Mafanikio ya Utawala wa Jakaya Kikwete ndani ya Miaka 10

Hujaeleweka,wewe unalinganishaje mafanikio kati ya JK na JPM?
Mimi naona JK yupo mbali sana ukilinganisha na huyu wa sasa,yapi.maoni yako
Unalinganisha kwa mizani gani? Miaka minne kea miaka kumi?
Tuache ubabaishaji
 
Hivi JK angesimama upande wa EL mnafikiri CCM mngeweza kuudhibiti ule moto, EL kagombea kupitia upinzani mmeona ule moto wake sasa ingekuwa yuko ndani na anaungwa mkono na JK mnafikiri mngemuweza na jinsi mlivyowanafiki..

JK ashukuruwe kwa uzalendo wake na kujitenga na kundi lake japo aliwatumia kama ngazi halafu akawabwaga..
 
bora hako kakundi hakakuathiri mishahara wala biashara za watu
Hebu niambia kwa sasa Kabila zima kila kona kila wilaya, hata wakwere umewasikia kwenye ukurugenzi wowote?
Akili Kama hizi ni matope au makamasi!? VP, PM, Speaker, Hawa ni wakabila lake!? Wakifika mawaziri Wa5 yaan Full minister wanatoka kabila lake anagalau andiko lako tulipe uhalali!?? Ukiondoa CDF tu , IGP, CGP, CGF, CGI hawa n wakabila lake!?? Njoo Mpk Boss wa TISS nae ni wakabila lake!??


Mkuu kuna wakati wewe na wapumbavu wengine wenzio huwa mnaamua tu kutype chochote baada ya kuvimbiwa kande!!!
 
Waalimu walikua wanapata matunzo sana (Shemeji) Hali kwa sasa ni ngumu (Shemeji)
 
Mkuu umeua kabisaaa...Yaani ni Pwentiii tupu ila hebu tudukiscuss hiyo namba 42 kuhusu mikopo!?? Hapo Kuna ukakasi kidogo hivi tukisema una watoto 10 ukawahudumia 9.. ilihali mwenzio kaja na watoto 20 akawahudumia 17.. hivi nani apo atakuwa kafanya kazi kubwa!! Ukidiscuss kwa figure ileile ambapo kimsingi ni ngumu kulingana na wakati ingeleta logic ila hapo siungi mguu hoja!!!
 
Wewe ni mzungu???
Kama na wewe ni ngozi nyeusi basi jua upo kundi moja na wapumbavu maana hata ulichoandika hapa ni upumbavu
 
Hivi hizo tenda si alikuwa anazisimamia mnyikulu .sijui bado anarun chini ya JPM. Hoja zote za hapo juu zinadhihirisha jinsi watanzania walivyokuwa wanafiki according to research .awamu ya nne mi karibia ingenipasua mchana kweupe.
 
JK alifanya mengi..lakini kwa haya machache nitaendelea kumkumbuka.
1. Serikali yake ambayo leo watu wanadai ilikuwa ya kifisadi ilitoa ushirikiano mkubwa kwa ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG. Mawaziri zaidi ya 13 wamepotezwa kutokana na uhuru mpana waliopewa CAG, BUNGE NA WAANDISHI WA HABARI.
2. Wakati wa utawala wa JK Wahalifu waitwao "WASIOJULIKANA" ambao wamejipatia umaarufu mkubwa kwenye zama hizi, hawakupata nafasi ya kuteka, kutesa na kuwapoteza moja kwa moja baadhi ya wananchi.
3. Pamoja na mazuri mengi aliyofanya JK hakuwahi kutumia majukwaa kujimwagia sifa, aliwaachia wananchi waseme
 
His own risk for his own choice,
and because he lost his choice, and again, on the other side the major rival also lost the battle, then he has got less risk.

Magufuli wasn't his choice,
And if in 4yrs tayari kumekucha kuanza kuwalinganisha basi kuna upande una speed inayomtisha aliyemtangulia, na wote wanaiona, yaani anayemfukuzia na anayefukuziwa,
Awamu hii inahubiri inayoyafanya ili watu waielewe awamu na kuiamini ipate support ya wananchi maana haina kundi la kisiasa la kuillinda,
Awamu inayoenda kuomba awamu bila kundi kama ilivyoingia bila kundi.
 
Tuorodheshe na mizigo aliotuachia,
1. Escrow
2. Kila nyumba ilikuwa na jenereta umeme haukuwa wa uhakika.
3. Iptl
4. Watu walijichukulia pesa ya umma wanavyotaka.
5. Ufisadi ulishamiri.
6. Shirika la ndege lilikufa
7. Shirika la reli lilikufa
8. Kampuni ya huduma za meli nayo ilikuwa taabani
9. Madeni ya wafanyakazi yaliongezeka
10. Mikopo ya vyuo kutofika kwa wakati hadi maandamano
11. Wizi ulishamiri hasa mabenki na mabasi kuvamiwa
12. Uraisi ilikuwa wa familia.
13. Miradi ilikuwa ya gharama kubwa kuliko uhalisia
14. Taiga walipanda ndege na hakujulikana aliyewapandisha.
15. Tembo na wanyama wengine walipungua kwa mask.
16. Maji yalikuwa Shida.
17. Mikataba mingi mibovu ilisainiwa.
18.
 
Baadhi ya hospitali za mkoa nazozijua ni hospitali ya rufaa ya mkoa wa singida,alipanua hospitali ya mkoa wa Mbeya na songea
Kati ya sekta ambazo Jk alifanya vizuri ni barabara,elimu,diplomasia,demokrasia na uchumi kiujumla ila shida yake kuu hakuwabana vilivyo aliowateua na kitendo cha demokrasia na uhuru wa kujieleza kuwa mkubwa kilisababisha viongozi wa serikali kushindwa kuelezea mafanikio ya serikali maana kwa sasa hata zahanati ikijengwa lazima tujue
 
Enzi za JK kwa watumishi bima ya Afya ulikuwa unaruhusiwa kumpachika yeyote unayemtaka la msingi usizidi ile idadi ya wategemezi, leo unaambiwa uwapachike mke wako,mzazi au watoto tu, huu ni upuuzi mkubwa sana, wanashindwa kujua kuwa kuna mtu hana baba wala mama mzazi ila kalelewa na ndugu na jamaa ambao leo wanahitaji msaada kutoka kwake....inasemekana serikali ilikusanya kidogo sana kulinganisha na leo, lakini naamini pesa ilikuwa kwenye mikono ya raia ndiyo maana watu waliishi maisha mazuri, walisomesha watoto, walijenga nyumba nk leo hii haya yamebaki historia. Sipendi watu kubeza jitihada za viongozi waliopita, naamini waliopita walifanya yao na waliopo pia wanafanya yao ili taifa liendelee, hakuna mtu mmoja anaweza kukamilisha kila kitu peke yake, hata JPM kwa sasa anafanya yake na wengine watakuja wafanye yao. Ila wote mnasema JK hakufanya kitu mnakosea sana.
 

Escrow na IPTL ni kitu kilekile kasome historia ya IPTL ilianza lini jamaa yangu na mkataba uliasainiwa lini..

Hakuna Kampuni au shirika hata moja lililomfia JK huwa mnasahau sana kasome tena historia, mashirika yalikufa awamu ya pili na ya tatu, tena awamu ya tatu ikaja kuyauza kabisa...
Ukiondoa mkataba wa Buzwagi nitajie mkataba mwingine mbovu uliosainiwa na JK, mikataba mingi mibovu inayoisumbua hii nchi ilisainiwa awamu ya tatu kama hujui pale tu sera ya ubinafsishaji ilipoanza..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…