Uislamu na Ukristo ni dini mbili tofauti, zenye mitazamo tofauti kiimani.
Katika Uislamu, msikiti ni nyumba takatifu ya kiibada. Kuanzia kujengwa, kutumiwa na kutunzwa kwa msikiti kumewekwa taratibu na sheria katika uislamu. Sio jambo la holela holela.
Kitendo cha mtu mmoja (pasipo kutumwa na waislamu) kwenda kukusanya sadaka za waumini wa kikristo kanisani (mahali ambapo waislamu wanaamini 'makafir' hukusanyika kumwabudu Yesu kama Mungu wao na 'makafir' hao kufundishana namna ya kukabiliana kiimani dhidi ya uislamu) kwa lengo la kupata pesa za kwenda kujenga msikiti wa waislamu kumeleta mjadala mkubwa na mpana katika jamii.
Wapo ambao wanasema hicho ni kitendo cha utu, ujirani mwema na upendo baina ya dini mbili tofauti zenye kukinzani kiasili.
Lakini wapo wanaoamini kuwa hicho ni kitendo cha dhihaka ya kiimani dhidi ya uislamu, kuudhalilisha utu wa kiimani wa muislamu mbele ya mkristo na kunajisi imani ya takatifu ya kiislamu.
Karibuni tujadili kwa kina, hekima na staha, ili kujua kama jambo hilo ni jema (ili tujenge utamaduni wa kuliendeleza) au kama ni jambo baya (tulikemee na kulifuta katika jamii yetu).