Umenena vyema.
Kwa haya uliyoyaandika na yaliyoorodheshwa na mleta mada, nina hakika awamu hii mpaka sasa hawajafikia hata 10%. Hata kama wakiongezewa miaka iliyobakia, sidhani kama watafikia hata 30%.
Awamu hii wamekwishaharibu kwenye eneo la uchumi, ari ya utendaji kazi na uzalishaji, kamwe hawawezi kufanya makubwa.
Kikwete alifanikiwa kwa vile kulikuwa na fedha. Uwekezaji wakati wa kikwete ulifikia ukuaji wa 28%, sahizi ni 4% tu! Uwekezaji huongeza pesa ya kodi lakini pia huleta fedha toka mataifa ya nje na kuhuisha uchumi wa ndani. Huyu amefukuza uwekezaji wa nje na hata kuondosha ambao tayari ulikuwepo ndani ya nchi. Angalia akina Bakhresa walivyowekeza SA, Burundi, Zambia n.k. Angalia viwanda vya cement vinavyojengwa na Watanzania nchini Msumbiji. Angalia vituo vya mafuta vinavyojengwa na Watanzania nchini Zambia, n.k. Angalia wawekezaji waliokuwepo Tanzania walioenda kuwekeza Mauritius. Wawekezaji wamekosa confidence ya mazingira ya uwekezaji Tanzania. Ni vigumu sana kuwarudisha au hata kuwaleta wapya.
Kikwete aliongeza sana uzalishaji na mauzo ya nje ya zao la korosho. Pesa hiyo ilisaidia mzunguko wa fedha na uletaji wa fedha za kigeni. Huyo ameua mauzo ya nje ya zao la korosho. Taarifa ya BoT inaonesha thamani ya mauzo ya mazao ya nje yameingia kwenye negativr growth. Haijawahi kutokea tangu uhuru.
Kikwete alijitahidi sana kuendeleza sekta ya utalii. Utalii ulifikia ukuaji wa 15%. Ongezeko la ukuaji wa utalii, liliifanya sekta ya utalii kuongoza katika uingizaji wa fedha za kigeni, ikifuatiwa na sekta ya madini. Huyu wa sasa ameushusha ukuaji wa sekta ya utalii mpaka 3.6%. Sasa hata wakija watalii 500, inatangazwa nchi nzima ili tujue kuwa watalii bado wanakuja!
Kikwete aliimarisha sana mahusiano ya nje. Licha ya kupata fedha kutoka kwenye uchumi uliokuwa unanawiri lakini pia aliweza kupata fedha nyingi za misaada na mikopo rahisi bila shida. Kwa nchi kama ya kwetu huwezi kupaa kiuchumi bila kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na misaada na mikopo. Ni wakati wa Kikwete, Tanzania ilikuwa ndiyo nchi ya kwanza katika Afrika kuweza kupata msaada mkubwa toka Marekani, ikifuatiwa na Ghana. Huyu alipokuja kutokana na mambo ya hovyo aliyoanza nayo pesa hiyo TZS 1.3 trillion tuliyokuwa tukiioata kila mwaka, ikapotea. Wenzetu Ghana walibahatika kupata mwendelezo mzuri wa uongozi, wanaendelea kupata mpaka leo, na Ghana inaongoza kwa ukuaji wa uchumi Afrika, na kuna wakati iliongoza kwa ukuaji wa uchumi Duniani. Ujerumani, ni kati ya mataifa yenye uchumi mzuri sana Duniani lakini ili kupiga hatua za maendeleo, baada ya vita kuu ya Dunia, ilipewa misaada. Misaada siyo mibaya, kama utaitumia kama mtaji.
Katika ujumla wake, ukiyatazama ambayo yalifanyika wakati wa Kikwete, tuwe wakweli wa nafsi zetu, yanayofanyika sasa ni kidogo sana yasiyostahili hata ulinganifu, lakini kelele ya kuyasifia imekuwa kubwa kuliko uhalisia. Nini cha ajabu kilichofanyika awamu hii ambacho hakikuwahi kufanyika?
Mwalimu Nyerere aliipokea nchi ikiwa haina grid ya Taifa. Alijenga grid ya Taifa. Alijenga mabwawa kama kidatu na Mtera. Kikwete akaongeza vyanzo vipya vya umeme wa gas. Kwa hiyo ujenzi wa bwawa jingine jipya awamu hii siyo kitu cha muujiza. Ni jambo la kawaida kwa nchi inayokuwa na ongezeko la watu.
Mwalimu Nyerere alinunua ndege 14 mpya, hakuna pangaboi hata moja. Sasa ndege za safari hii ni muujiza?
Wakati wa mwalimu kulijengwa reli toka Dar mpaka Kaprimposhi Zambia, karibia 2,000km. Sasa hii ya 300km ndiyo uwe muujiza?
Hospitali kama Muhimbili, na karibia zote za mikoa zilijrngwa wakati wa Mwalimu. Kikwete kioindi chake kulijengwa hospitali kubwa na uimarishaji wa hudumu za afya kwa kuboresha miundombinu yake. Sasa zahanati za awamu hii ziwe muujiza?
Hatujafikia pakulinganisha miradi ya awamu hii na ile ya awamu ya kwanza au awamu ya nne. Bado sana. Nauliza mambo machache:
1) Miaka 4 imepita, barabara km ngapi za lami zimejengwa awamu hii linganisha na 14,000km wakati wa Kikwete?
2) Madaraja makubwa mangapi yamejengwa awamu hii linganisha na madaraja 6 wakati wa Kikwete?
3) Ongezeko la la makusanyo ya serikali kwa 500% wakati wa Kikwete linganisha na ongezeko la sasa la makusanyo ya serikali
4) Linganisha ujenzi wa hospitali kubwa tatu (Mkapa, JK taasisi ya moyo na Mloganzila) zilizojengwa wakati wa Kikwete linganisha na awamu hii (hakuna hata moja labda ununuzi wa vifaa)
5) Linganisha ongezeko la wanafunzi wa vyuo vikuu lililoendana na ongezeko la mikopo, ujenzi wa UDOM na ubadilishaji wa vyuo vya kawaida kuwa vyuo vikuu, kutoka wanafunzi 3,000 mpaka 14,000. Ongezeko la 466%. Huyu wa sasa ameongeza wangapi?
6) Uletaji wa wawekezaji wakubwa kama Dangote wa zaidi ya $700m ulioendana na ajira za Watanzania 10,000. Huyu wa sasa ameleta uwekezaji gani ambao hata wa kufikia angalao $500m, na ajira za mara moja japo 5,000 tu? Au ndiyo vile viwanda 4,000 vilivyoajiri watu 12,000 (yaani kila kiwanda kina wafanyakazi 3!!!)
Awamu hii wafanye kazi lakini hawajafikia popote kiasi cha kujilinganisha na awamu iliyopita au awamu ya Mwalimu Nyerere. Wameharibu mambo mengi kwenye uchumi, wajisahihishe ili Mungu akiwajalia uhai, warekebishe katika kipindi cha pili. Kwa kipindi hiki their performance is very minimum, below our expectation.