Katika kipindi kifupi cha miaka 4 tumeshuhudia Rais wetu akisimamia kwa nguvu miradi mingi yenye thamani kubwa ya fedha na yote inatambaa kwa nguvu na speed kubwa.
Ni katika nchi hii tuliaminishwa kuwa hakuna hela, hela zinapatikana nje ya nchi tu. Lakini leo mheshimiwa rais amesema hela zipo hapa na nje hatoki na miradi inakwenda vizuri. Ni lazima tujiulize hizi hela zilikuwa wapi?
Badala ya kulalamika tujifunze mbinu anazotumia kupata fedha. Tuache kufanya kimoja kimoja kama tunaendesha familia zetu. Tukumbuke hii ni nchi siyo familia.
Rais wetu ana akili nyingi sana.
Tena katika kipindi cha miaka hii minne hata wazungu wasingeweza kwenda na hizi multiple and giant projects Kwa wakati mmoja. Only geniuses can do this.
Kwa wakati mmoja amefanya yafuatayo na yote yanatambaa.:
1. Ujenzi wa barabara zote zinaendelea na zina kamilika kwa wakati.
2. Ujenzi wa bwawa la umeme unaendelea na mkandarasi yuko sight
3. Ujenzi wa hospitali na vituo vya afya umekamilika kote nchini
4. Ujenzi wa stand za kisasa za mabasi nchi nzima
5. Ujenzi wa masoko nchi nzima
6. Ujenzi wa machinjio za kisasa
7. Ujenzi reli unaendelea
8. Ununuzi wa ndege
9. Uanzishwaji wa viwanda nchi nxima. Hadi sasa viwanda vimefufuliwa na kujengwa upya zaidi 4000.
10. Madawa supply ipo constantly kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya taifa
11. Usambazaji wa umeme mijini na vijijini unaendelea kwa kasi
12. Elimu bure inaendelea
13. Mishahara inalipwa kwa wakati.
14. Upanuzi wa viwanja vya ndege
15. Kuhamia Dodoma walisema hawezi sasa ameweza. Na amejenga temporary offices za wizara na permanent Ikulu.
16. Ujenzi wa hospitali ya uhuru
17. Ununuzi wa vivuko na meli
Yote haya yanakwenda kwa wakati mmoja. Only geniuses can do this coz anakuwa na planning.
Sasa vilaza ndo wanalalamika wanaona maajabu. Jamani ni kawaida tu msishangae tunachapa kazi. Na zote zitakamilika kwa 100% tumpe nafasi rais wetu achape kazi vilaza acheni kulalamika.
Usifikirie kama unaendesha familia yako fikiria kama unaendesha nchi. Hatutaki twende na kimoja kimoja nchi kubwa hii hatuta fika kwa wakati tunaotaka.
Tumechelewa mno, tumeibiwa mno.
Badala ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya rais wetu watu tuache kubeza juhudi hizi. Tumshukuru Mungu ampe afya njema rais wetu ili tufike mbali. Baada ya kipindi chake yawezekana tusipate mwingine kama huyu.
Tuache genius wetu afanye kazi.
Sent using
Jamii Forums mobile app