Tuendelee kutafakari!


Is that you Reverend? Long time no see , no hear!

Ooh, Thank God Rev. is back!
And as for "Kueleweka"? Let's see how this works out.
Yes, Tanzania will never be the same again after this. You can bet on that and take it to the bank!

Whatever happened to the Kifimbo Chezas/MamaNtilies/MdosiMzalendos. Everyone needs to be back.
The MzeeMwanakijijis are here, although hardly recognizable. Days have taken their toll you see. Mkangaras absconded. The once a while Kichuguus are here too.

The Great Nguruvis, Mag3s, JokaKuus, et al; are here, fighting in the trenches like hell like everyone else.
And of course the new squad and the crew of JF keep the fire burning.

Tanzania will be Great, with or without the Magufulis. Now, you tell me about "Kueleweka".
 
Muda utaongea! Tusihukumu kwa sasa.
 
Ni mengi ya kutafakarisha yametokea tangu Magufuli awe Rais

Kuingia tu:
1. Akateka Bunge, Tulia nusra awe spika, lakini haikuwa lazima kwani Spika aliekuwepo ali-oblige, na mara nyingi alikuwa India.

2. Akateka Katiba, na kuanza kutumia sheria zake mwenyewe. Akapiga marufuku mikutano ya kisiasa.

3. Akakichukua Chama na kukifanya chake. Watu wakadhani CCM ya Kikwete iliyooza sasa itanyooka. Wengi wanadhani kimakosa kuwa CCM ya Magufuli imenyooka.

4. Kufuata taratibu za kiutendaji sio muhimu tena, mradi wafanyakazi wamewekwa kwenye mstari wake kwa nguvu zake binafsi. Akidondoka leo hii, keshokutwa ukienda ofisini usishangae kukuta yale yale aliyoyaacha Kikwete.

5. Zamani niliamini, mtu akisoma kiasi cha kutosha, na isiwe hata ngazi ya PhD, atakuwa alishafahamu kuwa wazungu na watu wa mataifa mbalimbali wasiokuwa weusi nao ni watu wa kawaida tu kama weusi wa Tanzania. Kwa hiyo lisingekuwa jambo la kustaajabisha sana kuona mzungu anannyenyekea mbele ya mweusi, hasa Kiongozi. Hapa namkumbuka yule Prof. wa Makinikia, na ishara zilizotawala wakati huo.

6. Akachukua nyenzo zote za serikali ili zimuwezeshe kufanya anayoyataka yeye

Ni mengi ya kutafakarisha yametokea

1. Uhusiano wa kimataifa kwa taifa kama Tanzania ni muhimu sana na Kiongozi hawezi kujitoa na kutegemea wasaidizi wamfanyie kila kitu.

2.Wawekezaji wa nje ni wa mashaka. Hata huu wa ndani umekuwa mgumu, kwa sababu za kutofuata taratibu tu zilizotakiwa kufuatwa katika marekebisho yaliyotakiwa kufanywa katika sheria zetu ili kulinda haki yetu.
Kazi za mabavu bila ya fikara matokeo yake huwa giza.

3. Tunajenga uchumi wa viwanda. Mikakati iko wapi? Ni jambo la kutafakarisha. Na wakati huo huo hatujui kwa nini viwanda alivyojenga Mwalimu vilikufa!

tunajifunza mapya na kukumbuka mengi

Tunajifunza kuwa:
1. Kumbe tuliyokuwa tunayaona kwa wenzetu kwetu pia yanawezekana. Kiongozi kuhodhi madaraka yote, na neno lake ndilo sheria wakati wowote. Ni kwamba waTanzania hatuna tofauti yoyote na wenzetu. Kuna wakati tulidhani wananchi wetu wamekuwa na ufahamu mzuri, na kwamba hawawezi kupokwa haki zao. Uamini huu ulikuwa potofu kabisa.

2. Kuwa kiongozi anaweza kusema uongo na watu wakaendelea kushangilia na kusifu. Hilo ndio taifa letu.

3. Tumejifunza kuwa kwa nguvu, kiongozi anaweza kutumia utashi wake na "kulinyoosha taifa" bila ya kutengeneza mfumo unaoweza kuendeleza huko "kunnyoka" anakokutaka. Matokeo ya hili ni kama kule kunyooka kwa CCM nilikokusema hapo juu.

4. Tunakumbuka mengi. Lakini hasa Umoja wa Taifa letu unatia shaka sana. Sasa hadi tumeamua kujitoa ufahamu waTanzania kwa kulinganisha wasioweza kulingana hata kwa centimeter moja.

Kumshukuru Mungu? Ni sawa kabisa, na hasa Magufuli akiamua kutuonea huruma na kung'atuka akimaliza ngwe yake. Ni huruma yake tu, vinginevyo tutaendelea kumshukuru Mungu kwa Tanzania yetu hii.
 
Kwa hyo wewe una furahia mungu kutupa kichaa?
,au na wewe ni kichaa
 
Unamshukuuru MTU anayeonea watu na kuumiza familia !!!
 
hivi kila kitu kinaletwa na Mungu?

tuendelee kutafakari.
 
Mapungufu kama binadamu yanaingiaje wakati Urais ni taasisi? Maamuzi yanafanywa kama taasisi.
 
Asante Mkuu Joka..

Kwa mara ya kwanza leo nimeona mtu anamshukuru Mungu kwa kutupa MATATIZO.
 
Naongezea kuwa ana Hasira na mafisadi na wapiga deal anatamani wenye hela azipunguze ziende kwa wasio na hela ili tuwe sawa.KUSADIKIKA.
 
Mchungaji kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…