Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mwaka 1971 General Idd Amin Dada alipompindua Milton Obote alipokelewa kwa shangwe mno na mategemeo makubwa kuwa atairekebisha Uganda. Baada ya muda aliwapa siku 90 waasia wote kuondoka na mali zao kuzitaifisha. Hapo ndio wananchi walipoongeza nyimbo na mapambio kwa Amin na kusema kweli huyu ameshushwa kwa ajili ya taifa lao.
Jambo ambalo linafanana na hapa kwetu kwa sasa ni kuwa Amin hakupenda kukosolewa na mwanzoni alianza kuwashughulikia wanaomkosoa softly, baadae kuwafunga na mwishoni kuwaua. Alipenda asifiwe yeye tuu mpaka akajipa mavyeo ya kijeshi na kifalme na endapo alitokea mwingine anayesifiwa zaidi yake alimpoteza.
Baya zaidi alikosa vision na mission za uchumi hivyo taifa likaanza kudorora kwa kasi na ndipo anguko lake lilipo shika kasi.
Aliweza kukaa madarakani miaka minane sio tena kwa ridhaa ya watu wake waliomshangilia na kumsifu awali bali nguvu za kijeshi.
Kuna kitu twaweza kujifunza hapo, anayekubali kukosolewa ana nafasi ya kufanya vizuri lakini akataaye na kuabudu sifa hana nafasi ya kufanikiwa kwani atakwama
 
Tueleze yapi aliyokosolewa JMP hakayataa. Nakama kuna makosa kuna utaratibu wa kufuatilia ili mambo yarekebishwe.
 
Tueleze yapi aliyokosolewa JMP hakayataa. Nakama kuna makosa kuna utaratibu wa kufuatilia ili mambo yarekebishwe.
Mbona utaratibu huo hautumiki kwenye kuhamisha matumizi ya fedha za umma? Mbona utaratibu huo hautumiki kwenye kuwashughulikia kina Lugumi, Nyumba za umma, Meli Chakavu, Escrow, Richmond Dowans,Kiwira, rada n.k.

Chama Cha Majipu (CCM) kimekosa pumzi.
 

Bado haja raisisha uwekezaji wa biashara, na bado kuanzisha biashara na kuagiza vitu kutoka nje karibu haiwezekani.
Bado anapandisha kodi kwenye sekta ambazo isinge kuwa kwa hizo kodi watu wangeweza kupanua biashara zao na kuajiri watu.
Bado ananyanyasa haki za uhuru wa kusema (freedom of speech) na watu wanaenda jela kisa wamemtukana raisi. Akati Raisi mwenyewe hata hafiki kwenye top 50 list ya powerful leaders in the world. Hapo ndipo unaona alivyo insecure.
Bado hajaleta mashindano kwenye uzalishaji wa umeme na bado kuna monopolies kwenye sekta za viwanda, afya, elimu na ujenzi.
Bado hajaimarisha haki za kumiliki mali (private property rights) kwa wananchi wa ndani na wawekezaji wa nje. Investors hawataki kuja ku invest alafu mali zao zinyang'anywe tu na serikali, kisa serikali inajisikia.
Bado hajatatua tatizo la sukari, barabara na umaskini wa vijijini, mambo ambayo ni rahisi kutatua kiasi kwamba unaweza ukamuuliza economist yeyote atakwambia jibu.
Bado hajaimarisha uhusiano na nchi zinazotuba msaada na anaonesha ubabe kitu ambacho kimekatisha msaada na kumlazimisha aongeze kodi kwa wananchi wake wenyewe.
Kaharibu biashara bandarini mpaka bandari la Zanzibar linatupita.
Yani ninaweza kuendelea na mambo Magufuli hayawezi ikija kwenye economic policies mpaka kesho kutwa alafu una ushujaa wa kuja kusema umefurahishwa naye.
 
JPM nampa more respect. Hata binti yangu kapewa mkopo tena % za maana.

Rais anajuwa watanzania ni maskini. Ilifikia nahali watu wa chini tulipoteza dira. Heshima sana kwako Dr JPM.
 
Wewe naina interest yako ni wadada tu mkuu ha ha ha
 
Hutaki kulipa kodi ila unataka maendeleo? hii ni hesabu ya wapi hii ya kula bila kutokwa jasho?

Hahaha aliyekwambia kodi inaleta maendeleo ni nani. Na wanao kula bila kutoa jasho ni wanasiasa ambao hawafanyi biashara yeyote wala kazi yeyote ya maana lakini wako tayari kuongeza kodi wanapojisikia na kunyang'anya mali za watu ambazo hawaja zifanyia kazi na kuendesha magari ya kifahari akati hao watanzania wanofanya kazi juani siku nzima wanapanda mabasi.
Soko binafsi ndiyo pekee linaleta maendeleo. Kutoka bandarini mpaka kwenye utengenezaji wa umeme, barabara, ujenzi, hospitali, shule, vyuo, usafiri e.t.c kampuni bora, huduma bora, na bei au garama za chini zinatokana na mashindano kwenye sekta binafsi. Serikali ya tanzania hailewi hili swala ndiyo maana kila mwaka wanasoma bajeti na wanahitaji kuongeza hela ya matumizi kwasabu serikali yenyewe ikijidai itatatua matatizo ya kila mtu haitaweza kwasababu haina faida wala haitengenezi ela yake yenyewe. Kila siku itahitaji ela ya wananchi na kila siku kutakua na tatizo jipya ambalo sekta binafsi lingefanya kazi bora zaidi ya kulitatua.
 
Nia njema kwa sukar kg, 5000?
 
Wewe lazima utakuwa unakula bure na kulala bure ombi langu kama ujawa na majukumu yoyote yale usipende sifia sifia mambo kuwa uyaone TE="MJENGA, post: 14573380, member: 110291"]Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.[/QUOTE]
Wewe
 
Sithani kama rais amevunja sheria yoyote kuhamisha matumizi mfano mahakama waliagiziwa kupewa hela lakini hawakupewa kama inavyotakiwa alichofanya rais ni kuagiza zipelekwe, jinsi alivyosema ilionekana kama ameamisha lakini ukiangalia kwenye vifungu vya sheria hajavunja sheria. Masuala mengine kuna taasisi zinashughulia hivyo vitu. Mambo ya nyumba muulize mkapa kwani yalifanywa wakati ule na alitekeleza kama boss wake alivyomwagiza.
 
[emoji134] Ila Hapo Kwny Rushwa Umewaona Polisi Tu[emoji3] [emoji3]
 
MWENYE ENZI MUNGU TUBARIKI WATANZANIA NA RAISI WETU MILELE YOTE!
 
Ukiweka orodha ya sekta za rushwa humu ni nyingi, huo ulikuwa mfano tu...
Sawa Bana Lakn Futa Kauli Yako Maana Unavunja Kanuni Za Bunge[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Sawa Bana Lakn Futa Kauli Yako Maana Unavunja Kanuni Za Bunge[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]

Mmmmmmmmmhhhhh kauli gani tena nifute, nimekiuka kanuni gani ya bunge, comrade uniambie mapema kwani hii sheria ya mtandao ni hatari....
 
Mmmmmmmmmhhhhh kauli gani tena nifute, nimekiuka kanuni gani ya bunge, comrade uniambie mapema kwani hii sheria ya mtandao ni hatari....
Sasa Hapa Nitamuita Sajent At Army Akutoe Nje Maana Unakiuka Kanuni Ya 64-1 Kuongea Bila Kituo.

Halafu Hilo Jina Komredi Halipo Kwny Kanuni Za Bunge, Niite Mh Tafadhari[emoji87]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…