MAGARI YA UMEME: Fahamu Faida Zake, Aina na Namna Yanavyofanya Kazi

Mkuu upo dunia gani? Mbona sa izi kuna magari ukiwa ndani husii hata mlio wa gari
Dunia hii hii mkuu labda wewe mwenzangu upo kwenye space... gari gani hio husikii mlio yenye kutumia diesel au petrol?

ebu skia hizi



 
Hivi magari na viwanda kitu gan kinachafua mazingira zaidi....wazungu wanakomaa na magari wakati wanajua viwanda ni balaaa
 
Mchina anawacheki tuu...yakifika huku anatuletea PowerBank hataki masikhara kabisa
 
Mkuu Kila kitu Duniani kinatoka Ardhini. Chuma mchanga Malighafi za kutengeneza Sement nk lakini hatujaona huo Uharibifu mkubwa wa Mazingira ili Hali Kuna majengo Mengi Duniani kuliko idadi ya Magari Yote yatakayowahi kuwepo
 
Viwanda vinachafua mazingira saaana mkuu.

Nadhani hawa jamaa hua wana mission yao.
Kwa sasa biashara ya magari ina faida kubwa sana na inakua kama ulemavu flan aanautengeneza. Magari ya zaman yalikua na uwezo wa kudumu hata miaka 40 katika mazingira magumu na garama ndogo za matengenezo kama LandRover 109, staut,Isuzu injection, n.k ila ya sasa kila kitu umeme hivyo kuyafanya kua delicate sana.
Gari ikifika KM kadhaa basi haifai tena mana itakutesa sana na utanunua spea kila siku
 
Mkuu Tesla na makampuni Mengine wanawekeza kwenye nishati mbadala ya Jua Upepo na maji. Kwa Hiyo wanajenga charging stations nyingi kwa Kutumia solar panels hasa Tesla. Kikubwa Ni kuwa wanaandaa Mazingira mbadala baada ya mafuta kuja kuisha huko mbeleni.
 
Duu nimecheka Sana
 
Kama nakumbuka vzr hata mbuga ya kruger ya S/Africa wali convert landcruiser wakaifanya ya umeme wakaenda nayo porini,aisee ilileta taharuki kubwa sana kwa wanyama maana walikua wanajiuliza ni kitu gani hiki kinatembea bila ya sauti maana wale wanyama walishazoea magari ya diesel/petrol,mwishowe wakaachana na mpango wa matumizi ya gari za umeme huko mbugani.
 
Hahahahahah aisee ...kwa hiyo wanyama walikua wanajua hiyo..L.C Hardtop' hiyo LR defender ....sasa wakashtuka balaa kitu hakina mlio
 
Sasa wao hawanunui gari kwa sababu ya sauti. Maifa mengi ya ulaya yanahamia kwenye electric cars
 
Ishu ni kudai kuwa wanatunza mazingira kupitia hizo electric cars. Lakini upatikanaji wa hio lithium battery ni worse kabisa na inatumia precious resource ambayo ni muhimu kwa viumbe hai, shughuli za uchimbaji wa lithium zinatumia MAJI mengi mno. Moja kati ya athari ya uchimbaji lithium wanasema inaweza kusababisha ukame!

Besides, kweli ukae karibia lisaa kujaza chaji betri yako? unapoteza precious time
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…