Kwani wewe unadhani hawajui kuwa JK kafanya kazi nzuri sana
Ila tu inabidi wamshushe kwa sababau wasipofanya hivyo viatu vya JK ni vikubwa sana kwa wao kuvivaa!
Ngoja niongeze vitu vingine katika achievement za JK
35. Zana nzito za kutisha za jeshi letu
36. Mfumo wa IT wa kukusanya mapato wa Halmashauri na e-Government
37. Ajira kwa vijana (Bodaboda, Bajaji, M-Pesa, Tigo-Pesa, HalotelMoney)
38. Kununua Vivuko kibao nchini kwa mfano kununua MV Magogoni, MV Utete, ununuzi wa MV Pangani, MV Kinesi etc
39. Kufanyia repair vivuko kibao kama vile MV Alina, MV Kigamboni, MV Sebgerema etc
40. Miradi kibao ya Kilimo kwa mfano kufungua chuo kuu cha kilimo cha Mwalimu Nyerere huko Butiama
41. Miradi ya maji ya bomba na visima kibao, mfano Maji ya bomba ni mradi kama wa Ruvu chini unaosupply Bagamoyo, Bunju na Makongo
42. Kuongezeka kwa wanafunzi wanaopata mkopo chuo kikuu, Ikumbukwe JK ndo aligeuza vyuo vinavyotoa advanced diploma kuwa vya digree na alitoa mikopo kwa wanafunzi wengi mno katika utawala wake
43. Kwenye afya alipambana vilivyo na ugonjwa wa Malaria,
44. Kwenye Kilimo wakulima wa Kahawa, Korosho, Mbaazi, Alizeti, walipata neema sana
45. Aliibadirisha sheria ya madini ile ya mzee Ben angalau tukaanza kunufaika na madini (Achilia mbali sarakasi za kina mruma za kudai tunadaiwa trilion 425 ambazo hatupewi ng'o)
46. Aliukarabati uwanja wa mpira wa Uhuru (Shamba la Bibi) siku hizi una majukwaa na pitc nzuri sana
47. Aliwekeza pia ktk michezo kwa mfano, kutuletea makocha wa nje kama vile Maximo na kusaidia kuleta Hamasa ya mpira na watu kuipenda timu yao ya Taifa
48. Aligawa chakula kwenye majanga kama vile njaa, penye ukame aligawa chakula, alisema hakuna ambaye angekufa kwa njaa
49. Kijeshi alitupa heshima, Aliwatwanga M23, Alimnyoosha Kanali Bacar wa Anjuani Comoro
50. Aliipa heshima TZ kidiplomasia, alisuluhisha migogoro mingi ya majirani wetu kama vile Kenya etc
51. Aliongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilion 160 kwa mwezi mwaka 2005 hadi shilingi bilion 850 kwa mwezi mwaka 2015
52. Ujenzi wa nyumba za sehemu mbalimbali nchini kwa mfano huko Kimbiji, Tabata n.k
53. Mafanikio ya NHC na NSSF kwenye kujenga nyumba nzurinzuri nchi nzima za bei nafuu
53. Angalau alitutoa ushamba kwa kuvutia investment kama vile Mlimani City na Mashopping malls mbalimbali katika miji mikuu
53. Angalia daraja kama la Furahisha mwanza
54. Miradi ya stendi mbali mbali kama vile ile ya Mbezi Mwisho, Stendi ya Tegeta kwa gari zinazoenda Bagamoyo
55. Kwa mara ya kwanza tangu nchi hii ipate uhuru aliruhusu taarifa za CAG ziwe zinasomwa na kujadiliwa bungeni
56. Alituruhusu tuone Bunge Live, siku hizi wananchi hawaelewi sana kinachoendelea huko bungeni