Hakika hili ndilo swali linalogonga katika vichwa vya baadhi ya watu wakijiuliza namna Rais wa Tanzania Mh.Dr.John Pombe Magufuli alivyoweza kuleta maendeleo makubwa ya maajabu ndani ya kipindi cha miaka minne cha muhula wake wa kwanza.
Hebu fikiria anajenga mradi mkubwa wa kufua umeme wa Nyerere katika Bonde la Mto Rufiji, anajenga reli ya kisasa itakayotumia treni za umeme(Standard Gauge), elimu bure anatoa Bilion 23 kila mwezi kugharamia mpango huo,amenunua ndege kwa pesa taslimu ( cash Money) amejenga vituo vya afya zaidi 300 nchi nzima sambamba na vifaa tiba,hospital mpya za wilaya 67, kwenye miundombinu ya barabara ndio usiseme lami zinatandikwa nchi nzima,miradi ya maji safi na salama ipatayo 1,801ambayo mpaka sasa miradi 500 ipo katika hatua mbalimbali ya utekelezwaji, umeme Vijijini,mwendokasi awamu ya 3 Mbagala,DSM na mengineyo mengi nikisema niyaandike yote hapa sitomaliza.
Sasa hivi hakuna sehemu hata moja Tanzania ambayo Kama ukitembelea lazima ukute shughuli fulani ya maendeleo inaendelea,ama iwe mradi wa maji,umeme,barabara,ujenzi wa zahanati N.K.
Ni miaka minne ya mafanikio makubwa, ni miaka minne ya uthubutu ,utashi ,uzalendo,l na uchapakazi wa hali ya juu wa Rais Magufuli.
Tuendelee kujivunia mafanikio haya Tanzania inayopiga kwa kasi chini ya uongozi imara wa Serikali ya Chama Tawala.
Augustino Chiwinga
0621448591