Umenena vyema.
Kwa haya uliyoyaandika na yaliyoorodheshwa na mleta mada, nina hakika awamu hii mpaka sasa hawajafikia hata 10%. Hata kama wakiongezewa miaka iliyobakia, sidhani kama watafikia hata 30%.
Awamu hii wamekwishaharibu kwenye eneo la uchumi, ari ya utendaji kazi na uzalishaji, kamwe hawawezi kufanya makubwa.
Kikwete alifanikiwa kwa vile kulikuwa na fedha. Uwekezaji wakati wa kikwete ulifikia ukuaji wa 28%, sahizi ni 4% tu! Uwekezaji huongeza pesa ya kodi lakini pia huleta fedha toka mataifa ya nje na kuhuisha uchumi wa ndani. Huyu amefukuza uwekezaji wa nje na hata kuondosha ambao tayari ulikuwepo ndani ya nchi. Angalia akina Bakhresa walivyowekeza SA, Burundi, Zambia n.k. Angalia viwanda vya cement vinavyojengwa na Watanzania nchini Msumbiji. Angalia vituo vya mafuta vinavyojengwa na Watanzania nchini Zambia, n.k. Angalia wawekezaji waliokuwepo Tanzania walioenda kuwekeza Mauritius. Wawekezaji wamekosa confidence ya mazingira ya uwekezaji Tanzania. Ni vigumu sana kuwarudisha au hata kuwaleta wapya.
Kikwete aliongeza sana uzalishaji na mauzo ya nje ya zao la korosho. Pesa hiyo ilisaidia mzunguko wa fedha na uletaji wa fedha za kigeni. Huyo ameua mauzo ya nje ya zao la korosho. Taarifa ya BoT inaonesha thamani ya mauzo ya mazao ya nje yameingia kwenye negativr growth. Haijawahi kutokea tangu uhuru.
Kikwete alijitahidi sana kuendeleza sekta ya utalii. Utalii ulifikia ukuaji wa 15%. Ongezeko la ukuaji wa utalii, liliifanya sekta ya utalii kuongoza katika uingizaji wa fedha za kigeni, ikifuatiwa na sekta ya madini. Huyu wa sasa ameushusha ukuaji wa sekta ya utalii mpaka 3.6%. Sasa hata wakija watalii 500, inatangazwa nchi nzima ili tujue kuwa watalii bado wanakuja!
Kikwete aliimarisha sana mahusiano ya nje. Licha ya kupata fedha kutoka kwenye uchumi uliokuwa unanawiri lakini pia aliweza kupata fedha nyingi za misaada na mikopo rahisi bila shida. Kwa nchi kama ya kwetu huwezi kupaa kiuchumi bila kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na misaada na mikopo. Ni wakati wa Kikwete, Tanzania ilikuwa ndiyo nchi ya kwanza katika Afrika kuweza kupata msaada mkubwa toka Marekani, ikifuatiwa na Ghana. Huyu alipokuja kutokana na mambo ya hovyo aliyoanza nayo pesa hiyo TZS 1.3 trillion tuliyokuwa tukiioata kila mwaka, ikapotea. Wenzetu Ghana walibahatika kupata mwendelezo mzuri wa uongozi, wanaendelea kupata mpaka leo, na Ghana inaongoza kwa ukuaji wa uchumi Afrika, na kuna wakati iliongoza kwa ukuaji wa uchumi Duniani. Ujerumani, ni kati ya mataifa yenye uchumi mzuri sana Duniani lakini ili kupiga hatua za maendeleo, baada ya vita kuu ya Dunia, ilipewa misaada. Misaada siyo mibaya, kama utaitumia kama mtaji.
Katika ujumla wake, ukiyatazama ambayo yalifanyika wakati wa Kikwete, tuwe wakweli wa nafsi zetu, yanayofanyika sasa ni kidogo sana yasiyostahili hata ulinganifu, lakini kelele ya kuyasifia imekuwa kubwa kuliko uhalisia. Nini cha ajabu kilichofanyika awamu hii ambacho hakikuwahi kufanyika?
Mwalimu Nyerere aliipokea nchi ikiwa haina grid ya Taifa. Alijenga grid ya Taifa. Alijenga mabwawa kama kidatu na Mtera. Kikwete akaongeza vyanzo vipya vya umeme wa gas. Kwa hiyo ujenzi wa bwawa jingine jipya awamu hii siyo kitu cha muujiza. Ni jambo la kawaida kwa nchi inayokuwa na ongezeko la watu.
Mwalimu Nyerere alinunua ndege 14 mpya, hakuna pangaboi hata moja. Sasa ndege za safari hii ni muujiza?
Wakati wa mwalimu kulijengwa reli toka Dar mpaka Kaprimposhi Zambia, karibia 2,000km. Sasa hii ya 300km ndiyo uwe muujiza?
Hospitali kama Muhimbili, na karibia zote za mikoa zilijrngwa wakati wa Mwalimu. Kikwete kioindi chake kulijengwa hospitali kubwa na uimarishaji wa hudumu za afya kwa kuboresha miundombinu yake. Sasa zahanati za awamu hii ziwe muujiza?
Hatujafikia pakulinganisha miradi ya awamu hii na ile ya awamu ya kwanza au awamu ya nne. Bado sana. Nauliza mambo machache:
1) Miaka 4 imepita, barabara km ngapi za lami zimejengwa awamu hii linganisha na 14,000km wakati wa Kikwete?
2) Madaraja makubwa mangapi yamejengwa awamu hii linganisha na madaraja 6 wakati wa Kikwete?
3) Ongezeko la la makusanyo ya serikali kwa 500% wakati wa Kikwete linganisha na ongezeko la sasa la makusanyo ya serikali
4) Linganisha ujenzi wa hospitali kubwa tatu (Mkapa, JK taasisi ya moyo na Mloganzila) zilizojengwa wakati wa Kikwete linganisha na awamu hii (hakuna hata moja labda ununuzi wa vifaa)
5) Linganisha ongezeko la wanafunzi wa vyuo vikuu lililoendana na ongezeko la mikopo, ujenzi wa UDOM na ubadilishaji wa vyuo vya kawaida kuwa vyuo vikuu, kutoka wanafunzi 3,000 mpaka 14,000. Ongezeko la 466%. Huyu wa sasa ameongeza wangapi?
6) Uletaji wa wawekezaji wakubwa kama Dangote wa zaidi ya $700m ulioendana na ajira za Watanzania 10,000. Huyu wa sasa ameleta uwekezaji gani ambao hata wa kufikia angalao $500m, na ajira za mara moja japo 5,000 tu? Au ndiyo vile viwanda 4,000 vilivyoajiri watu 12,000 (yaani kila kiwanda kina wafanyakazi 3!!!)
Awamu hii wafanye kazi lakini hawajafikia popote kiasi cha kujilinganisha na awamu iliyopita au awamu ya Mwalimu Nyerere. Wameharibu mambo mengi kwenye uchumi, wajisahihishe ili Mungu akiwajalia uhai, warekebishe katika kipindi cha pili. Kwa kipindi hiki their performance is very minimum, below our expectation.
Kwani wewe unadhani hawajui kuwa JK kafanya kazi nzuri sana
Ila tu inabidi wamshushe kwa sababau wasipofanya hivyo viatu vya JK ni vikubwa sana kwa wao kuvivaa!
Ngoja niongeze vitu vingine katika achievement za JK
35. Zana nzito za kutisha za jeshi letu
36. Mfumo wa IT wa kukusanya mapato wa Halmashauri na e-Government
37. Ajira kwa vijana (Bodaboda, Bajaji, M-Pesa, Tigo-Pesa, HalotelMoney)
38. Kununua Vivuko kibao nchini kwa mfano kununua MV Magogoni, MV Utete, ununuzi wa MV Pangani, MV Kinesi etc
39. Kufanyia repair vivuko kibao kama vile MV Alina, MV Kigamboni, MV Sebgerema etc
40. Miradi kibao ya Kilimo kwa mfano kufungua chuo kuu cha kilimo cha Mwalimu Nyerere huko Butiama
41. Miradi ya maji ya bomba na visima kibao, mfano Maji ya bomba ni mradi kama wa Ruvu chini unaosupply Bagamoyo, Bunju na Makongo
42. Kuongezeka kwa wanafunzi wanaopata mkopo chuo kikuu, Ikumbukwe JK ndo aligeuza vyuo vinavyotoa advanced diploma kuwa vya digree na alitoa mikopo kwa wanafunzi wengi mno katika utawala wake
43. Kwenye afya alipambana vilivyo na ugonjwa wa Malaria,
44. Kwenye Kilimo wakulima wa Kahawa, Korosho, Mbaazi, Alizeti, walipata neema sana
45. Aliibadirisha sheria ya madini ile ya mzee Ben angalau tukaanza kunufaika na madini (Achilia mbali sarakasi za kina profesa mruma za kudai kuwa tumeibiwa na ACACIA madini na kodi vyenye thamani ya trilion 425 )
46. Aliukarabati uwanja wa mpira wa Uhuru (Shamba la Bibi) siku hizi una majukwaa na pitch nzuri sana
47. Aliwekeza pia ktk michezo kwa mfano, kutuletea makocha wa nje kama vile Maximo na kusaidia kuleta Hamasa ya mpira na watu kuipenda timu yao ya Taifa
48. Aligawa chakula kwenye majanga kama vile njaa, penye ukame aligawa chakula, alisema hakuna ambaye angekufa kwa njaa
49. Kijeshi alitupa heshima, Aliwatwanga M23, Alimnyoosha Kanali Bacar wa Anjuani Comoro
50. Aliipa heshima TZ kidiplomasia, alisuluhisha migogoro mingi ya majirani wetu kama vile Kenya etc
51. Aliongeza ukusanyaji wa mapato kutoka shilingi bilion 160 kwa mwezi mwaka 2005 hadi shilingi bilion 850 kwa mwezi mwaka 2015
52. Ujenzi wa nyumba za sehemu mbalimbali nchini kwa mfano huko Kimbiji, Tabata n.k
53. Mafanikio ya NHC na NSSF kwenye kujenga nyumba nzurinzuri nchi nzima za bei nafuu
53. Angalau alitutoa ushamba kwa kuvutia investment kama vile Mlimani City na Mashopping malls mbalimbali katika miji mikuu
53. Angalia daraja kama la Furahisha mwanza
54. Miradi ya stendi mbali mbali kama vile ile ya Mbezi Mwisho, Stendi ya Tegeta kwa gari zinazoenda Bagamoyo
55. Kwa mara ya kwanza tangu nchi hii ipate uhuru aliruhusu taarifa za CAG ziwe zinasomwa na kujadiliwa bungeni
56. Alituruhusu tuone Bunge Live, siku hizi wananchi hawaelewi sana kinachoendelea huko bungeni