MAGARI YA UMEME: Fahamu Faida Zake, Aina na Namna Yanavyofanya Kazi

Teknolojia zinabadilika.

Kuna documentary nimeona wanafanya tafiti ya teknolojia ya kutumia graphene kutengeneza battery ambazo zina last muda mrefu kuliko hizo za lithium.

Electric cars is the future. Ni suala la muda tu teknolojia ya battery itakuwa bora zaidi.
 
kwa TZ tuwe na campaign ya kufunga nishati ya Gas. miaka ya nyuma tulitamgaziwa tupeleke magari watufungie hiyo mifumo na vituo vikajengwa vya kujazia gas sikumbuki iliishia wapi hii campign sijasikia tena.
 
hii habari ni pigo kubwa sana kwa nchi ambazo uchumi wake unategemea mafuta na baadhi ya nchi za Africa ambapo mafuta yanazidi kugunduliwa. hata viwanda vingi kwa sasa duniani vinaelekea kwenye mifumo ya gas kujiendesha. technologia inabadilika kwa kasi sana dunuani.
 

Petrol station kuweka vituo vya kuchajia magari hawawezi,ni threat kwao.
 
Niliona Documentary kule youtube,kuna nchi hapa E/Africa wao wamepiga marufuku pikipiki za kutumia mafuta wanataka za umeme tu,so wameamua kufanya majaribio kwny mji mkuu wao kwanza na kuna Co. Ya kimarekani imepewa hio Tenda.

Pikipiki hizo battery yake inaweza kutembea km 150 ndipo inaisha chaji,then hio Co. Ya Kimarekani ina vituo sehemu mbalimbali hapo mjini ambako pikipiki ikifika inabadilishiwa battery ndani ya dakika 1 inawekewa battery iliyojaa then inasepa zake inaacha hio,hakuna muda wa kusubiri kuchaji battery.

Labda model ya dizaini hii ingeletwa na kwny magari kama installation za battery hizo kwny gari zingekua ni rahisi(kitu ambacho najua ni vigumu kwa nature ya gari za umeme zilivyo).
 
But Pia mkuu upo uwezekano wa Kujaa betri kwa dakika 18. Sioni Kama Ni kupoteza Muda hata ingekuwa lisaa limoja kwa range ya 500+ km.. Sababu siyo Muda wote gari inatembea.
 
Tafiti ndio hazija maliza, kwa sasa wanatumia lithium na wanaendelea kuproduce lithium batteries na kuharibu mazingira vile vile.

Kweli wanataka battery iwe future.

Kuna swali najiuliza, hivi gari za electric zinapotembea wakati yale maringi yanazunguka kwanini hayarudishi chaji kwenye battery?
 
Hio Idea ni nzuri lakini battery zina degrade. Atakuja mtu aweke battery yake ishaanza kufifia. Unapewa battery fully charged lakini unaona unakwenda short distance
 
Shida kubwa kwa Tanzania ni hii teknolojia kuwa mpya, si kwa EV tu hata hizi hybrid. Hebu jaribu nenda kwa fundi wako muulize nataka agiza Prius ana maoni gani uone atakavyo kujibu.... Bila shaka atakwambia gari mbovu zile... Hazitengenezeki nk uvivu wa mafundi wetu ndio unapelekea tunaendelea ishi na teknolojia ya zamani. Mfano mwaka huu ni 2021 eti unaenda nunua toyota starlet ya mwaka 1999 na wewe unvimba barabani una gari, kweli? Au sababu fundi wako alikwambia gari hilo ni gumu (sijui ukigongana haliumii) na lina injini nyepesi kitengenezeka? Huwezi fanana na mtu alie nunua toyota ractis ya mwaka 2012 japo gari ya 2012 kwa wenzetu ina teknolojia ya zamani lakini kwetu utaitwa una "new model" lakini uko watembea na teknolojia ya kisasa ya gari yako na usalama wako, gari za kisasa zina mifumo mingi ya usalama, ulaji mzuri wa mafuta (economy) comfort nk.

Nashauri watanzania tubadilike, tukumbuke gari halijaumbwa kupigwa au kugongana eti utaskia makaratasi yale, ukigongana hiyo ni ajali, kwenye ajali safety features za gari huwa ni kumlinda mtumiaji wa gari atoke salama sio gari lisiumie, endeleeni kutumia magari yakigongana uso kwa uso dereva ana banwa na steering.

Kabla hatujaamua kuanza na EV sababu ya upungufu wa charging stations (kwa east africa kuna fast charging station iko chuo cha makerere Uganda tu) basi tununue hybrids mf toyota aqua... Hichi kidudu kipo poa na bei ya kawaida tu
 
Hio Idea ni nzuri lakini battery zina degrade. Atakuja mtu aweke battery yake ishaanza kufifia. Unapewa battery fully charged lakini unaona unakwenda short distance
Uzuri ni kwamba zile battery zote ziko owned na Co.,so kwa case yoyote ile ni mtu anaipeleka hio battery karibu na kituo kilicho karibu nae wanabadilisha chap then nduki
 

Nazipenda prius/honda fit hybrid(kwa ajili ya matumizi ya mafuta),ila mafundi wa kibongo kwa kukatisha tamaa wako vzr.
 
Kwahiyo imeshindikana kabisa kuundiwa jiko ili betri ijichaji pale gari ikiwa inatembea!?
 
Kuna gari za hybrid zinacharge battery zake.
 
Kuna gari za hybrid zinacharge battery zake.
Simaanishi hio system ilokuwemo kwenye hybrid, nazungumzia full electric car. Wakati maringi yanazunguka, kwanini mzunguko wa hayo maringi usitumike kuzalisha umeme na kurudisha chaji kwenye betri? Windmill inazunguka ndio inatowa umeme, Hydro Elctric Power turbines zinazunguka na kuzalisha umeme, vipi maringi ya gari yanazunguka lakini hayazalishi umeme?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…