Magari 56 ya Wakuu wa Wilaya kununuliwa mwaka wa fedha 2024/25

Magari 56 ya Wakuu wa Wilaya kununuliwa mwaka wa fedha 2024/25

Hii ndio Taarifa iliyokuja leo kutokea Bungeni, kama ilivyotolewa na Mohamed Mchengerwa ambaye ni Waziri wa TAMISEMI.

==
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema katika mwaka 2024/25, TAMISEMI imepanga kutumia shilingi bilioni 190.57 kwa ajili ya ununuzi wa magari ya Viongozi wa Mikoa na Wilaya, kuendelea na ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa miundombinu ya Mikoa ikiwemo majengo ya utawala, Ikulu ndogo, makazi ya Viongozi na Watumshi wa Mikoa, Wilaya na Tarafa katika Mikoa 26.

Mchengerwa ametoa taarifa hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo April 16, 2024 wakati akitoa hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2024/202 ambapo amesema shughuli zitakazotekelezwa katika utawala bora ni pamoja na ununuzi wa magari 9 ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Mikoa ya Katavi, Njombe, Iringa, Kigoma, Mwanza, Singida, Dar es Salaam na Manyara”

“Shughuli nyingine ni ununuzi wa magari 56 ya Wakuu wa Wilaya na 47 ya Wakurugenzi wa Halmashauri”
Haina shida tukutane 2025 ,uchaguzi ukifanyika, nchi sijui imerogwa na nani kwamba ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya sana hakuna magari , tunashindwa jifunza kwa Rais wa Zanzibar
 
Unakideri wewe, mtu yeyote nayejadili ni CHADEMA?

CHADEMA ilishakufa toka 2017 baada ya wabunge wake kununuliwa na mnnuaji.
2020 ikafa rasmi haina mbunge , sasa hao unaosema CHADEMA ni wapi ? Mbona nyie UVCCM hamusemi hawa watakuwa ni CUF, ACT,NCCR, NLD, UPDP vyama hivi si vipo?
😆😆😆😆😆😆
 
Hii ndio Taarifa iliyokuja leo kutokea Bungeni, kama ilivyotolewa na Mohamed Mchengerwa ambaye ni Waziri wa TAMISEMI.

==
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema katika mwaka 2024/25, TAMISEMI imepanga kutumia shilingi bilioni 190.57 kwa ajili ya ununuzi wa magari ya Viongozi wa Mikoa na Wilaya, kuendelea na ujenzi, ukarabati na ukamilishaji wa miundombinu ya Mikoa ikiwemo majengo ya utawala, Ikulu ndogo, makazi ya Viongozi na Watumshi wa Mikoa, Wilaya na Tarafa katika Mikoa 26.

Mchengerwa ametoa taarifa hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo April 16, 2024 wakati akitoa hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2024/202 ambapo amesema shughuli zitakazotekelezwa katika utawala bora ni pamoja na ununuzi wa magari 9 ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Mikoa ya Katavi, Njombe, Iringa, Kigoma, Mwanza, Singida, Dar es Salaam na Manyara”

“Shughuli nyingine ni ununuzi wa magari 56 ya Wakuu wa Wilaya na 47 ya Wakurugenzi wa Halmashauri”
Kama yanahitajika wanunue ila Sasa Yale ya zamani Huwa yanaenda wapi?

Kimsingi Serikali hutumika Bilioni 550 Kwa ununuzi wa magari,vipiri,matengendzo na Mafuta.
 
Yale yaliyopo vipi yamechoka ? Kwa mwendo huu itabidi tuanze kufikiria jinsi ya hawa jamaa kununua magari wanayotaka wenyewe kutoka kwenye mishahara yao Gari za kununua zibakie ambulances, Fire n.k....

Hawa watumishi wetu wanatu-cost sana aisee....
 
Wilaya hizo ni zipi na je ni wilaya iliyo ktk mikoa iliyolengwa ya kujazia kura kujihakikishia CCM inapata kura nyingi kupitia presha na ukada wa maDC hao

56 x 470,000,000 = 26,320,000,000

Mchengerwa ametoa taarifa hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo April 16,2024 wakati akitoa hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2024 /2025 ambapo amesema shughuli zitakazotekelezwa katika utawala bora ni pamoja na ununuzi wa magari 9 ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Mikoa ya Katavi, Njombe, Iringa, Kigoma, Mwanza, Singida, Dar es Salaam na Manyara”
 
Gari ndiyo zinahudumia wananchi?
Hakuna maji ya uhakika
Umeme
Dawa hospitalini
Watoto wanakaa chini mashuleni
Mazao yanaharibikia mashambani
Wewe unajitia midole hapo lumumba huku ukiwa umevimbiwa kwa rushwa na unabana pua ati NDIIYO VYEMA. akili zipo za kutosha kweli? Au ni kama yule chizi anayeombewa na pengo kila siku?
Hao wanaokwenda kusikiliza hizo changamoto gari zitawarahisishia kufika kusiko fikika!
 
Unakideri wewe, mtu yeyote nayejadili ni CHADEMA?

CHADEMA ilishakufa toka 2017 baada ya wabunge wake kununuliwa na mnnuaji.
2020 ikafa rasmi haina mbunge , sasa hao unaosema CHADEMA ni wapi ? Mbona nyie UVCCM hamusemi hawa watakuwa ni CUF, ACT,NCCR, NLD, UPDP vyama hivi si vipo?

Ndio. Wanaoleta mabandiko ya magari ni CHADEMA.

Wekeni sera zenu wananchi wawasikilize, na sio porojo zenu. Kwani Erythrocyte ni CUF au UDP?

Kama unataka kujua athari zake, subiri CHADEMA wagawiwe(hawachaguliki) nafasi chache Serikalini 2025. Endeleeni kujenga haya mazingira.

Kideri mwenyewe😌😌😁
 
Upo sahihi kabisa:
Kwa miaka 65 sasa, Sera za CCM ni zipi?
CHADEMA wamesema KATIBA MPYA.

Tuelimishe za CCM.
 
Kupanga ni kuchagua, kipaumbele cha chama changu cha mapinduzi ni kufadhili maisha ya anasa kwa viongozi wakati mambo ya msingi yanatushinda. Sad.
sio tu kushindwa yanatafutiwa visingizio lukuki ili yashindwe kufanyika 😂 ila kumlipa mzee Toyota billion 50 aingize hio mikoko umatumbini ni chap sana 😁
 
Iko ivi hayo magari yananunuliwa kwa mujibu wa sheria na katiba tulionayo,hata ww ungekuwa raisi usingezuia ilo,
Shosti unapuyanga , Katiba ipi inazungumza kuhusu magari ni ibara ipi?
Nimekaa mahakamani miaka 25 katiba ipo kwenye finger tips, Sijawahi kusoma hiyo.
 
Back
Top Bottom