Mafia: Watu 7 wafariki dunia baada ya kula nyama ya Kasa

Mafia: Watu 7 wafariki dunia baada ya kula nyama ya Kasa

Mkoa wa Pwani kuna Wilaya inaitwa Mafia ndio huko mkuu

Kasa Ng'amba huyu mtamu Ila ukimkuta amekula Mwani wenye sumu kaa mbali nae kukuua sumu yake ni dakika sifuriView attachment 2549436
Nimekupata, asante sana!

Hiyo wilaya imejitenga sana maana mara ya mwisho kusikia neno Mafia duu, miaka kadhaa imepita.
Kabila gani wanapatikana huko!?
 
Kwanini kwa sasa sio salama, ina maana siku za nyuma kasa alikuwa salama. Inakuaje anawaua na ni walaji wazoefu wa seafoods vyenye sumu wanajua
Kasa wapo wa aina mbili ukijichanganya ukamla mwenye sumu kwisha habar yako
 
Vijiwe vyako hivo lazima utambe
Huko nili hustle sana sema mwishowe huko nkaishiaga ngome [emoji1]
Uvuvi haramu, kisiwa kina wambea bana.....usifanye jambo [emoji1]
Risasi vidole kibao
Sema licha ya kashkash za huko mafia nlipapenda sana

Kuna pweza wengi sana sana nlikuwa na mradi mmoja niupigage huko
Wa kuleta pweza dar koki na makoki
Kuna wasomali fulani walikuwa wana kampuni yao inatwa Asmara walikuwa dar walikuwa wanahitaji
Ile najipanga nianze kuwaletea...
Jamaaa wakapotea hewani waliondoka
Mchongo ukafa bye bye

Ova
 
Watu wa baharini huko wana makankasha mi ntalala njaa kila siku.Nilienda Mtwara nikakuta wanauza tududu wamechomeka kwenye mijiti wanatutia kwenye pilipili wanabugia kama hawana akili.Walivyosegeza tu niliwaambia siwezi toeni huo uchafu.
Wanaitwa kumbwa, kukaa kwangu Mtwara nilishindwa kula, mm nilikuwa napga Kolekole tu
 
sasa hao haswa huyo papa na nguru umchome na moto mdogo mdogo kisha mihogo ya nazi ila kunyusa uliokolea nazi utakula had ukimbie, au upike bamia la kukoroga umtumbukize humo vitaaam
Yees hao watamu papa na nguru tena nguru wa kuchoma unaweza ukamla na ugali Safi kabisa hana shida,
 
😂😂😂Mi samaki wengine bhana yaani ile shape tu unaweza umsile.

Kuna samaki anaitwa sijui ndo kamongo tulikuwa tunakula sana Kuna mzee anatuletea maana ni mvuvi ila kila siku analeta mkia yaani ni mkubwa ..Yeye anauza kweny mahoteli makubwa basi bhana siku moja alikuja kutuambia "Huyu samaki ukija kumuona kichwa chake unaweza usimle".

Basi bhana Kuna siku alikuja usiku na kichwa cha huyo samaki maana wanakitumia kama kweny mambo ya ushirikina ili wavue Zaid samaki wengine ....Aisee sijui ndo jina halisi hilo kamonga maana Kuna watu kibao nawajua wanaitwa hivyo makonga.

Yule samaki ana kichwa kama cha ng'ombe na meno kama ya mtu 😟yaani ana mapembe hayo meno kama mtu niligopa sana ...Akatumbia huyu Bei yake ni ghali sana ..

Maana Kuna Yale majongoo ya baharini alikuwa anasafirisha kwenda Zanzibar pamoja huyo samaki eti watalii ndo wanakula.
huyo simjui, lakini kwa majongoo ya baharini nayafaham yako kama mafunza yana bei mno
 
Back
Top Bottom