Mafanikio ya Rais Samia kwa 3 years ni yapi? Nijue nikae sawa

Kiongozi aliyeleta mafanikio katika hii Nchi ni Nyerere pekee,wengine hao mafanikio yanatokana mabadiliko ya kimazingira ya siasa za Dunia na naturally

wewe ndio huna akili nyerere lini alileta maendeleo nchi hii weww unaonekana enzi za nyerere hujazaliwa. mimi nina miaka 67 sasa hivi enzi za nyerere maisha yalikuwa ya kijela, dawa ya mswaki mnapewa kibali kila kaya dawa ya mswaki 1 kilo ya sukari sabuni ya kufulia miche 2 kila kaya kwa kibali ndio uende duka la serikali RTC ukanunue tena kwa foleni dukani walikuwa wanauza unga wa ugali uliitwa unga wa yanga mchungu sana hayo ndio yalikuwa maisha ukiwa na TV wewe jela mpaka ukakatie kibali upewe kadi kama kadi za gari watu wadhulumiwa nyumba zao na kupewa NHC na watu wengi walifariki kwa mawazo nyumba zilijengwa kabla ya uhuru wakaja wahindi kudhulumiwa weww ulikuwa wapi?
 
Umeliweka vizuri, kama mtoa mada hatakuelewa atakuwa ni mlemavu wa akili
 
Tofauti ya Samia na Magufuli ni kwamba Magufuli alikuwa anajitangaza sana yeye mwenyewe na wasanii kuhusu mambo aliyoyafanya. Halafu Magufuli alikuwa mwongo kwa kuwa alikuwa anaponda watangulizi wake, hasa Kikwette.

Kwa mfano mambo ya barabara za Dar es Slaam chini ya DMDP na daraja la Tanzanite ni miradi iliyofanyiwa planning, financing na kuwa launched na JK kati ya 2012 na 2015.

Hayo madaraja ya Tazara na Ubungo yalikwishafanyiwa kazi zote na JK lakini mshamba yule alikuwa haonyeshi credit kwa JK
 
Nyie watu muwe na huruma.
Hata kama si kwa viwango mlivyotarajia lakini amefsnya hivyohivyo..si kwamba hajafanya chochote.

Mama wa watu si ajabu anakosa hata muda wa kulala

Nilikuwa najaribu tu kuwaza,wote tuna 24 hrs..
Kesho yupo huku,kesho kaamkia huku,
Keshokutwa kule,yaani ni purukushani tupu.
Tumpe appreciation hata kwa kidogo hichohicho anachokifanya.
 
Naona kabisa dalili za awali za kumpoteza mwanamageuzi ..CCM haitakiwi kusifiwa kwa chochote ndani ya nchi hii, imetuchelewesha sana, kwa muda iliokaa ilibidi tuwe tunalisha africa nzima
 
Naona kabisa dalili za awali za kumpoteza mwanamageuzi ..CCM haitakiwi kusifiwa kwa chochote ndani ya nchi hii, imetuchelewesha sana, kwa muda iliokaa ilibidi tuwe tunalisha africa nzima
Ujicheleweshe mwenyewe na ujinga wako uje kulaumu wengine?
 
Naona kabisa dalili za awali za kumpoteza mwanamageuzi ..CCM haitakiwi kusifiwa kwa chochote ndani ya nchi hii, imetuchelewesha sana, kwa muda iliokaa ilibidi tuwe tunalisha africa nzima
Katika hali ya kibinadamu huruma imeniingia.
Kwamba hajafanya chochote?
Jamani nyie🥺
 
By the way SAMIA ukimlinganisha na mtangulizi wake-Magufuli,SAMIA ana mafanikio mengi zaidi.
1.Democracy
2.Uchumi
Uchumi kwa lipi wakati shilingi inapoteza thamani na vyakula na bidhaa muhimu zimepigwa na mfumko wa bei?
Maisha yamekuwa magumu na watu wengi wanaishi kwa stress
 
Katika hali ya kibinadamu huruma imeniingia.
Kwamba hajafanya chochote?
Jamani nyie🥺
Sio swala la huruma ni kusutwa nafsi Kwa sababu unajua kabisa unaongea uongo na unafiki.

Leo hii kuanzia form standard 7 Hadi university ni Elimu Bure maana hata huko university wanafunzi wowote wamepata mikopo ndio maana husikii kelele.

Wengine ni Watumishi wanafahamu fika kabisa Rais Samia kawaongezea salary hususani Watumishi wa kada za chini ambao ndio wengi,wamelipwa malimbikizo,wamefutiwa Madeni ya Bodi na Mimi binafsi nimemaliza deni mwezi wa 6 bila Samia lilikuwa haliishi.

Hapo sijataja maelfu ya Ajira alizomwaga Toka amekuwa Rais.
 
By the way SAMIA ukimlinganisha na mtangulizi wake-Magufuli,SAMIA ana mafanikio mengi zaidi.
1.Democracy
2.Uchumi
Uchumi upi?huu ambao vitu vimepanda bei,hakuna umeme wa uhakika,hakuna nishati ya mafuta ya uhakika? uchumi n
umeharibika sana.
 
Uchumi kwa lipi wakati shilingi inapoteza thamani na vyakula na bidhaa muhimu zimepigwa na mfumko wa bei?
Maisha yamekuwa magumu na watu wengi wanaishi kwa stress
Ni lini Shilingi haijawahi poteza thamani dhidi ya Dola? Tafuta thamani ya Dola 2015 harafu uke uangalie 2020 ulete jibu au miaka yote ya nyuma.

Hiyo imekuwa trend ya uchumi wa Tanzania Kwa mda mrefu sana Sasa.

Mwisho Shilingi kupoteza thamani haona athari zozote za kuhimiza uchumi.Mnatakiwa kujielimisha maana ya Uchumi kabla ya kupayuka.

Lugha rahisi ya kuelezea uchumi kupungua ni kupungua Kwa uzalishaji,swali.uzalishaji umepungua? Jibu ni hapana.Kiwango.cha mikopo kwenda sekta binafsi kiko Juu kuliko wakati wowote katika haistoria ya Tanzania ndio sababu husikii Benki zikipata hasara Wala mikopo chechefu kama ya awamu ya 5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…