Anase
Anatoa siku 7 soko la madini lijengwe, soko gani la maana litajengwa kwa siku 7, hata soko la kuuza vitunguu linahitaji muda mrefu. Angalia wizara hazina mahali pa kukaa Dodoma zipo kwenye vibanda vya bati na nyingine zimepangisha UDOM na kwingineko. Yote haya ni kwasababu ya matamko ya barabani. Huo unaitwa ‘mji wa serikali ‘ Dodoma ni kichekesho, mji wa kudumu wa serikali unajengwa kwa dharura? Ndio maana mji wetu mkuu utabaki kuwa hovyo kwani mifumo ya kudumu haipo kila kitu ni cha muda mfupi. Tujifunze Nigeria walivyojenga Abuja kwa ustadi mkubwa kabla ya kuhama kutoka Lagos.
 

ili nimuone wa maana, aipitishe katiba mpya iliyoandaliwa awamu iliyopita...vinginevyo sitamuelewa...
 
Ninakushanga kwa kuwa muumini wa kila linaloandikwa kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii. Pole sana kwa kuishi katija dhana potofu
 

🤣[emoji119]
 
Kwa kipindi bila unafiki huendi kokote, sifia upate kitu, jipendekeze upate kitu, kuwa mbali ukose kila kitu, hii ndio tanzania ya sasa !!duh maisha haya naogopa hata kusema
Nafikiri wewe ndiye mnafiki katafute nchi ya kuishi, Tanzania imekushinda kipanta.
 
Tatizo sio kufanya anayoyafanya, yaani ni kama serikali haijiamini na inakaririsha wananchi tuiamini yenyewe ndio imefanya makubwa zaidi
Serikali haijiamini hahahaha! Nipe tafsiri ya Serikali kujiamini, Nina kengeza hapa. M16_kwaoz
 
Mifumo wanayotaka watu ni ya ulaji si maendeleo ya nchi, wanaotakiwa kubadilika ni watu kuwa na fikra chanya kuelekea maendeleo, ndiyo sababu awamu ya tano inafanya yale inayokusudia bila kuangalia nani anayekuja baadaye na atafanya nini. Kwa sababu haitasaidia kuweka mifumo ambayo itadumu kwa miaka kumi akija Rais mwingine analeta mipango yake kana kwamba hapakuwa na mipango endelevu.
Dr. Magufuli kafufua Air Tanzania, kajenga standard gauge, kajenga steglers gouge, kajenga barabara za mikoa zote kusogeza maendeleo kwa wananchi, atakuja Rais mwingine ataacha ATC ife, treni mwendo kasi ife, atarudisha makao makuu Dar, hiyo ndiyo bongo kaka, Mwalimu Nyerere alijenga viwanda vingi kushinda hata Kenya, kaja Mwinyi akauza viwanda akishirikiana na awamu ya tatu, awamu ya nne ikawa kwenye madini na gesi mikataba tata nchi ikakamuliwa kisawasawa, hapa tunapiga story hatujapata watu watimilifu wenye uzalendo uliotukuka kuongoza nchi yetu, Rais wetu anajaribu kutuonesha njia, lakini anakutana na vipingamizi vingi, anajaribu kuunda safu ya miaka 40 ijayo kwa kuteua vijana katika uongozi wake ili wajifunze mengi kutoka kwake kuwa uongozi si lelemama lazima mtu kukomaa na kusimamia kwa nguvu zote kile unachokiamini bila kutetereka, kuweka nidhamu ya watendaji wake nk. Mambo mengi ni ya kujitolea zaidi kwa Rais kutekeleza majukumu yake kuliko wajibu alio nao. Watanzania tutambue nchi yetu inataka wananchi wake wasaidiane na Serikali kujiletea maendeleo, badala ya kukejeli viongozi kana kwamba hawatekelezi majukumu yao.
 
Kuchukua maamuz magumu ili nchi isonge mbele inataka Busara ya Hali ya Juu
 
Hongera Rais kwa kazi nzuri unayoifanya,
huku kwetu tunakuona kama Musa wa Tanzania uliyekuja kuwaokoa Wa Tanzania.

Najaribu kukufatilia sana uongozi wako,
nilichogundua kutoka ni uongozi wako ambao umetukuka sana tena sana.

Najua unapambana sana na agents wa mabepari wakizungu.

Wanakuzuria mambo mengi sana kwa kujinasibu,eti wanasimamia demokrasia...
Raisi Magufuli,,hakika wewe umeletwa na
Mungu.

KWA MUNGU TUNAKUOMBEA,,NA UTASHINDA KWA ASILIMIA 90...2020..
WEWE NDIO UTAVUNJA REKODI ZOTE


MUNGU IBARIKI TANZANIA.

ADUI ZETU WAPISHE MBALI
AMINA...
 
Mi nampongeza sana mh. Magufuli kwa kujenga miundombino ya kisasa kama vile reli, barabara na kununua ndenge zaidi ya 5 mpaka sasa. Ila sasa nashangaa mno kwa kushindwa kuboresha sekta ambazo zinawagusa wananchi moja kwa moja. Sekta hizo ni kama kilimo, ufugaji na uvuvi, elimu na afya. Ni dhahiri kuwa huwezi kupambana na mambo makubwa huku madogo yamekushinda.

Nianze na kilimo, kwenye kilimo ameshindwa kuweka uhakika wa soko kwa mazao ya mkulima, pia ameshindwa kupeleka pesa za kutosha katika sekta hii.

Kwenye elimu napo bado mambo ni magumu mno watoto bado wana chini, mishahara ni midogo kwa walimu, bado kuna uhaba wa walimu ktk madarasa ya awali na shule ya msingi. Madarasa hayatoshi na matatizo mengine mengi.

Ushauri ni kuwa anza kuboresha elimu, kilimo, na afya ili hata tukinunua ndege hizo pesa tutakazo pata kwenye ndege zikajenge miradi mingine sasa. Siyo unanua ndege huku watu wanaugua kipindupindu kwa kunywa na maji machafu.
 
Wandugu habari za muda huu.

Kwanza kabisa Nikiri wazi kitendo alichokifanya raisi Magufuli leo hii ikulu ni zaidi ya uzalendo.

Kitendo cha kudhamini na kujali kazi za wabunifu wetu ambao wamekuwa siku zote wakiteseka na kukosa support kutoka serikalini na hata wengine kuishia kupewa vitisho, kubezwa, na hata kukamatwa kutokana tu bunifu zao wazifanyazo kwa nia njema kabisa ya kuisaidia jamii inayowazunguks kwa visingizio kibao tu kama vike viwango vyao vidogo vya elimu walivyonavyo.

Hili tukio la leo limenikumbusha kuna wakati niliona katika stesheni moja hivi jamaa kwa kutumia kemikali flani flani alizozichanganya aliweza kuweza kuzalisha umeme wa kutosha ambao ulimuwezesha kuchomelea vyuma(welding).

Sio siri nilistaajabishwa sana na ubunifu wake mpaka nikafikia kuapa LAITI NINGELIKUWA RAISI WA NCHI HII kwanza kabisa ningemfanya mbunifu huyu ajulikane ndani na nje ya nchi, lakini pia kumsaidia zaidi ili aendeleze ubunifu na kazi zake.

Pili, Mh raisi leo hii ametukumbusha maana halisi ya Elimu. Nimefurahi sana alipota 'definition' sahihi kabisa ambayo naamini itasaidia kuwakumbusha vijana wengi wa kitanzania wanaojiita 'wasomi'.


Naomba niishie hapa, ila mwisho kabisa nilitamani san raisi leo pale ikulu angewatumbua wale watu wote wa tanesco na kuteua wengine ili iwe fundisho maana kusema ukweli wale wasomi (mainginia na wataalam mbali mbali wa tanesco) wametuaibisha sana wasomi wote wa vyuo vikuu nchini wenye fani mbali mbali , na hasa wa sayansi, including Mr. President mwenyewe.

Niishie hapa kwa leo.
 
Shida ya one-man show. Yaani yeye anahusika na barabara za huko ndani ndani kwa Mkoyoyo, mpaka kwenye koro-show na mbaazi za mashangazi wa Majaliwa na Nape. Ndiyo maana huwa anajifananisha na malaika. Pombe's failure was inevitable, the wise saw it coming. Sasa sijui waimba ngonjera wake bado mna pumzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…