Waungwana mimi naona Rais John pombe magufuli apite tu uchaguzi ujao hakuna namna na asipopita mi sikubali ntaandama peke yangu Wala sitataka sapoti ya mtu.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Mheshimiwa Rais ameanzisha jitihada kubwa za kulikomboa taifa letu kiuchumi kwani wote tunaona mabadiliko kimaendeleo, tukilinganisha na wakati uliopita. Amekuwa akitumia muda wake mwingi katika harakati za kubuni namna gani atalikomboa taifa letu na wananchi wake kutoka katika lindi la umasikini.

Tumemsikia mara kadhaa akisema kuwa wakati mwingine analazimika kulala chumbani na mafaili ili ayafanyie kazi hata usiku wa manane. Hii yote inaonyesha jinsi gani rais wetu alivyo na uchungu na nchi yetu. Kuna wakati aliwahi kusema kuwa kazi hii ( ya u-rais) ni ngumu sana, lakini kwa bahati mbaya baadhi ya watu hawakumuelewa na wakatafasiri vibaya (wengine kwa makusudi), wanafikiri mtu akiwa rais, kazi yake ni kutoa amri tu, kumbe sio.

Kuna mambo mengi magumu (complex issues) unatakiwa uzifikirie kwa kina na hatimaye uzipatie suluhisho, hapo ndipo ugumu unapoanzia. Kuna masuala ya afya, maji, miundombinu n.k., yote haya kwa ujumla wake yatazame kitaifa uone changamoto zake; lakini yote haya Mheshimiwa rais ameyatekeleza kwa asilimia kubwa na bado anaendelea kutekeleza mengine.

Ni masikitiko makubwa kuona kuwa pamoja na jitihada hizi za rais wetu mpendwa kulikwamua taifa letu, kuna baadhi ya watu wameanzisha jitihada za kumkwamisha au kumkatisha tamaa ili watimize matamanio yao. Nasema matamanio yao kwa kuwa harakati zao hizo za kumkwamisha rais hazina maslahi kwa taifa, bali ni kwa maslahi yao.

Inasikitisha zaidi tunapoona kuwa watu hao ni watumishi au wamewahi kuwa watumishi katika ngazi mbalimbali. Tulitegemea watu hao wangekuwa mfano bora (role model) wa kuigwa matendo yao na wananchi wa ngazi zote kwa mustakabali wa ustawi wa taifa letu. Badala yake, watu hawa wamegeuka na kuwa kikwazo kwa rais wetu mpendwa.


Mwanaharakati mmoja aliling’amua hili na kutufahamisha wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Baadhi ya watu walimuona ni mzushi, kumbe ni ukweli mtupu na leo hii mambo hayo yamejidhihirisha. Inasikitisha sana.

Lakini wananchi tujiulize swali moja; wakati tunamchagua kiongozi wetu (rais wetu), matamanio yetu yalikuwa ni nini? Wengi watasema tulitaka atuletee maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Tumeona mheshimiwa rais amekuwa na maono makubwa sana juu ya uchumi wa taifa letu.

Leo tunashuhudia shirika la ndege (ambalo kwa kweli lilikuwa limekufa) likifufuliwa kwa kununua ndege nyingi (tena kwa fedha taslimu); Dreamliner, Airbus na bombardier huku ndege zingine tatu (za ukubwa niliotaja) zikiagizwa. Nani angeweza kutekeleza jambo hili?

Tumeshuhudia barabara nyingi zikijengwa na zingine kupanuliwa (kama hii ya Morogoro road, Kimara-Chalinze), angalia barabara za juu (fly overs) kama pale Tazara, Gerezani, hii inayojengwa Ubungo na kule Salender. Hii yote ni kuhakikisha kwamba tatizo la foleni za magari (traffic jam) katika jiji la Dar es Salaam linabakia kuwa historia.

Hata sisi huku mitaani barabara za mitaa ni nzuri; bodaboda, magari madogo na hata makubwa yanapita bila shida yoyote. Juzi nimesafiri kwa dakika 7 umbali ambao hapo awali tulikuwa tunasafiri kwa dakika 30, na hii ni kutokana na barabara kuwa nzuri. Je, haya sio maendeleo?

Usafiri wa majini ni wa uhakika, kuanzia vivuko hadi meli katika bahari na maziwa hapa nchini. Hivi juzi tu Rais alipotoka mapumzikoni Chato alienda Mwanza (akipitia Biharamulo, Katoro, Geita na Sengerema), akiwa huko, pamoja na mambo mengine, alienda kukagua ujenzi wa meli mpya.

Tuliona jinsi alivyosisitiza kukamilika kwa meli hiyo ikiwa ni pamoja na kuziagiza mamlaka zinazohusika kutoa vibali na kusaini nyaraka za kusafirisha malighafi zinazotumika kutengeneza meli zisicheleweshe. Mkandarasi alimuahidi kuwa meli hiyo itakamilika mwezi 3 mwakani. Kumbe tuona rais wetu sio wa kukaa ofisini tu, anakwenda mwenyewe kuangalia utekelezaji. Rais wetu anapiga kazi usipime!

Mheshimiwa rais wetu anatujengea reli ya kisasa (standard gauge), hii ni ya kasi kubwa ili watu (na mizigo) waweze kutekeleza majukumu yao ya kibiashara kwa haraka iwezekanavyo. Badala ya kuchelewa njiani kwa siku mbili au tatu, sasa itakuwa safari ya masaa sita tu (kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza).

Juzi tumeona garimoshi ya ya kutoka Tanga kuelelekea Moshi imefufuliwa baada ya kutotoa huduma kwa muda mrefu. Hii itarahisisha kusafirisha mizigo kutoka bandari ya Tanga kuelelekea maeneo mengine ya Kaskazini. Na juzi Mheshimiwa rais akiwa njiani kuelekea Rufiji, alitoa maagizo kwa uongozi wa Tazara kuhusu ufanisi wa reli hiyo.

Hii yote ni kwamba Mheshimiwa rais anahakikisha sekta ya usafirishaji inaimarika.Tujiulize, haya sio maendeleo? Hakuna nchi(duniani) iliyoendelea bila kuipa kipaumbele sekta ya usafirishaji kwani ndio kichocheo kikubwa cha uchumi.

Mheshimiwa rais ametujengea vituo vya afya vingi sambamba na ugawaji wa madawa kwenye vituo hivyo. Wananchi angalau sasa hivi tukienda kutibiwa tuna uhakika wa kupata dawa. Hivi juzi tu kimefunguliwa kituo kipya cha afya Kimara na wananchi wanafurahia kupata huduma ya matibabu.

Mheshimiwa rais ameweza kufanikisha mpango wa elimu bure, kutoka elimu ya awali mpaka ya kidato cha nne. Tujiulize, ni nchi ngapi zimeweza kufanikisha hili? Na kwa hili tumeshuhudia watoto wengi wakiandikishwa. Hakuna nchi iliyoendelea bila kuweka kipaumbele kwenye elimu. Mheshimiwa rais aliliona hili na ndio maana akaanzisha mpango huu kabambe wa elimu bure ili watoto wetu wengi wasome bila kujali uwezo wetu kiuchumi sisi wazazi.

Leo tunashuhudia idadi ya watoto wanaoandikishwa ni mara mbili ya ile idadi ya awali. Hii ni kutokana na huu mpango wa elimu ya awali, msingi na sekondari (hadi kidato cha nne) kuwa ya bure inayoendana na upanuzi au ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Wanafunzi wa vyuo vikuu, wengi leo wananufaika na mikopo ya elimu ya juu kutoka bodi ya mikopo, tofauti na hapo awali. Hii ni kutokana na mikakati maalumu ya Mheshimiwa Rais ili kufanikisha wanafunzi wengi wafaidike na mikopo hiyo. Miaka ya nyuma wanafunzi wengi walikuwa hawawezi kusoma vyuo vikuu kutokana na ufinyu wa bajeti iliyokuwa inatolewa kwa bodi ya mikopo.

Hivyo wanafunzi wengi waliokidhi vigegezo hawakuweza kujiunga vyuo vikuu kutokana na ufinyu huo. Leo hii Mheshimiwa Rais ametenga bajeti ya kutosha ili wanafunzi wengi waliodahiliwa vyuo vikuu waweze kusoma elimu ya juu. Tunataka Rais atufanyie nini zaidi ya haya?

Nchi nzima sasa hivi; kila mkoa, wilaya au kata, kuna harakati za kuanzisha viwanda, na hii ni chachu ya maendeleo katika taifa letu. Huu nao ni mpango mkakati wa Rais wetu. Tunashuhudia viwanda vingi vinaanzishwa (hasa kanda ya Mashariki), tutaona baada ya muda mfupi masoko yetu yatatawaliwa na bidhaa zetu za ndani na bidhaa zingine tutauza nje (export). Hizi ni jitihada za Mheshimiwa Rais.

Juzi mkoani Ruvuma (kwa Mheshimiwa Christina Mndeme, Mkuu wa Mkoa), wamefanya kongamano la viwanda na fursa za uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wa nje na wa ndani kuwekeza nchini. Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa waziri mkuu, Mheshimiwa Kasimu Majaliwa. Hii itatoa ajira kwa Wanaruvuma na wananchi wengine kwa ujumla.

Mheshimiwa Rais ameweza kuanzishwa kwa mradi wa umeme utokanao na maporomoko ya maji ya mto Rufiji(Stieglers Gorge) ambao uliasisiwa na Mwalimu Nyerere miaka mingi iliyopita. Mradi huo, ambao jana Mheshimiwa Rais aliweka jiwe la msingi, na kuamua kwa kauli moja na wananchi kuwa utapokamilika uitwe jina la muasisi wake (nadhani utaitwa Nyerere Hydroelectric Power), utakuwa chachu kubwa kwa maendeleo kwani viwanda vingi vitatumia nishati hiyo kwani gharama yake ni nafuu sana kulinganisha na nishati itokanayo na vyanzo vingine, kama vile injini za diesel, jua, upepo, jotoardhi, makaa ya mawe, uranium n.k Unafuu huu wa nishati utawezesha hata wananchi wa kawaida kuanzisha viwanda vidigovidogo na hata majumbani kwetu gharama ya nishati itapungua sana.

Bwawa hili sio tu litakuwa chanzo cha umeme, bali pia litatumika kwa shughuli za uvuvi, utunzaji wa mazingira, utalii n.k. Jamani, haya sio maendeleo?

Mheshimiwa Rais amekuwa mzalendo namba moja mwenye uchungu na maliasili za nchi yetu. Tumeshuhudia akizilinda rasilimali zetu kwa nguvu zake zote. Wengi tumeona anavyodhibiti madini, gesi, misitu, mito, hifadhi za wanyama za taifa n.k. Alipokuwa anatoka mapumzikoni hivi karibuni, aliwaambia wananchi wasimwage ovyo kemikali (zebaki) wanazotumia katika uchenjuaji wa madini kwani zina athali kwa uoto wa asili na pia kemikali zikiingia majini na kisha watu kunywa maji hayo, wanaweza kupata saratani.

Aliwashauri pia wapande miti ili kutunza mazingira. Jana tena akiwa anaweka jiwe la msingi, aliwaagiza viongozi wa wizara ya maliasili kuligawa eneo la Selous na kupatikana hifadhi ya taifa itakayoitwa Nyerere National Park. Kuhusu upande wa madini, tumeona mikataba ya madini imepitiwa upya na baadhi ya vipengele vimerekebishwa ili wawekezaji wasijinufaishe peke yao, bali pawe na faida pande zote mbili (win win situation) ili mwisho wa siku hawa wawekezaji watakapomaliza madini na kuondoka zao wasituachie mashimo tu bila faida yoyote.

Mheshimiwa Rais kaanzisha masoko ya madini nchi nzima ili sasa madini tunayochimba yauzwe ndani ya nchi na faida yake (mzunguko wa fadha) itumike hapahapa nchini. Hii pia itasaidia kutunza takwimu za mauzo (sales data) kwa ajili ya marejeo ya aina yoyote ile hapo baadaye.

Jitihada za Rais katika kudhibiti madini zimedhihirika tena pale dhahabu kilo 35 na shilingi milioni 500 zilipokamatwa uwanja wa ndege wa huko Kenya. Hizi ni jtihada za Mheshimiwa Rais, na tayari fedha hizo pamoja na zile zitakazopatikana baada ya dhahabu iliyokamatwa kuuzwa, amezielekeza katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Fuga (railway station) mpaka Nyerere Hydroelectric Power Station.

Mheshimiwa Rais, wananchi wanatambua jitihada zako katika suala zima la kuwaletea maendeleo. Hata hawa wanaokupinga sio kwamba hawatambui, ila wanafanya hivyo kwa maslahi (interest) yao. Na pengine nia yao ni kukupa hofu au kukukatisha tamaa. Lakini Rais wetu, kwa bahati nzuri, wewe moja ya taaluma zako ni ualimu, kwa hivyo una saikolojia ya hali ya juu na ndio maana hubabaiki kwa kuwa unajua maana ya kila wafanyalo.

Rais wetu mpendwa piga kazi, wananchi tupo pamoja na wewe. Sisi wananchi ndio tuliokuchaguwa wewe uwe kiongozi wetu na kwa hivyo una kibali mbele ya Mwenyezi Mungu, kwani sisi tuliokuchaguwa ni wa Mwenyezi Mungu.

Musa aliwaongoza wana wa Israel kutoka utumwani Misri kwenda nchi ya ahadi, Mheshimiwa Rais, utuongoze Watanzania katika zama hizi tunapongia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda. Tunazidi kukuombea kwa Mwenyezi Mungu.

HAPA KAZI TU.
 

Kwenye umeme kukatika umetukosea sana ndugu! Umeme kukatika kumepungua kwa 98% siku hizi ukiulizwa umeme ulikatika lini unaweza ushindwe kukumbuka. Mimi pamoja na kuwa nipo kariakoo iliyodorora lakini bado nakubali kuwa Rais Magufuli ni Rais sahihi sana kwa Taifa letu ila namwombea asikatishwe tamaa na hizi lawama , hasa kwenye Madini asilegee hata kidogo , endelea kuwabana Barick na makampuni mengine hadi kielweke , angalau madini yaweze kuchangia pato la Taifa.
 
Mkuu are you serious ???
Hauko serious kabbisa.
Vipi kuhusu Ubungo interchange??
Ile fly over ya mfugale ni awamu ya tano.
Mradi wa daraja la kigamboni na muhimbili cardiac institute ndio awamu ya kikwete.
 
Mkuu are you serious ???
Hauko serious kabbisa.
Vipi kuhusu Ubungo interchange??
Ile fly over ya mfugale ni awamu ya tano.
Mradi wa daraja la kigamboni na muhimbili cardiac institute ndio awamu ya kikwete.

Watanzania wengi hasa wadogo ni mbumbumbu daraja la salenda linajenga kwa msaada wa south Korea, fly over zote ni pesa ya bank kuu ya dunia na walianza toka zamani ukiona daraja leo planning imeanza zaidi ya miaka 5. Airport imejengwa kwa miaka mingi tu😂 lakini ndiyo inaisha. Hata treni plan haikuanza leo na plan ilikuwepo mpaka ya kujenga treni upande wa mtwara na lindi. Hebu tuletee budget ya serikali utuambie hizo fly over wamelipa lini😂 pumba tu
 
Mkuu are you serious ???
Hauko serious kabbisa.
Vipi kuhusu Ubungo interchange??
Ile fly over ya mfugale ni awamu ya tano.
Mradi wa daraja la kigamboni na muhimbili cardiac institute ndio awamu ya kikwete.

Fanyeni shughuli vijana badala ya kushinda mitandaoni tu wakati hamna kitu mifukoni nchi ni maendeleo ya vijana msisubiri serikali pekee na ushabiki kwenye kila kitu kidogo kinachojegwa ni mambo ya kawaida
 
Fanyeni shughuli vijana badala ya kushinda mitandaoni tu wakati hamna kitu mifukoni nchi ni maendeleo ya vijana msisubiri serikali pekee na ushabiki kwenye kila kitu kidogo kinachojegwa ni mambo ya kawaida
Waambie wasio nazo.
Maana mm nina maendeleo ya baba na mama wameniandalia.
Bado yangu nayaongezea.
Kwahiyo usione twashinda net ukadhan hoe hae.
Huwez kumkuta msomali Tz anakufa na njaa.
 

Hakuna kweli hata moja, wewe ni moja ya wale waongeao bila kushirikisha bongo
 

Utapata tabu sana kung’arisha kisicho ng’ara. Sisi wananchi tunataka kuona uchumi ukikua na mchikamano wa nchi, hizi ngonjera/poroje zote hazina mana kama nchi hali ni tete hivi.
 

Jiwe unayemsema ndiye chanzo cha matatizo makuu nchini
 
Waambie wasio nazo.
Maana mm nina maendeleo ya baba na mama wameniandalia.
Bado yangu nayaongezea.
Kwahiyo usione twashinda net ukadhan hoe hae.
Huwez kumkuta msomali Tz anakufa na njaa.

Tumia muda kujifunza maana madogo wa siku hizi mnaingia kwenye mijadala na kutoa pumba tu
 
Muanzisha uzi, kwa kuwa huu uzi umefika page zaidi ya 1,2000, ili anayeufungua leo aweze kupata kuyajua makubwa aliyoyafanya Rais Magufuli ungeyachukua kuyaweka kwenye updates za post yako ya kwanza.
 
Naipenda sana nchi yangu, kwani ni nchi inayoongozwa kwa utawala bora.


Nchi yangu [emoji1241] sasa tuna ndege za kutosha.

Barabara za juu na chini ambazo zinaendelea kujengwa.

Reli ya umeme ambayo pia inaendelea kujengwa.

Viwanda vingi vimejengwa na vingine vinaendelea kujengwa.

Wasomi wameongezeka na wengi wameajiriwa.


Nitakipenda zaidi Chama changu

Kwani kimefanya mambo mengi mno.
 
Umesahau majeruhi wa ajali ya tanker iliyotokea morogoro wanalamba laki ,tano cash..😛😜😜
 
Pia alimteua Jokate kuwa RC. Magufuli anajua kurudisha shukurani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…