Anase
Anatoa siku 7 soko la madini lijengwe, soko gani la maana litajengwa kwa siku 7, hata soko la kuuza vitunguu linahitaji muda mrefu. Angalia wizara hazina mahali pa kukaa Dodoma zipo kwenye vibanda vya bati na nyingine zimepangisha UDOM na kwingineko. Yote haya ni kwasababu ya matamko ya barabani. Huo unaitwa ‘mji wa serikali ‘ Dodoma ni kichekesho, mji wa kudumu wa serikali unajengwa kwa dharura? Ndio maana mji wetu mkuu utabaki kuwa hovyo kwani mifumo ya kudumu haipo kila kitu ni cha muda mfupi. Tujifunze Nigeria walivyojenga Abuja kwa ustadi mkubwa kabla ya kuhama kutoka Lagos.Kwamba yeye hajui mifumo na mifumo haipo! Ukweli ni kwamba mifumo ipo, sheria zipo, nk.
Kwa mfano kuna viongozi wa Serikali za Kijiji, Serikali za Mitaa, Madiwani, Wabunge na hatimaye Mawaziri. Na kila kiongozi ana majukumu, madaraka na mamlaka yake.
Kilicho wazi ni viongozi "kula bata" na kulewa madaraka.