhusu mazuri yake kwani to be honestry sioni mazuri na wingi wa wanaochangia wanaonyesha mapungufu sababu ndio yako bayana kama nguzo za umeme sasa mleta mada inabidi upokee kila aina ya mchango.
 
Back
Top Bottom